Unatumia mbinu gani kukwepa kula chakula ugenini pale unapokaribishwa?

Enzi ya Secondary unajua tena shule za bweni, basi wik end nikaenda kwa mshikaji wangu yeye alikuwa Day, hawa walikuwa Christian, Jamaa yangu ananijua mimi siyo Christian!, pale mezani kulikuwa na kipande cha nyama mimi nilikuwa nishakistukia ni Mdudu, basi mzee wake ananisogezea pata kijana, yule jamaa yangu akakizuia akamwambia Dingi huyu Muislam, Mzee alijisikia vibaya sana na kuniomba radhi...Tangu hapo mara chache sana nakula UgeniniπŸ˜€πŸ˜€.
 
Njia sahihi ya kukwepa kula ugenini ni kwenda kinyume na ratiba ya kawaida ya chakula.
Na muda sahihi kwenda kutembelea ugenini ni asubuhi na uondoke kabla mchana haujafika, ukikuta wanataka kula asubuhi ni rahisi kuwadanganya kwa kuwaambia kuwa umetumia dawa za Minyoo ambapo imeshauriwa ukae masaa sita ndiyo ule chakula ili dawa ifanye kazi kwa ufanifsi.
Ama utembelee kuanzia saa tisa alasiri ama kumi jioni mida hii familia nyingi zinakuwa zimeshakula chakula cha mchana na uondoke kabla ya saa kumi na mbili jioni ukisingizia unawahi usafiri ili ufike kabla ya giza
 
Ntazingatia hili.πŸ“πŸ“πŸ“Œ
 
Niko kwenye mfungo,.
 
Kama si mahali pa kulala, jenga tabia ya kutembelea ugenini mida ambayo si ya milo..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…