Maelezo haya mazuri ilipaswa yawe sehemu ya posti yako ya kwanza, Hakika flow ya comment ingekuwa nzuri na kwa kiasi kikubwa ungefanikiwa kufikia lengo la kuweka tangazo.
Kiukweli hadi muda huu naandika hii comment bado sijaelewa nini hasa huduma yako.
Ushauri.
Tulia soma comment angalau ishirini za kwanza, kisha tumia hizo comment kama sehemu ya kuboresha posti yako ya kwanza, Tangazo zuri halihitaji haraka.
Mfano hai: Angalia hili tangazo langu hapa:
Nunua bidhaa kutoka Mataifa 15 ikiwemo USA, UK, UAE na China sasa
Tangazo nimeweka 2016, content inaelewek na ni valid hadi ssa.
Ombi: Rekebisha post ya kwanza, utaona comment za wadau zikiwa na mashiko.
Ni hayo tu. Sio kwa ubaya bali kukusaidia iwapo hata unaweka tangazo lingine tumia muda mwingi kupangilia na kulihakiki vyema.