Unapoanzia uchawi ndipo sayansi inapoishia



Zongo liko popote na kwa yeyote. Je unajua ya kuwa hata mwanao wa kumzaa unaweza kumpiga zongo bila kujua yaani kumdhuru kupitia macho.


Zongo ndio kijicho.
 
Nakubaliana na wewe mkuu,

"sayansi inapoishia ndipo uchawi unapoanzia"

1. Hii ya mtu kutumia macho kumdhuru mtu mwingine kwa kutumia mionzi isiyoonekana ushahidi wake mzuri ni bluetooth jinsi inavyofanya kazi, mtu ili apone ni lazima adisconect na hio mionzi, manabii wanaijua vizuri hii mechanism pia waganga na wataalam ndio maana kupona kwake ni kwa ghafla tu na kuumwa kwake ni sekunde chache tu.

2. Sayansi ina wachukulia watu wenye majini kama wagonjwa wa akili, ni kweli kwa sababu dalili zote ni kama za wagonjwa wa akili, (mwisho wa sayansi)

Lakini inasemekana kuwa ili uweze kutabiri yajayo, kuona vitu visivyokuwepo, kumfahamu nje ndani mtu usiyemjua ni lazima upitie ktk hali ya ugonjwa wa akili ndio utaweza kufanya hayo yote,
Ushahidi mzuri ni mtu au mganga akipandisha mapepo huweza kuona kile unachokifikiria ktk akili yako kwa kufanya connection kama jinsi ambavyo bluetooth inavyo connect, hapo anakuwa kadukua mawasiliano ya fikra zako, kisha anaanza kukusoma na kukueleza A to Z na kuchomekea maneno kadhaa ya uongo ili umuamini na apige mpunga, hii connection hufanyika kupitia kiganja cha mkononi au paji lako la uso,

Sayansi inapoishia uchawi ndipo unapoanzia
 
Nifundishe chumaulete mkuu[emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
najaribu tu kufikiria hii sayansi yetu ya kienyeji sijui iko vipi? kwa mfano mchawi ana uwezo wa kuingia ndani kwako hilo hatubishi, sasa kwa nini hawezi kuchukua kitu ama hela zilizouko mezani ama kabatini, simu ama laptop?
 

Duh
Wanaingiaje?
Mtu anawezaje kuwazuia wasiingie chumbani, nyumbani au hata kufika eneo la nyumba kwa nje?
 
Kwa uelewa wangu lakini,

Uchawi ni connection kati ya mtu na mtu, mtu na mnyama,

Na sio mtu na kitu,
Pesa ni kitu pia mitihani ni kitu.
Mchawi hawezi kuconect na kitu.

Badala yake, mchawi anauwezo wa kuconnect na akili ya mtunga mtihani akajua kilichomo kichwani mwake, ikiwa atapatikana physically japo mara moja tu.

Hivyo basi mchawi hawezi kuiba pesa au mtihani.
 

Umetupanga mzee baba. nice
 
Duh
Wanaingiaje?
Mtu anawezaje kuwazuia wasiingie chumbani, nyumbani au hata kufika eneo la nyumba kwa nje?
Wachawi hufanya mambo kinyume
.. Huingia uchi
.. Huingia kinyumenyume
.. Huingilia kwenye pembe za nyumba hasa kushoto
Mchawi hapatani na vitu vyenye ugwadu na harufu kali kwahiyo ukiwa na ndimu kitunguu saumu na chumvi ni kinga tosha kabisa.... Kwa wale waamini na waaminio kinga na tumaini lao kubwa pamoja na hayo mengine yote ni Yesu Kristo kupitia damu yake takatifu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…