Laki tatu Hana uwezo wa kutoboa Kwa familia ya mke na watoto wawili tuache kumpa matarajio hewa ...
Mke na watoto wawili wanahitaji Milo miratu Kwa siku ,....hapa tuseme amenunua ...
Kilo Kumi za Michele -25,000
Unga Kila 10 ,- 20,000
Mafuta ya Kula Lita 5- 25,000
Sukali kilo 5-16,000
Maharage kilo 5-10,000
Hapo tuseme Laki imeisha Kwa vitu vya mhimu sanaaaaa.....hivyo vyakula nimeassume vitamaliza mwezi japo Sina uhakika .....
Hapo Laki imeisha imebaki Laki mbili (200,000)
Twende matumizi mengine ..
-Kubadili mboga mboga ,dagaa ,nyama kidogo ,mchicha ,sio Kila siku mtakula mahalage ...---20,000
-gesi au mkaa --25,000
-chumvi ,majani ya chai --4000
-sabuni ,kipande na Unga &steel wire kusugulia sufuria -5000
Maji ya kununua Kwa mwezi /bill -5000
Umeme kulipa Kwa mwezi -5000
Nauli ya kwenda kazin na Kurudi baba pekee yake -30,000
Nauli za mke na watoto kutoka sehemu kwenda sehemu Kwa emergency, mkee hawezi kaa nyumbani kama jiwe ,kwenda sokon n.k-20,0000
Hapo umetumia Laki na uchafu (130,000) ...
Baada ya yote hayo imebaki 70k..
Hujanunua vocha ya kuwasiliana na mkeo tuseme Kwa mwezi utatumua -5000
Mtoto amepata kikohozi ,au kichwa kinauma ,umenunua hata Panado .n.k -5000
Kanisani hujatoa sadaka wewe na mke ,Kwa mwezi wote wawili tuseme -10,000
Hela ya takataka ,ulinzi shirikishi mtaani maana mjumbe atakuja kudai [emoji23]-5000
Mwanaume hauwezi kaa nyumbani tu utaangalia hata mpira ,bia moja ,-20,000
Hapo hujanunua nguo ,mkeo hajaenda saloon ,wewe hujaenda saloon kunyoa ndevu ,watoto hawajaenda hata kutembea kokote hata beach ,watoto hujawanunulia hata biscuit,ndugu hujawapa hata 100, mama mzazi hajakuomba hata 5000,,,, hujapata emergency ya kuumwa hata hospital,,hujahonga Kwa michepuko ,hujapoteza pesa (maana kuna hela zinapotea tu automatic bila kujua sababu [emoji23]...
Laki tatu hutoboi aiseee....
Na hapo ili utoboe mwezi lazima uishi kama shetani kwa matumizi ya hapo juu.....