Unatakiwa Kuelewa Au Kufahamu Kuwa Pesa Ya Halali Hapa Duniani Haipo

Unatakiwa Kuelewa Au Kufahamu Kuwa Pesa Ya Halali Hapa Duniani Haipo

Jambo gumu ambalo nimekubaliana nalo ni kua nchi zetu hizi kufikia Dunia ya kwanza labda Muumba aingilie kati.

Hamuwezi kua mnazalisha Nyambizi, ndege za kivita, mitambo mizito, satellites au robots mkawa mnasumbuana na jezi za vyama haiwezekani.

Inauma sana ila kweli

Wewe unajua Elimu ya Polisi
 
Kijana umetapali nani tena? Au umefanya ufusadi katika ofisi unayofanyia kazi? "Acha kujifariji kwa mambo ya hovyo na ushetani..."

Mosi: hakuna pesa chafu duniani.. pesa zote ni safi, pesa haina uwezo wa kujichafua wala kujisafisha kwasababu haina uhai.. pesa ni kitu kilichowekewa thamani tu ili kufanya maisha ya duniani yaende vile inavyotatikana...

Pili: njia unazo tumia kupata pesa ndizo zinazotoa identity ya pesa yako.. kama njia zako si halali kama vile uwizi, ufisadi, umalaya, udangaji, kulawitiwa(ushoga) Utapeli na mambo machafu yanayo fanana na hayo. moja kwa moja pesa yako itahesabika kama pesa chafu (kwa sababu ya njia ulizotumia kuzipata na wala si pesa yenyewe). Mfano, mimi mzee wa zamani nauza duka, ikatokea fisadi papa mmoja au changudoa kaja kununua budhaa kwangu.. ile pesa niliyopatia mimi kwangu itahesabika safi kwa sababu nimeipata kwa njia halali.. kanipa pesa nimempa huduma halali... ingekuwa nauza vitu vitu visivyo halali moja kwa moja pesa inakuwa chafu... "what's matter is how a person get the money but not the money by itself

Mzee wenu na yeyuka! 🚶‍♂️🚶‍♂️🚶‍♂️
Hayo yote ni maelezo ya mtafutaji anayehangaika kujikomboa kimaisha.
 
Hubadilika kuwa pesa Halali ikiwa tayari ipo mkononi mwako, njia yoyote ya kuitafuta hata kama ni haramu maandishi yake kamwe hayabadiliki ikiwa tayari iko mkononi mwako.
Ahaa pesa mbele ya watu unatusukuma au tukusake kwa mapanga, nondo, marungu na bastola????
Shiiiiiit!
 
Habari wana jamiiforums!!, poleni na majukumu ya hapa na pale 🤝. Kwa yeyote anaeamini kuwa anapata au atapata pesa ya halali katika harakati zake hiyo sio kweli, zaidi zaidi utaendelea kuwa maskini wa kutupwa na mtu wa kutumwa tumwa kila iitwapo leo.

Hili ni wazo la kifalsafa na kidini ambalo watu tunatazama kwa namna tofauti.

Inabidi tuelewe kuwa hakuna pesa iliyo "safi 100%" kwa sababu kila shughuli ya kiuchumi inahusisha masuala ya pesa lazima kuwe na makosa ya:-
  • Wizi au udanganyifu
  • Unyonyaji
  • Mifumo yenye kasoro,
  • Au madhara fulani kwa wengine kwa njia ya moja kwa moja
Pesa Inayotokana na kazi, au huduma zinazokubalika kisheria na kimaadili.

Kwa mfano, mwalimu anayefundisha, mkulima anayelima, au mhudumu wa afya anayetoa huduma, hawezi kuwa na pesa inayoweza kukidhi Mahitaji yake kikamilifu bali ataambulia kuwa na chenchi ambayo anaikusanya kila mwezi.

Kwa hiyo kauli ya "hakuna pesa ya halali duniani kote" ni ukweli inabidi tuukubali kivyovyote vile ; -

Najua kuna maoni tufauti Watu wengine wanakubaliana kuwa, kuna tofauti kati ya pesa iliyopatikana kwa uhalifu na kuna pesa iliyopatikana kwa kazi ya halali..

Kuwa mkweli hela yako ni ya halali au ndo bado upo unapambana mdogo mdogo mpaka tone la mwisho. ?? 😊😊.
kitu halali huwa kina sifa gani
 
Back
Top Bottom