Unatakiwa Kuelewa Au Kufahamu Kuwa Pesa Ya Halali Hapa Duniani Haipo

Umejuaje kama ni matajiri wa halali,? ( hao unaosema ni wa halali yawezekana hujajua background yao ndo maana unasadiki kwa kuangalia vitu juu juu alafu unapata jibu la kusema pesa zao ni halali
 
Kwa hiyo kauli ya "hakuna pesa ya halali duniani kote" ni ukweli inabidi tuukubali kivyovyote vile ; -
Kuna mtu anafanya biashara sasa yeye anachofanya akisikia duka la upande wa pili linauza bidhaa labda 12,000 yeye anapandisha bei anauza 15,000 kitu kile kile ambacho mwenzie anakiuza 12,000 sasa hii inakua ina maana gani kifedha? Na akiulizwa anadai bei aliyochukualia mzigo ni tofauti na yule anaeuza 12,000
 
Mimi nilikuwa nauliza AI kuhusu uchumi wa dunia na pesa zinavyopatikana , naona anajibu utapeli mtupu wala hakuna uhalisia ..Kiufupi , hii dunia hakuna cha halali ni utapeli mtupu
AI ipo programmed Kwahiyo kuna baadhi ya mambo haiwezi kukuambia ukweli. Mwanzo ilikuwa inagoma kuchambua masuala ya betting ila kwa sasa naona wazee wa code wameruhusu..
 
Ndo unyonyaji wenyewe huo kibishara, kwa hiyo hapo ili apate pesa lazima afanye dhulma.
 
pesa ya halali ipo ila haiwezi kukupa utajiri, ila ipo

yaani nilime mahindi yangu au nipande miti, then nije niiuze miaka 10 baadae wachane mbao halafu uniambie hiyo pesa ni haramu... yaani sijaipata kihalali. au kuna mtu nimemuumiza hapo?
Hizo tunaita hela za mboga, bila kuwa mjanja yawezekana hata hiyo miti ukipanda ikashindwa kuota.
 
Kama kazi yako unayoifanya kwa sasa unaweza kuimuelezea mama yako mzazi na akakuelewa tena akakutakia baraka tele, sahau kuhusu utajiri

narudia tena, SAHAU KUHUSU UTAJIRI
 
Kama kazi yako unayoifanya kwa sasa unaweza kuimuelezea mama yako mzazi na akakuelewa tena akakutakia baraka tele, sahau kuhusu utajiri

narudia tena, SAHAU KUHUSU UTAJIRI
Upo sahihi kabisa mkuu. Hiyo inakuwa siyo kazi bali ni kibarua cha kila siku cha kupata hela ya kula na kesho uamke tena kuhangaika mtaani.
 
Kijana umetapali nani tena? Au umefanya ufusadi katika ofisi unayofanyia kazi? "Acha kujifariji kwa mambo ya hovyo na ushetani..."

Mosi: hakuna pesa chafu duniani.. pesa zote ni safi, pesa haina uwezo wa kujichafua wala kujisafisha kwasababu haina uhai.. pesa ni kitu kilichowekewa thamani tu ili kufanya maisha ya duniani yaende vile inavyotatikana...

Pili: njia unazo tumia kupata pesa ndizo zinazotoa identity ya pesa yako.. kama njia zako si halali kama vile uwizi, ufisadi, umalaya, udangaji, kulawitiwa(ushoga) Utapeli na mambo machafu yanayo fanana na hayo. moja kwa moja pesa yako itahesabika kama pesa chafu (kwa sababu ya njia ulizotumia kuzipata na wala si pesa yenyewe). Mfano, mimi mzee wa zamani nauza duka, ikatokea fisadi papa mmoja au changudoa kaja kununua budhaa kwangu.. ile pesa niliyopatia mimi kwangu itahesabika safi kwa sababu nimeipata kwa njia halali.. kanipa pesa nimempa huduma halali... ingekuwa nauza vitu vitu visivyo halali moja kwa moja pesa inakuwa chafu... "what's matter is how a person get the money but not the money by itself

Mzee wenu na yeyuka! πŸšΆβ€β™‚οΈπŸšΆβ€β™‚οΈπŸšΆβ€β™‚οΈ
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…