Kuna dada mmoja ofisini alikuaga anaongea kama wewe dada Karusii. Unakuta tuko wengi ofisini sasa si unajua tena stori watu wanaanza kuongea kuhusu michepuko basi yeye ataanza kukemea, anakua mkali...! " Ooh, mtu umeoa/olewa utakuaje na mtu mwingine..?" "Mapenzi ni kwa mtu mmoja tuu..." " Penzi haligawanyiki.." "Haiwezekani mtu mwenye akili timamu uchepuke.." Yani alikua anakasirika hadi anaondoka kabisa hilo eneo.
Basi bana... ikafika kipindi tukapataga kazi fulani ikawa ni lazima mimi na yeye tuwe tunabaki ofisini kila siku kuifanya kwenye computer. Kusema kweli mimi nilikua na behave vizuri tuu sema sasa ile kukaa wote karibu kwa mda mwingi mpaka usiku, tukajikuta tunaanza kuongea mambo mengi, saa nyingine tunakula pamoja, mara tumeshikana mikono, mara kaniegemea, siku isiyo na jina mara hamad! Tumekiss!!!
Tuseme tu ni zaidi ya miaka minne sasa tunaendelea kumegana kwa siri sana..! Binafsi nimeshafanya effort kadhaa za kuvunja uhusiano lakini mwenzangu akiona tu dalili kama nataka kumpotezea aisee anakuja juu balaa hataki kabisa kusikia!
Kwahiyo haya mambo yanatokeaga tu sometimes wala hatupangi.