Unapoongoza elewa kuwa wewe ni kiongozi tu! Tabia za kufokeana Kama watoto peleka Kwa watoto wako nyumbani

Mbona kama umechefukwa? Usilie ndugu yangu
 
Daah yaani inaelekea hujawahi kuwa kiongozi hata wa kichwa chako ( sijatukana wakuu tunaeleweshana) kuna wakati unafanya makosa mwenyewe mpaka unatamani ujifoke. Sasa uko kwenye kazi ufanye makosa halafu mimi kiongozi wako nikulee lee tu hapana nitakufokea ila pia kufokea ina taratibu zake siwezi kukufokea mbele za watu au wafanyakazi wenzio nitakuita chemba na kukufokea hata kama una mwili kama mh Wassira nitakufokea tu. Uongozi ni mgumu sana ndugu.
 

Na Hilo ndilo ninalolisema!

Upo sahihi!

Nimeandika ujumbe huu Kwa watu wenye tabia hiyo, utakaowaumiza ndio wenye tabia ya kufokea watu bila adabu mbele za watu
 
Haka ka utamaduni ka kufokeana si kazuri, kalianza rasmi 2016 - Wote ni watumishi wa umma sasa kunifokea fokea kisa wewe eti ni bosi ni USHAMBA tu...hata mkeo pale home ukimfokea fokea ujue hizo siku mbili unyumba kwa jirani...
 
Nakwambia hivi, una bahati!
 
Haka ka utamaduni ka kufokeana si kazuri, kalianza rasmi 2016 - Wote ni watumishi wa umma sasa kunifokea fokea kisa wewe eti ni bosi ni USHAMBA tu...hata mkeo pale home ukimfokea fokea ujue hizo siku mbili unyumba kwa jirani...

😀😀😀

Mfokea mtu Kwa adabu.
Kwenye vikao, au chemba.

Lakini kufoka na kubagaza watu mbele ya halaiki Kwa kweli Hilo haliwezekaniki.

Hata Baba mwenye hekima hawezi mfokea mtoto wake mbele za watu ati ili apate sifa Kwa majirani.

Au mke umfokee mbele ya watoto au majirani alafu Kama anajielewa akuchekee bila kurejesha mapigo.
 
Hapana!

Embu fikiria Taikon napewa kacheo Fulani alafu nakuja kumfokea Baba yako au mtu aliyelingana na Baba yako ambaye kanizidi Hadi Mimi umri.

Huko ndio kuvurugwa

Ila Makonda alikuudhi sana.
 
TRA inabidi wachapwe viboko kabisa.
 
TRA inabidi wachapwe viboko kabisa.
hahaaa kuna bosi wao mmoja wa zamani ila katumbuliwa sasa hivi anafoka huyo hahaaaaa tena bila staha , ooh mimi nina Phd ya kwiyooooo mxiuuuuuuuuuuu
 
Hongera wewe umestarabika.

Wenzako hadi wapigw eza vichwa ndio waelewe.
 
Watoto wa kigitali wanachekesha sana, anafokewa Baba/Mama Mzazi ije kuwa ndezi wa Mchambawima ulete ujinga ujinga eti kisa hutaki kufokewa?

Kuna hasara zingine hupotea kizembe sana ikiwa mfanyakazi atakuona jinsi gani wewe Bosi ulivyo bwenyenye kwa kila kitu kukiendesha kipoa poa (leissezafair leadership styles).
 

Ndio uanzishe hiyo Kampuni yako ili ufanye hayo hakuna atakayekuingilia lakini sio kujifanya unajua kufoka kwenye mambo ya Kisiasa huku ukijua wote ni wamiliki WA nchi hii.

Upo utaratibu wa kumfokea mtu na sio mbele za watu kwenye mambo ya kitaifa.

Hakuna atakayekuzuia kumfokea Baba au Mama yako, au Mkeo au watoto au Wafanyakazi wa taasisi au Kampuni yako lakini kwenye ishu za kinchi ujipange
 
We jamaa ulikuwa na duka kihonda Moro?
 
Maada Nzuri sana.
Ila mbona andiko lako umeliandika kwa Kufoka na wewe pia Mkuu?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…