Unasomea Udaktari miaka mingi, kisha unakuja kulipwa hivi

Udaktari ni wito, kama shida yako ni kupata hela nyingi kafanye biashara
Unakuta mtu ameingia jeshini kufata maokoto! Unajua kila kitu wito
Kuna mtu hata leo wakiacha kulipwa hela nyingi ataridhika mana kwake ni wito!
Ualimu ni wito pia yani karibu kazi zote duniani ni wito.
Ukitaka hela kuwa mfanyabiashara
 
Zitaje hizo shortcut
 
Sasa BOT kwa mfano waajiri Daktari kwa kazi gani?

Ninachofahamu kila taasisi ya umma iwe serikali kuu ama halmashauri lazima kuwe na wanasheria ama wahasibu piga ua hawakosekani.

Lakini sio kila taasisi ya umma wanaajiri madaktari maana mfano TPDC wataajiri mwanasheria kwa ajili ya ushauri ama kusimamia masuala yote ya kisheria , mhasibu kwa ajili ya mahesabu na kumbukumbu za taasisi ama IT kwa ajili ya mifumo ya kieletroniki.

Mtu akiumwa anaenda hospitali ya kawaida sasa huyo MD aajiriwe TPDC kwa kazi gani?

Nimefanya kazi taasisi nyingi na kwenye kampuni binafsi ninachojua kote huko kuna wanasheria wa taasisi/kampuni lakini sijawahi kuona daktari wa kampuni.
 
MD aajiriwe TRA kwa kazi gani? Mwanasheria anaajiriwa TRA kwasababu ya kufanya kazi za kisheria ama accountant kazi za kiuhasibu, IT kazi zinazohusiana na mifumo ya computer ya taasisi.
Mzee Umechanganya Reply 😅😅
Sijasema mahali popote Kuwa MD au MMed Au Fellow "Super Special" (Phd) Wa Afya waajiriwe Mahali kokote Kule TRA au Taasisi nyingine soma kwanza kabla ya Kuquotes..

Kingine Hiyo slip aliyopost ni Mtumishi aliyeajiriwa Wizara ya afya na Tamisemi..
Je umepata Wasaa wa Kuangalia Walioajiriwa kwenye TAASISI kama Muhimbili, Bugando, Ocean Road na Tasisi zingine ukalinganisha pesa zao...

Maana unachofanya nikulinganisha Taasisi na Serkali za mitaa na Serkali kuu..

Ningeona Bora kama mngelinganisha MD kutoka kwenye Taasisi kama Muhimbili au MOI na Hizo taasisi zenu au NIMR na taasisi zenu
 
Tulinganishe Mwanasheria aliyeajiriwa Kwemye Taasisi yoyote na Daktari aliyeajiriwa Kwenye Taasisi yoyote ile kama Muhimbili,MOI, ocean road na NIMR
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…