Nimesha subscribe ngoja nipitie nyuz zngne huku ntaja sio muda ,yanayonikuta kwa mtoto wa kichagaaaa
Nimerudi sasa niwape ka kisa kadogo kwa ufupi yaliyojiri, miezi kadhaa nlikuwa na mtihani wa programming chuo Fulani katikati ya nchi ,
Wakati naingia kwenye hall ya mtihani ,nikabahatika kukaaa nyumaa .... Mbele yangu alikuwa amekaa mdada aliesuka Nywele za gharama na anaonekana ni wa kishua kabisaa, basi nikamshika bega nikamuambia "ntaangalizia kwako" akacheka akasema sawa ,ile wakati anageuka sasa ndonikaona kuwa alikuwa binti mkali mlaini soft mwenye tabasamu mwanana na kwa kuwa nliingia hall kwa mlango wa nyuma hivo Mara ya kwanza sikumuona sura lakini hapo ndonikamuona alivo kisu .
Paper limekuja likawa ni multiple choices tu so nikajaza chap ,likaja karatasi ya kusaini nikacheki mtiririko wa majina nkaja gunduaa ni mchaga mmojaa.
Nikanote jina nikasain na kwa kuwa mie ndo nlikuwa MTU wa mwisho nikabaki na ile sheet ya kusaini hadi navoenda kusanya ile paper nikaenda kurudisha kwa mwalimu.
Msako wa kujua anasoma kozi gani ukaanza chapu na kutafuta namba yake ,basi kuna jamaa yangu akanisaidia kucheki kwa course zote zinazosoma programming at the end tukaipata kwa Dada mmoja lakini naye akaanza kudoubt kwamba tunaitaka ya nini mwisho we akamgey jamaa then jamaa kanipigiaaa pasi ndevuu nicheze na nyavu.
Nikamtext yule Dada kwa WhatsApp akaja nijibu kesho yake,hakuwa online kwa siku hiyo nzima ,nikamuambia a to z na lengo langu ..... Akaanza ni avoid sasaaa hapo ndo mchezo ukaanzaaa.
Kuna siku Niko na jamaa yangu mwingine katika kujiongelesha kumbe huyo Dada nae ashawahi mtokea ,na ile story yangu akawa anaiskiliza huku ananichora akaja nipanga huyo unaemsemea ni Fulani akataja na sifa zake na kumbe ni kweli ni yeye, jamaa akanambia huyo dogo haeleweki mnaweza mkaongeaa vzuri Leo kesho akija mnaanza alifu tena.
Basi akanitiaa moyoo, pambana ,.....siku moja tumetoka class mie huyo jamaa na cozi zingine nyingi kwakuwa hilo somo tunashare watu wengi,basi akasema jamaa yangu ngoja nikuitie huyu Dada mmalizane maana kama SMS hajibu hapa ndopenyewe .
Sikutaka iwe hivo kwa kuwa yule Dada angetushtukia kuwa tunapasiana ,ye kamchomoa jamaa na jamaaa kanipasia na mie nijaribu ,kitu ambacho mie cikukipenda lakin ckutaka kumuangusha jamaaa ,basi pindi limeisha ndotunasepa sepa mie namvizia yule Dada Mara paaap cjui kapitia mlango gani nakuta yuko mbele yetu ,jamaa yangu kasema nimuungiee ,ckutaka nionekane mnyonge nikaendaa, nikamuita Xxxx akashtuka ,nikampa hi akaitikia lkn kam MTU Fulani anaye shangaa ,nikamwambia usiogope ,nikatoa simu nikamuonesha chatting zetu ,nikamuuliza hii namba unaijuaa akasema kama naijuaa ndioo nkasema ndo Mimi naekusumbua ,akacheka ,akasema sawa saiv naenda kula tutaonana badaeee,tukaagana.
Bahati mbaya nimeenda kula sehem ambayo nayee kaenda kula ,akaniona na yule jamaa ambaye nae alimtongoza kitu ambacho mie ckutaka ajue kuwa tuna urafiki nayee,basi hapo nikaanza kuona naelekea kuharibu basi.
Maisha yakaenda test Nazo zmepamba ,nikawa nikimtafuta hajibu text ,nkaaamua nishirikishe room mates wangu basi tukaandika scripts pale,....... Mmojawao akanambia usimkurupukiee we nenda nae taratibu ,labda hataki kuonekana wa Maji mara1, basiii siku ikapita.
Nikawa namtafuta Mara moja moja tunachat tuna textiana lakin ni hadi nimuanze,......... Nkaja kumbushia jambo langu ...akazugazuga weeee akanambia sijui nini am sorry kwa hilo ,..
Till now sijamtafuta ,hajanitafuta japo kuna muda natamani Fanya hivoo ila nahic nalazmisha sana mambo alafu ye hayuko interested nami. Basi nikawa namuona tu class akiwa disc na last time nimeonana nae juzi kwenye UE ya programming nika assume sijawahi ijua ile sura.
Samahani kwa story ndeeeefu ,japo kuna vitu sijaandika humu.