Unapoanzia uchawi ndipo sayansi inapoishia

[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
 
Reactions: uth
Dunia inamambo ndugu walininyima raha na amani ila kilikuja kurudi lkn kwa tabu maana nilizimishwa kama masaa 6 watu nimekufa lkn niliamka tena na hapo nilivyotoka nje nikajikuta kivuli kipo. Uchawi upo mkuu
Duh pole sana
 
Reactions: uth
Wakuu, si kweli hata kidogo kuwa unapoanzia uchawi ndipo sayansi inapoishia!!, kimsingi uchawi (hypnotism /mesmerism) ni sayansi, ni field moja kati ya field za sayansi, chukua mfano zama za Issack Newton hadi katika miaka ya 1900 hivi Newtonian mechanics ilikuwa inatawala sana lakini ilifika mahali kulingana na maendeleo ya sayansi duniani Newtonian mechanics ilishindwa kutanzua baadhi ya problems ndipo ikaja modern mechanics ambapo mambo mengi yakatanzuliwa na ugunduzi mkubwa ukafanyika lakini pia tukumbuke kuna mambo mengi leo hii bado ni nadharia tu kwa sababu sayansi ya leo bado haitoshi ku formulate ili kujua ukweli wake na hapa unakuja kuona mapungufu ya sayansi hii leo mfano, nini ni chanzo cha nguvu ya uvutano!!?, jibu lake lipo katika nadharia tu (Einstein general law of relativity ). Halikadhalika uchawi (hypnotism ) ni tawi moja la "elusive science" ambalo kulitanzua na kuliweka wazi watu wameshindwa kwa sababu hawako interested nalo, leo watu wako interested na mambo ya rocket,computer,machineries, nuclear science,nk mambo ambayo ni tangible.

Nadhani itafika muda "uchawi" utakuwa applicable pale ambapo sayansi ya leo itakaposhindwa kutanzua matatizo kama jinsi classical mechanics iliposhindwa na modern mechanics ikachukua nafasi. Hapa tunazungumzia uchawi wa kuleta manufaa (productive) sio ule wa kuua watu nk.
 
CC : Kiranga with due respect
 
Reactions: uth
I like ur argument
 
Bro Mshana jr, hebu nisaidie hii tofauti. Je si kwamba uchawi unahusisha imani ya giza na hufanywa hadharani na faragha na dini nayo inahusisha imani ya nuru na pia hufanywa hadharani na faragha ? Na je sayansi si si ile hali ya kutafuta urahisi katika kurahisisha shughuli za binadamu za kila siku ? Na hapa binadamu anaisumbua akili ili kila muda unavokwenda anajitahidi kurahisisha shughuli zake kwa kutumia zana tofauti anazoboresha kila muda unavyoenda. kwa hiyo hapa binadamu anategemea ubongo wake na kwenye imani anategemea nguvu ilio nje yake kwa kujiunganisha nae kupitia sadaka. wadau mtanisahihisha
 
Hebu msome Mokaze post number #226..... Amejibu kwa weledi na ufafanuzi wenye maarifa mengi
 
Reactions: uth
Bro nimemsoma, ni kwamba nilihitaji kufahamu ni kwa nini basi hizi imani zinakinzana kuanzia kale. lakini sayansi hii ya kawaida inashirikiana au kutegemeana kwa ujumla wake ? mwongozo kidogo tafadhali
 
Reactions: uth
Bro nimemsoma, ni kwamba nilihitaji kufahamu ni kwa nini basi hizi imani zinakinzana kuanzia kale. lakini sayansi hii ya kawaida inashirikiana au kutegemeana kwa ujumla wake ? mwongozo kidogo tafadhali
Hazikinzani hizi ni tafsiri tu za watu ndio zinaleta ukinzani... Ni sawa na shilingi huwezi kuitazama pande zote mbili kwa wakati mmoja, ukijaribu kufanya hivyo ndipo ukinzani unapokuja
 
Nimekupata bro. baadae meeting .nawaibia muda wao kidogo
 
Reactions: uth
Sawa BABU tangazo lako tume liona
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…