Unatumia njia gani kuishi na dada wa kazi ( house girl) muda mrefu?

Unatumia njia gani kuishi na dada wa kazi ( house girl) muda mrefu?

Mi nilijipa umuhimu kama kaka, mpaka kwenye cherehan nikampeleka ebwana eeh. Huko ndo akapata walimu akasema hata mwaka hajamaliza. Ukitafuta mdada wa kazi usimtese ila pia usijipe umuhimu sana
Hii nayo ipo
Unamuwazia mema, kumbe yeye Yuko na mengine
 
Mjali yeye na wazazi wake; mnunulie kitu cha kumpa ujuzi, ambacho atajifunza kwa muda mrefu mfano cherehani.
Mwisho: Usikubali kama mwanaume kuajiri binti wa kazi mzuri kuliko mkeo.
 
Usimkaripie/kumfokea ovyo ovyo au kumsema sema mpe uhuru wa kujitawala ,mnunulie baadhi ya mahitaji yake,kama mnatoka na familia nae usimwache,kazi za nyumbani baadhi kama watoto wakubwa/kujitanvua baadhi ya kazi wasaidiane nae kwa zam,jitahidi ukipeleka watoto wako auti nae mbebe nenda nae yaani ishi nae kama moja ya familia yako hakikisha mnachokula na familia yako hata kama umeleta nje ya nyumbani kama zawadi nae mpe.ukifanya hivyo hata kaa akumbuke kwao.
Mi nimeishi na mfanyaazi miake 8 hadi kaolewa harusi kutokea kwangu
umesema yote, tumeisha naye sasa tunaelekea mwaka wa 11, ila tayari ameshapata mchumba. Ataondoka kwa sababu ya kwenda kuolewa
 
Back
Top Bottom