Unapenda Paka? Tupia picha ya Paka wako tumuone

Unapenda Paka? Tupia picha ya Paka wako tumuone

Vishu Mtata na Mbaga Jr OKW BOBAN SUNZU mna maoni gani wazee wa u much know
🤣🤣🤣Hata mi napenda paka ndgu yangu ila tu asiwe mkubwa.
Na nina bahati nao sana, huwa wananikubali mno na najua kucheza nao wakafurahi.

Paka akiwa mkubwa afu dume huwa yanakua mabaya kishenzi.

Toka nakua home tunafuga paka.

Mnyama nisiemkubali ni dogi, sinaga imani na yule mwamba.
 
Paka wangu washenzi sana,, hawajai kutulia nyumbani hata uwape nini, kutwa kiguu na njia nadhani wanatafuta mademu maana ni madume tupu
Humlishi vizuri, kama kwako anakula vizuri, unakaa nae mda mrefu wala hawezi kuzurula.
Kama ni pisi basi vijamaa vitakua havikauki hapo. Usiku utakua unakereka na ugomvi wa kugombea papuchi.
 
IMG_20231229_124034_44.jpg
 
Kuna mmoja alinilia vifaranga vyangu na ninamlisha daily aisee nilimpigia Buti Moja akapaa kama sita hewani sijawahi muona mpaka Leo
Mdogo wake Kuna siku nimeandaa kambale wangu naenda dukani kuchukua unga wife alikua kasafiri narudi napishana nae mlango wa jikoni nimesonga ugali kucheki kitoweo hamna

Nilimpigia na mpini wa jembe naye akayeyuka kusikojulikana ila usiku nahisi wanakujaga maana nasikia wanalialia Sasa sijui wanazagamuana au vipi
😂😂😂 we jamaa katiri sana
 
Mimi pia paka kama siwaelewi, wana viburi sana. Halafu huwezi kujua mood yake kama amekasirika ama anafuraha, yeye yupo tu.

Ni tofauti na mbwa, mbwa akikasirika unajua, akiwa ana huzuri ama mawazo ama stress kwa mfano ameachwa na mke wake ama mume wake ama mchepuko unajua na akiwa na furaha unajua mapema tu.

Binafsi Mbwa is my favorite hasa hawa local breed. Ni washkaji sana.

Paka akae mbali na mimi.
Local breed, nampiga misosi ya kutosha na afya inazingatiwa kwa wakati, balaa sana.
 
Home tulikua tunasumbuliwa sana a panya,one day nikaenda kwa mshikaji wangu nikakuta paka wao kazaa,nikachukua kitoto cha paka,hadi leo nyumbani paka ndio mnyama pendwa ndani ya nyumba,hiyo ilikua 2007.na hakuna panya home
 
Back
Top Bottom