Unasemaje kuwa umefunga wakati kila jioni unakula?

Unasemaje kuwa umefunga wakati kila jioni unakula?

Okay, nashauri tuendelee kufunga usiku badala ya mchana kama ilivyo asili ya mwanadamu, kuvimbiwa usiku ni mbaya kiafya maana unaenda kulala...
Kuna watu wanakula mchana kutwa na usiku pia wanakula chakula cha usiku (dinner) na wanavimbiwa.

Kulia sana mpk kuvimbiwa iwe mchana au usiku ni ulafi wa mtu tu.

Na kufunga katika uislam ni kujizuia na mengi (Sio kula na kunywa tu)

Ni kunyenyekea. Kukaa na njaa kutwa nzima na hali chakula unacho ni kwa sababu umefanya utiifu juu ya aliyoyaamrisha Allah.

Ukiona mtu baada ya maghrib anakula sana huyo ni mlafi tu.

Siku zote tunatakiwa kula kwa kiasi iwe Ramadhan au siku nyenginezo.

Na kwa Ramadhan tunatakiwa tule vyakula vyenye kutia nguvu na Sio kula chakula kingi.

Maana funga pia Sio kuacha kula ukasababisha mwili kuwa dhoofu ukashindwa kufanya kazi na kutafuta rizk.

Mnakwama wapi wenzetu mbona mambo rahisi kueleweka haya.

Swimu twasihaa-fungeni mpate afya. Hivyo ndio tulivoambiwa.
 
Salamu kwenu

Huwa siwaelewi watu wanaposema wanafunga wakati kila siku jioni wanakula.

Ninawafahamu watu wengi tu wanaofunga mpaka siku 21 kwa kunywa maji tu na kila siku wanaendelea na shughuli zao.

Mimi mara nyingi tu naenda mpaka siku saba bila kula na kazi nafanya kila siku.

Nadhani wanapaswa kutumia jina jingine lakini sio kufunga.
Tuonyeshe huyo anaefunga siku 21 kwa kunywa maji tu?
Kukaa Siku 7 bila kula ndio unajiona mtakatifu acha dharau na imani za watu wengine. Blalifaken!!!
 
Humu kuna wajinga wengi sana huwa nawapuuzia sana hasa Wasio Waislamu hutubeza ya kuwa tunabadilisha muda wa kula.

Sasa nakuuliza maana ya kufunga ni kujizuia kula pekee ? Huu ujinga amewaambia nani ?

Kwetu sisi Waislamu kufunga ni kujizuia kula, kufanya uovu, batili kuanzia alfajiri ya kweli mpaka jua linapo zama. Hii ndiyo maana ya funga kwetu sisi Waislamu.

Sasa unapotushangaa sisi na sisi tunakushangaa wewe kuhusu maana yako batili ya kufunga.
Achana nao mkuu watakuharibia funga yako.
 
Kuna watu wanakula mchana kutwa na usiku pia wanakula chakula cha usiku (dinner) na wanavimbiwa.

Kulia sana mpk kuvimbiwa iwe mchana au usiku ni ulafi wa mtu tu.

Na kufunga katika uislam ni kujizuia na mengi (Sio kula na kunywa tu)

Ni kunyenyekea. Kukaa na njaa kutwa nzima na hali chakula unacho ni kwa sababu umefanya utiifu juu ya aliyoyaamrisha Allah.

Ukiona mtu baada ya maghrib anakula sana huyo ni mlafi tu.

Siku zote tunatakiwa kula kwa kiasi iwe Ramadhan au siku nyenginezo.

Na kwa Ramadhan tunatakiwa tule vyakula vyenye kutia nguvu na Sio kula chakula kingi.

Maana funga pia Sio kuacha kula ukasababisha mwili kuwa dhoofu ukashindwa kufanya kazi na kutafuta rizk.

Mnakwama wapi wenzetu mbona mambo rahisi kueleweka haya.

Swimu twasihaa-fungeni mpate afya. Hivyo ndio tulivoambiwa.
Hao wanaokula mchana na usiku hao ndio hawajafunga sasa. Ila kiafya, usiku mwili unakuwa inactive, haupaswi kupeww chakula kingi, bali mchana wakati upo active ndio unapaswa kupewa chakula zaidi, its a simple health fact, tujali afya zetu.
 
Maji ya Nini brother...?? Me nawajua watu wanafunga 40 kavu bila kula kitu we unasema maji... Bado hujui kufunga na wewe tafuta neno jingine...
Hmmm, hao ni zaidi ya MUNGU wao YESU ambaye alionyesha udhaifu kiasi cha kutiwa majaribuni na SHETANI mara tatu alipokuwa amefunga kwa muda wa siku 40, hao ndo wafungaji sasa [emoji3]
 
Tuonyeshe huyo anaefunga siku 21 kwa kunywa maji tu?
Kukaa Siku 7 bila kula ndio unajiona mtakatifu acha dharau na imani za watu wengine. Blalifaken!!!
Kuwa na adabu kijana. Tumia lugha ya staha. Nikuoneshe kwasababu gani? Kufunga ni suala binafsi. Kupita mitaani na kusema umefunga, mara utoke saa tisa ili ukapike ni ushamba mkubwa hasa ikizingatiwa kwamba alfajiri ulikula na ulikula usiku wake mara mbili zaidi.
 
Hmmm, hao ni zaidi ya MUNGU wao YESU ambaye alionyesha udhaifu kiasi cha kutiwa majaribuni na SHETANI mara tatu alipokuwa amefunga kwa muda wa siku 40, hao ndo wafungaji sasa, hao ndo wana haki-miliki ya hayo maneno, wengine ni marufuku kuyatumia hayo maneno
Yesu kaonesha udhaifu wapi? Kashinda majaribu sasa udhaifu utoke wapi?
 
Kuwa na adabu kijana. Tumia lugha ya staha. Nikuoneshe kwasababu gani? Kufunga ni suala binafsi. Kupita mitaani na kusema umefunga, mara utoke saa tisa ili ukapike ni ushamba mkubwa hasa ikizingatiwa kwamba alfajiri ulikula na ulikula usiku wake mara mbili zaidi.
Shaitwan wahed!!!! hii tabia ya kudharau watu usiowajua imewagharimu wengi lakini hamjifunzi.
Wewe unaposimulia kushinda na njaa siku 7 ulitaka tukusifie? Ungekaa kimya sio kutafuta sifa mitandaoni.
Mambo ya waislam waachie waislam wenyewe
 
Kwamba siku zingine hamjiepushi na uovu? Sasa swala tano zinakuwa za kazi gani kila siku.

Mnaita kufunga kimsingi kwasababu hamli mchana na ndio mimi nimetoa changamoto kwamba huko sio kufunga.

Halafu jinsi unavyojibu hapa inaonesha namna gani hauelewi maana ya kufunga.
Padri akikosea haimaanishi ukristo haufai bali ni padri kimario ndio hafai, sasa unauliza sala tano za nini unataka kusema hakuna muislam anaenufaika na sala 5?
 
Kuwa na adabu kijana. Tumia lugha ya staha. Nikuoneshe kwasababu gani? Kufunga ni suala binafsi. Kupita mitaani na kusema umefunga, mara utoke saa tisa ili ukapike ni ushamba mkubwa hasa ikizingatiwa kwamba alfajiri ulikula na ulikula usiku wake mara mbili zaidi.

Nakuelewa sababu inatakiwa mtu akifunga iwe ni siri ya yeye na Mungu na siyo kutangazia watu.

Tena inatakiwa hata mdomo usiachwe ukauke ili ujulikane umefunga.

Mdomo unatakiwa kupakwa mafuta.
 
Yesu kaonesha udhaifu wapi? Kashinda majaribu sasa udhaifu utoke wapi?
Udhaifu utoke wapi? alipofunga kwa siku 40 akiwa nyikani pasina kula chochote hakuhisi njaa? Alihisi njaa, huo ni udhaifu, na ndo maana alipohisi njaa tu Shetani alimjia na kumjaribu kwa kumwambia "kama wewe ni Mwana wa Mungu, amuru mawe haya yawe mikate"
 
Wewe ukihisi njaa unakuwa na udhaifu?
 
Wewe ukihisi njaa unakuwa na udhaifu?
Unapohisi njaa ni udhaifu wa kimwili, ni kiashiria cha mwili kudhoofu na kuhitajia nishati tegemezi itokanayo na mlo

Waswahili walijisemea "njaa mwana malegeza, shibe mwana malevya"
 
Kitendo cha kuhisi njaa ni udhaifu wa kimwili, ni kiashiria cha mwili kudhoofu na kuhitajia mlo, kwenye somo la bailojia kuna kipengele kinaitwa 'metabolism' naamini unakifahamu

Waswahili walijisemea "njaa mwana malegeza, shibe mwana malevya"
Yesu alikuwa na mwili hivyo ni sawa akisikia njaa. Tafsiri ya udhaifu itakuwa sawa katika mwili hivyo nimekuelewa.
 
Salamu kwenu

Huwa siwaelewi watu wanaposema wanafunga wakati kila siku jioni wanakula.

Ninawafahamu watu wengi tu wanaofunga mpaka siku 21 kwa kunywa maji tu na kila siku wanaendelea na shughuli zao.

Mimi mara nyingi tu naenda mpaka siku saba bila kula na kazi nafanya kila siku.

Nadhani wanapaswa kutumia jina jingine lakini sio kufunga.
Sio siku ni masaa, sababu unapiga ugali ama wali ama magimbi ama viazi miogo saa kumi alfajiri mchana kutwa umeshiba.
 
HABARI wakuu, Ninajua hii IG yangu sio ngeni hapa katika kuchangia mada mbalimbali na kwa wale wadau wa jukwaa la fulsa ajira na ujasiliamali, nadhani wapo wenye kumbukumbu ya uzi niliowahi kuuanzisha namna nilivyopambana kutoka ziro to the point of hiro, na kuna jumbe nyingi nimeweza kupokea huko Pm na kuna vijana hadi sasa baadhi nimejitahidi kuwasaidia namna gani mimi niliweza kupambana hadi nilipo na kuna wengine tulishawahi kukutana nao Live na ningetamani kama yupo atakaepitia huu uzi ningeomba achangie, mimi ni mtu wa aina gani na kwanini huwa siku zote najitoa kwa ajili ya kuhakikisha vijana wenzangu ambao pengine tumetokea familia duni kupambana na kubadilisha historia za familia tulizokulia, Pia niwaombe Msamaha wale ambao hawajabahatika kujibiwa na Mimi PM zao na niwatie moyo kuwa kila mtu atajibiwa kwa mda wake maana kila siku ninafanya hivyo kuhakikisha kuwa vijana wanapata mwanga namna ya kujipambania na kufikia ndoto zao japo kwa uchache, Pia cha kutambua hapa ni kwamba ushauri wangu sio sheria pia haikuandikwa kila mtu atapitia njia nilizopita mimi ila nimefanya hivyo kuwasanua mwenye kujaribu ajaribu na mwenye kujitia moyo kuwa one Day yes, aamini hivyo kupitia ule uzi wangu wa "Kijana anaetafta mchongo apitie hapa"

Hakika nimepata vingi vya kujifunza kutokana na ule uzi na nimegundua Tanzania inao vijana wenye nia ya maendeleo, Changamoto hawana namna ya kupata watu sahihi wa kuwasaidia au njia sahihi ya kuwafikisha wanapotaka kufika,

Pia nimekutana na Negative comment nyingi kwa baadhi ya wadau ila kibinadam I take it easy maana ndivyo inavyotakiwa kuwa siku zote,
LEO nimeamua kushare na nyie wazo ambalo nimekuwa nalo kichwani ni Takribani Miaka 4,3 hivi na ni kuhusiana na vijana na Sanaa, Kama wengi tunavyojua vijana wengi wanavipaji, wapo Wabunifu, Waimbaji, Wachezaji (Dancers) Wachoraji, Waruka sarakasi, Watangazaji,Mafund ujenzi n.k..
Changamoto Kubwa kwa Vijana hawa 100% yao hawajui ni namna gani wanaweza kugeuza talanta zao na kuwa pesa, na wengi wao huishia kumaliza pesa zao katika kupambania talanta zao ambapo kimsingi hawajui namna ya kugeuza Talanta hizo kuwa pesa, hii imewaumiza wengi sana.

Mara nyingi kama nilivyowahi kusema Awali kuwa maandiko yangu huwa ni marefu sana maana huwa siamini katika njia fupi kwenye kupata maendeleo ila naamini maendeleo huja kwa utulivu wa akili, fikra yakinifu na maamuzi sahihi,

Hapa kama wewe ni Kijana mwenye Talanta na mwenye kutaka kuishi maisha yako kupitia kipaji chako hakikisha unajulikana sana, yaani kabla hujafikiria kutoa pesa yako kwenda studio kurekodi wimbo na kulipa galama za kutafta Mahojiano (Interview) Huko kwenye vituo vya Radio mikoani Jiulize hili swali Je? Huko ninakoenda kusikilizwa nitasikilizwa na watu wangapi wasionijua?
Kibaya zaidi kijana anatoa hela ili ahojiwe Redio Flani ambayo kimsingi inasikika mkoa mmoja tu tena kwa baadhi ya wilaya, na wasikilizaji wake wanakuwa watu wake hao hao ambao pengine amewapanga yeye mwenyewe kuwa kwa mda flani nitakuwa katika kituo flani nahojiwa tegeni sikio,! That is Poor in steve nyereres Voice!

Hapa cha kujifunza ni kwamba kwa miaka hii na vizazi hivi Medias hazina power tena ushahidi tunaosisi wasomaji wa Uzi huu kuwa mara ya mwisho kusikiliza Radio ilikuwa lini? Au kusikiliza mahojiano ilikuwa lini? Au siku umeskiliza tangazo kwenye Radio ukalizingatia ilikuwa lini? Majibu ni kwamba kwa kweli kwa vizazi hivi kwa sasa watu hawana mda tena na Media, Saizi kila kitu kinapatikana katika Social Networks na kwa vijana wanaojielewa na wanaotambua fulsa zilizopo huko kwa sasa ni mamilionaire na hawana mda na Radio wala Tv kupush kazi zao,

Mfano wa vijana ambao kwa sasa ni maarufu na wanatengeneza Pesa kupitia social Networks
Dulvan Comedian
Jaymond comedian
Oka martn na Carpoza...
Killy Paul tiktok

Hawa ni comedian ambao kimsingi kazi zao zote wanatumia mitandao yao binafsi kujitangaza, na hapa nimezungumzia hawa wachekeshaji tu ambao mwanzo tuliamini fani zao ndio pekee zinaendana na Mitandao ya kijamii lakini kwa sasa tumeona kuna vijana hata katika fani ya uimbaji wanatumia mitandao ya kijamii kufaidika na vipaji vyao wakiwemo Vijana kutoka Kigoma wanaojiita AFROCOVERS, wao kazi zao wanaziendesha mitandaoni na wanapiga pesa video zao zinaingia hadi trending na wamepata umaarufu mkubwa,

Pia tumkumbuke kijana LODY MUSIC ambae kwa sasa anaonekana msanii chipukizi anaekuja kwa kasi umaarufu wake umetokea mitandaoni, Mimi kwa mara ya kwanza nimeona Clip ya wimbo wake ikitembea mitandaoni hata kabla hatujajua jina lake na hapo ndio umaarufu wake ukaanzia hadi sasa ni msanii mkubwa,,,

Lengo la Uzi huu ni kutaka kuwakumbusha vijana umhimu wa kuitumia mitandao ya kijamii kutangaza kazi zao kuliko kutumia galama kubwa kurekod na kutumia pesa nyingi na kukimbilia platform ambazo hazina manufaa wala haziwatangazi
Ushauri kama unakipaji na unajiamini fanya yafuatayo tafta simu inaweza kurekodi video
Chukua video fupi rekodi clip ukiimba kapera (singing without instrument) kisha tafta namna ya kupenyeza kazi yako ionekane na Ig yako ijulikane hapo umeshaula saiz makampuni mengi yanatufta watu wakuwekeza kwao, ukishapata umaarufu mtandaoni ww tayari ushakuwa brand,

Mimi kama Terminator nimekaa chini nikafikiria ni vijana wangapi wanao uwezo wa kufanya kazi zao na kuzipenyeza mtandaoni hadi wakapata kuonekana?

Je? platform mbalimbali zinazotumika kwa lengo la kunyanyua vipaji zinawafikia vijana wote nchi nzima?

Je? sanaa vipaji ni waimbaji tu?

Je? ni sehem gani kutatokea platform ambayo itawatambua wachoraji,
Wapambaji, mafundi ujenzi wenye ubunifu, Dancers, washereheshanji na vijana wenye vipaji wanaoishi vijijin?

MAJIBU NI HAKUNA...

Tumeamua kuja na Project inayoitwa @Support_kipaji.tz
Hii ni project ambayo tumeaiandaa kwa lengo maalumu ya kukuza, kussuport, na kuinua vipaji mbalimbali pia kusogeza vipaji ambavyo pengine havionekani kuweza kuvisogeza karibu na wadau ili waweze kuviona,

Ni watu wengi wanakutana na kazi nyingi nzuri lakini wanashindwa kuwapata watu wenye uwezo na kazi husika kutokana na mazingira, pengine kutokuwepo na njia rahisi ya kuwatambua na kuwajua, hii inadumaza fulsa kwa vijana wabunifu ambao hawana namna ya kutangaza ubunifu wao,

Hivyo kwa moyo wa dhati kabisa ningependa kuwakaribisha Ndugu Jamaa na marafiki wenye lengo la kutaka kuwasaidia vijana pia kwa wale wenye nia ya kutaka kutangaza vipaji vyao Twende kule INSTAGRAM, Tukafollow Support_kipaji.tz kisha tukasupotiane huko.

HUDUMA ZITATOLEWA BURE BILA MALIPO LENGO LETU NI KUHAKIKISHA VIJANA WANATANGAZA VIPAJI VYAO NA WANAKUTANA NA WATU SAHIHI.

Pia zawadi nyingi nyingi zitakuwa zikitolewa kwa kazi nzuri kila mwisho wa mwezi. Kuanzia Laki2 hadi hadi laki5, Lengo letu ni kuinua vipaji vya wadogo zetu

Namna tunavyofanya Unatutumia kazi yako na taarifa zako binafsi unavyopatikana kisha tunakutangazia na kukutag bure lengo ni kwamba ukutane na wadau.

Page yetu ni mpya kabisa hivyo tunatamani kuanza na wewe!
 
Kwamba siku zingine hamjiepushi na uovu? Sasa swala tano zinakuwa za kazi gani kila siku.

Mnaita kufunga kimsingi kwasababu hamli mchana na ndio mimi nimetoa changamoto kwamba huko sio kufunga.

Halafu jinsi unavyojibu hapa inaonesha namna gani hauelewi maana ya kufunga.
Ili uwe muislam kuna nguzo za uislam
1:shahada
2:swala
3:funga
4:zaka
5:hija
Kila nguzo moja hapo imepewa jina na inafanyikaje! Hiyo namba tatu imeitwa funga na imeelezwa inafanyikaje ndio hiyo kujizuia kula, kunywa, kumuingilia mke! Vyote hivyo vimezuiliwa kwa mchana! Hiyo ndio imani ya waislam na ndio muongozo wao na ndio inaitwa funga, sasa kwa imani ya dini yako, au kwa imani nyingine hiyo sio funga basi usilazimishe waislam nao wasiite funga sababu wewe hutaki au una tafsir yako ya funga, kaa kwa kutulia, tuliza mshono!
 
Kaa kwa kutulia, endelea vizuri na mabadiliko ya ratiba ya kula.
 
Back
Top Bottom