Unatumia mbinu gani kukwepa kula chakula ugenini pale unapokaribishwa?

Unatumia mbinu gani kukwepa kula chakula ugenini pale unapokaribishwa?

mcTobby

JF-Expert Member
Joined
Feb 16, 2018
Posts
7,894
Reaction score
22,679
Wadau , tupeane mbinu za kukwepa kula chakula ugenini pale unapokaribishwa Pasipo kuzusha sintofahamu kwa wenyeji wako hadi wajisikie vibaya..

Na sababu za kutokula ugenini kunaweza changiwa na mambo mengi ; mazingira ya uandaaji chakula, kupikiwa chakula usichoendana nacho kiimani mfano pork n.k au pia kuepuka kuwapa bajeti isiyokuwa na ulazima na mambo mengi...
FB_IMG_1740404752602.jpg
 
View attachment 3442412
"Na mji wowote mtakaouingia, wakiwakaribisha, vileni vyakula viwekwavyo mbele yenu."
(Luka 10:8)

1 Timotheo 4:4-5
“Kwakuwa kila kilichoumbwa na Mungu ni chema, wala hapana cha kukataliwa, kama kikilipokewa kwa shukrani; kwa kuwa kimefanyika kitakatifu kwa neno la Mungu na kwa maombi.”
 
Kwa Wasukuma ukikataa chakula unapokaribishwa unaonekana mchoyo

Haitakiwi kuvuga hata kama umeshiba
Wasukuma kuhusu chakula sio shida zao mavyakula yapo tele.

Na mtu aonekane ameshiba hatakiwi kumaliza chakula.

Shida kuna jamii unaenda kula yao shida, chakula kimepikwa kidogo na wanalazimisha mno ule licha kusema umeshiba.
 
Wengine wanakaribisha ile kimazoea tu ,kiuhalisia chakula ni kidogo na umefika muda ambao wameshapika tayari.

Ubaya wanalazimisha mpaka kero.
Hapo ndo kisanga, unaweza kuta umepiga share za watu wengine ukiondoka ni lawama.
 
Back
Top Bottom