Unaridhika na Mwenza uliyenaye au unavumilia tu?

Hapo kwenye haishi hamu wala utamu ndo nimepapenda 😜
Kabisa,yaani wanawake huko nje wakitaka kunitega,ghafla huwa naukumbuka utamu wa Mke wangu. Bila kujali urembo(uzuri) wao,huwa wanashangaa tu wamekula block!.

Kuna Mwanamke mmoja juzi juzi hapa amenijia na gia ya kutaka ushauri wa kiroho kwangu kumbe hamna cha kutaka ushauri wa kiroho wala nini. Kala block😀. Uzuri nia halisi ya mtu huwa haijifichi. Huwa wanafikiri Mimi ni kipofu kama wao. Sikia,Yesu alichokisema 👇

YOHANA 8
12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.

Mke/Mume wa kushushiwa na Mungu anapaswa kutunzwa,yai likasome!.

I always tell my dear wife kwamba "kwenye maisha haya utakutana na karaha nyingine tu za kimaisha lakini sio karaha za Ndoa. Kula raha za Mumeo mama". Huwa anareply kwa mng'ao wa tabasamu usoni mwake!

Kuna watu wanatamani kumroga kwa wivu lakini harogeki kwa sababu ana full protection(Jesus Christ) so, huwa wanaishia kumnunia tu na kutokujibu salam zake🤣🤣🤣🤣🤣.
 
Hakuna mwanadamu mkamilifu kila mmoja ana upungufu hapa ama pale. Unachotakiwa kufanya ni kutafuta ambaye ana mapungufu ambayo unaweza kuhimili muanze maisha.

Kurafufa ambaye utaridhika kwa kila kitu basi ushike udongo uumbe wa kwako ila si mtoto aliyetoka kwenye tumbo la mwanamke.

Tukiacha maisha ya kufikirika na kuangalia uhalisia, hayo mambo ya kutaka uridhike kwa kila kitu hayatakuwepo
Sahihi kbsa mkuu
 
Wakati mwingine tunajidanganya kwa jina la 'uvumilivu' wakati ndani ya moyo tumechoka.

Kuridhika ni amani. Ni kula na kucheka na mtu kutoka moyoni na kulala bila mawazo.

..........Lakini kuvumilia... ni kuishi kwa matumaini ya kwamba 'siku moja atabadilika'.

Tusidanganyane. Sio kila uhusiano unaodumu una maana. Baadhi yetu tumebaki kwa sababu ya woga wa watu watasemaje kutokana na muda tulioupoteza.

Lakini kumbuka, maisha ni mafupi sana kuvumilia mtu asiyekuthamini.

Kuridhika kunaleta tabasamu halisi.

Ulipoamua kupenda, ulitaka amani sio vita ya kila siku. Chagua unachoweza kuishi nacho milele, sio unachoweza 'kustahimili' tu.

Furaha yako pia ina thamani."
"Better to be alone and be happy, than being with someone and be unhappy"~Lucky Dube
 
Kabisa,yaani wanawake huko nje wakitaka kunitega,ghafla huwa naukumbuka utamu wa Mke wangu. Bila kujali urembo(uzuri) wao,huwa wanashangaa tu wamekula block!.

Kuna Mwanamke mmoja juzi juzi hapa amenijia na gia ya kutaka ushauri wa kiroho kwangu kumbe hamna cha kutaka ushauri wa kiroho wala nini. Kala block😀. Uzuri nia halisi ya mtu huwa haijifichi. Huwa wanafikiri Mimi ni kipofu kama wao. Sikia,Yesu alichokisema 👇

YOHANA 8
12 Basi Yesu akawaambia tena akasema, Mimi ndimi nuru ya ulimwengu, yeye anifuataye hatakwenda gizani kamwe, bali atakuwa na nuru ya uzima.

Mke/Mume wa kushushiwa na Mungu anapaswa kutunzwa,yai likasome!.

I always tell my dear wife kwamba "kwenye maisha haya utakutana na karaha nyingine tu za kimaisha lakini sio karaha za Ndoa. Kula raha za Mumeo mama". Huwa anareply kwa mng'ao wa tabasamu usoni mwake!

Kuna watu wanatamani kumroga kwa wivu lakini harogeki kwa sababu ana full protection(Jesus Christ) so, huwa wanaishia kumnunia tu na kutokujibu salam zake🤣🤣🤣🤣🤣.
Wacha bhana.
Upendo wa hivi ndo naoutaka mimi
 
Back
Top Bottom