Unatumia mbinu gani kukwepa kula chakula ugenini pale unapokaribishwa?

Unatumia mbinu gani kukwepa kula chakula ugenini pale unapokaribishwa?

Njia sahihi ya kukwepa kula ugenini ni kwenda kinyume na ratiba ya kawaida ya chakula.
Na muda sahihi kwenda kutembelea ugenini ni asubuhi na uondoke kabla mchana haujafika, ukikuta wanataka kula asubuhi ni rahisi kuwadanganya kwa kuwaambia kuwa umetumia dawa za Minyoo ambapo imeshauriwa ukae masaa sita ndiyo ule chakula ili dawa ifanye kazi kwa ufanifsi.
Ama utembelee kuanzia saa tisa alasiri ama kumi jioni mida hii familia nyingi zinakuwa zimeshakula chakula cha mchana na uondoke kabla ya saa kumi na mbili jioni ukisingizia unawahi usafiri ili ufike kabla ya giza
Hii ndo kanuni☝️
 
Katika kitu sikikubali katika jamii zetu za kitanzania ni hiki.

Mimi nikiwa nataka kula huwa sina kuzuga , na nikiwa sina mpango wa kula nayo sina kuzuga.


Jambo la mwenyeji kumlazimisha kumkaribisha mgeni, na mgeni nae kulazimishs kukataa alafu mwishoni ndo anakubali ni jambo la ajabu sana
 
Usitembelee kwa watu mida ya kula

Mila na tamaduni zote za makabila ya kibongo msosi ni jambo la HESHIMA kumpatia mgeni….. inakua ni kama fedhea kubwa kukataa kula ugenini
 
Wewe hujawahi kumtembelea jamaa yako lkn mke wake anajihusisha na mambo ya kichawi, mfno kitumbua kukipitisha kwenye K
Hahahha, hiyo sijawahi kuona wala kuwaza kama itatokea. But kwa jinsi ninavyopenda kula si rahisi kuacha msosi wowote.
 
Tunasema unatakiwa utie sunna ni jambo la kiungwana kama huamini mwenyeji wako kula nae sahani moja au mtu wa nyumba yake
 
Usitembelee kwa watu mida ya kula

Mila na tamaduni zote za makabila ya kibongo msosi ni jambo la HESHIMA kumpatia mgeni….. inakua ni kama fedhea kubwa kukataa kula ugenini
Sana yani timing mida ya kula ishapita ili usingizie ushakula
 
Niliwai kwenda ugenini kwa watu ambapo wao wanatumia kinywaji cha asili kinaitwa togwa nikakaribishwa sana kwakubembelezwa ad nikakubali mwishon nilishindwa kumaliza kabisa ilinishinda nilikunywa kwakuogopa watajiskia vibaya
 
Njia sahihi ya kukwepa kula ugenini ni kwenda kinyume na ratiba ya kawaida ya chakula.
Na muda sahihi kwenda kutembelea ugenini ni asubuhi na uondoke kabla mchana haujafika, ukikuta wanataka kula asubuhi ni rahisi kuwadanganya kwa kuwaambia kuwa umetumia dawa za Minyoo ambapo imeshauriwa ukae masaa sita ndiyo ule chakula ili dawa ifanye kazi kwa ufanifsi.
Ama utembelee kuanzia saa tisa alasiri ama kumi jioni mida hii familia nyingi zinakuwa zimeshakula chakula cha mchana na uondoke kabla ya saa kumi na mbili jioni ukisingizia unawahi usafiri ili ufike kabla ya giza
Mimi ndo nafanyaga hivi mkuu mule mule yan
 
Wasukuma kuhusu chakula sio shida zao mavyakula yapo tele.

Na mtu aonekane ameshiba hatakiwi kumaliza chakula.

Shida kuna jamii unaenda kula yao shida, chakula kimepikwa kidogo na wanalazimisha mno ule licha kusema umeshiba.
Kwa huo ujamaa wa kulishwa bure tena kwa kushinikizwa ule, ni lini utakuja kumshawishi mbongo aione CCM ni adui yake......

Ndio tatizo lilipo...Lissu ana kazi sana.
Mbongo hajawa tayari kukombolewa..
Na akishashiba anawaza Yanga na Simba siku imeisha....
 
Wadau , tupeane mbinu za kukwepa kula chakula ugenini pale unapokaribishwa Pasipo kuzusha sintofahamu kwa wenyeji wako hadi wajisikie vibaya..

Na sababu za kutokula ugenini kunaweza changiwa na mambo mengi ; mazingira ya uandaaji chakula, kupikiwa chakula usichoendana nacho kiimani mfano pork n.k au pia kuepuka kuwapa bajeti isiyokuwa na ulazima na mambo mengi...
View attachment 3442412
Nimefunga
 
Jana imetoka shamba nafika Kwa wenyeji nakuta ugali wa muhogo na omena na mayai wamechanganya dah nikapewa sahani kukataa nashindwa ikabidi Nile kidogo
 
Niliwai kwenda ugenini kwa watu ambapo wao wanatumia kinywaji cha asili kinaitwa togwa nikakaribishwa sana kwakubembelezwa ad nikakubali mwishon nilishindwa kumaliza kabisa ilinishinda nilikunywa kwakuogopa watajiskia vibaya
Hahah,

Mi niliwahi kuishi huko Mafinga ndani, wao bwana walikuwa ni ulanzi (bamboo juice) ndio kitu kinapatikana kwao na muda mwingi nikienda ndio nakaribishwa huo sikuwa navunga ni kupita nao tu mpaka nalewa na nikauzoea.
 
Back
Top Bottom