Mbeya, Mwanza, Moshi huko wakristo ni 80% lakini mwezi wa kwaresma kila mtu yuko huru hakuna makatazo ya watu kula katika hicho kipindi
Kwani mtu akila mbele yako inaharibu funga yako?
Kiukweli moja ya sababu ambayo inanifanya niwaone waislamu wengi ni weak sana ndio hii.
Napenda kutumia mfano wa watoto ambao umri wao hauruhusiwi kufunga, hao watoto wanapikiwa na nani katika hicho kipindi cha mfungo?
Unawezaje kuwapikia chakula watoto wako ambao hawajafikia umri wa kufunga ukiwa wewe umefunga na ukaweza kujizuia usitamani halafu ukashindwa kujiuzuia pindi umuonapo mtu mzima akila mtaani?
Au hiyo futari ambayo mnafuturu saa 12, mara nyingi huwa inaandaliwa mapema kabla ya muda wa kufuturu haujafika. Kwamba huwa inaandaliwa na watu ambao hawajafunga ili kusudi watu waliofunga wakipika wasipate tamaa?
Ni hao hao waliofunga ndio wanaopika lakini hapa unaweza kujiuliza wanawezaje kuzuia hiyo ashki ya kutamani kula?