Unatakiwa Kuelewa Au Kufahamu Kuwa Pesa Ya Halali Hapa Duniani Haipo

Unatakiwa Kuelewa Au Kufahamu Kuwa Pesa Ya Halali Hapa Duniani Haipo

Habari wana jamiiforums!!, poleni na majukumu ya hapa na pale 🤝. Kwa yeyote anaeamini kuwa anapata au atapata pesa ya halali katika harakati zake hiyo sio kweli, zaidi zaidi utaendelea kuwa maskini wa kutupwa na mtu wa kutumwa tumwa kila iitwapo leo.

Hili ni wazo la kifalsafa na kidini ambalo watu tunatazama kwa namna tofauti.

Inabidi tuelewe kuwa hakuna pesa iliyo "safi 100%" kwa sababu kila shughuli ya kiuchumi inahusisha masuala ya pesa lazima kuwe na makosa ya:-
  • Wizi au udanganyifu
  • Unyonyaji
  • Mifumo yenye kasoro,
  • Au madhara fulani kwa wengine kwa njia ya moja kwa moja
Pesa Inayotokana na kazi, au huduma zinazokubalika kisheria na kimaadili.

Kwa mfano, mwalimu anayefundisha, mkulima anayelima, au mhudumu wa afya anayetoa huduma, hawezi kuwa na pesa inayoweza kukidhi Mahitaji yake kikamilifu bali ataambulia kuwa na chenchi ambayo anaikusanya kila mwezi.

Kwa hiyo kauli ya "hakuna pesa ya halali duniani kote" ni ukweli inabidi tuukubali kivyovyote vile ; -

Najua kuna maoni tufauti Watu wengine wanakubaliana kuwa, kuna tofauti kati ya pesa iliyopatikana kwa uhalifu na kuna pesa iliyopatikana kwa kazi ya halali..

Kuwa mkweli hela yako ni ya halali au ndo bado upo unapambana mdogo mdogo mpaka tone la mwisho. ?? 😊😊.
HUo ni Mtazamo wako,,,,
Pesa ya halali ipo,,,,,,,,
Utajiri wa Haki na halali upo.......
Matajiri wa haki na halali wapo... tena ni matajiri kwelikweli na hawana mbwembwe wala mayowe.....tena wenye hofu ya Mungu,,,
Lakini wewe huwezi kuwaona sababu umezongwa na vitu pamoja na watu wa ajabu ajabu,
 
Inategemeana na chimbo unalopigia pesa au urithi wa wazazi.

Ila mambo yakienda tofaut mwanaume huamua kuchukua maamuz magum yaan plan 'B' na C
Kwa africa, pesa za kurithi ni ngumu sana kuziendeleza, ( mda wote tunawaza kugawana mirathi tu alafu chimbuko la pesa wazazi huwa hawasemi zimetokea wapi)
 
Back
Top Bottom