Unapenda movies? Pitia hapa kidogo

Tungoje msaada...

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Wewe ni mwandishi wa vitabu? Sijui soko la vitabu likoje lakini wewe ni mwandishi na mchambuzi mzuri sana. Nimevutiwa namna ulivyozichambua movie hizo. Nitatafuta moja baada ya nyingine nisione

Sent using Jamii Forums mobile app
Mimi ni mwandishi mkuu, mwanafasihi, mchambuzi wa filamu na pia mwanahabari huru ninayejitegemea (a freelance journalist).

Pitia na post #45 kuna movies za ziada. Hakika hutajuta.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Katika movie za hivi karibuni maze runner ile ya kwanza kabisa imebaki kuwa muvi yangu bora kabisa....mkuu ingependeza kama ungenijulisha muvi zenye mfanano na maze runner
Me nime angalia Maze runner zote, naona ziko vizuri Yaani zile hekaheka ndo zinazonifurahisha

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hiyo Papillon niliona documentary yake, jela aliyokuwa amefungwa huyo jamaa ipo kwenye kisiwa cha devil island French Guinea ambacho kwa sasa ni kituo cha utalii kwa wale watalii wanaopenda kurandaranda na cruise ships.
Huwa wanaenda kuangalia cell ya Papillon na aliandika jina lake sakafuni.


Sent from my iPhone using JamiiForums
 
Kuna movie inaitwa interstellar nimeiangalia sijaielewa hata kdg
Sent using Jamii Forums mobile app
 
Jamaa alikuwa mwamba sana.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Hapo pet sementary pekee ndo nimeiona kijana una madini
 
hizi movie kwa uchambuzi wako nimezielewa sana nipe namna ya kuzipata (kuzipakua ) nifanye kweli usiku huu
 
Kuna movie inaitwa interstellar nimeiangalia sijaielewa hata kdg

Sent using Jamii Forums mobile app
Nini hujaelewa mkuu? Mbona ipo clear. Bwana mmoja, mwanasayansi wa mambo ya anga, anapewa kazi maalum ya kutafuta makazi mapya ya binadamu baada ya dunia kukumbwa na uhaba mkubwa wa chakula kutokana na majanga ya asili kama vile ukame na vimbunga.

Kutokana na majanga hayo kumekuwa hakukaliki hivyo NASA wanafanya namna kutafuta makazi mengine ambayo yatamkidhi binadamu mbali na dunia wanayoishi. Lakini sabb ni hatari kupeleka watu wote kwa mkupuo maana hawana taarifa zaidi kuhusu huko, ndo wanaamua kuwatuma baadhi.

Filamu hii inachanganya kidogo maana inahitaji uelewa wa mambo ya sayansi ya space. Nadhani uliona mambo kama vile wormhole na dimensions. Sasa Wormhole ni njia za kinadharia ambazo zinaaminika zinafupisha safari ndefu za mambo ya anga za juu, yani kama vile shortcuts kwenye space. Na ndo hiyo wanayoitumia wanasayansi hao kufikia huko kwenye ulimwengu mpya wapate kuona kama pataweza kalika.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Nipe tofauti Kati ya hizi thriller movie na horror movie
Thrilller mara nyingi huwa na mambo ya kiuwerevu, uhalifu, udadisi na ujasusi na visa vyake husababisha kimuhemuhe (suspense).

Horror lengo lake kuu ni kuchochea hofu, woga na mshtuko.

So unakuta muda mwingine movie inaweza ikawa horror na pia ikawa thriller. Mfano MARA.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…