Unatumiaje laki tatu kwa mwezi?

Labda kama yupo dar au Arusha. Mikoani anatoboa ila asahau kununua Nguo
 
😀😀😀😀😀
 
Kabla sijasema umeshanichamba hivi? Nikisema je?
Nimechekaaaaaa
Nakuambia ukweli nifah, ulikuwa uko vizuri sana, lakin baada ya kuwa na yule jamaa ukabadilika, jamaa mtu wa kujisikia sana, majivuno meengi wakati hela hana. ujanja janja tu amekutumia kupata umaarufu tu
 
Nimesoma maelezo ya wengi, lakini hiyo laki3 inategemea mazingira aliyomo, lakini hata kama Yuko wapi Bado hiyo laki 3 itamfanyia KAZI na maisha yataenda tu, watu wanashangaa tu kuwa pesa ndogo hiyo lakini Kuna watanzania hata laki moja hawapati Kwa mwezi, wanazo familia na maisha yanasonga tu
 
Mshahara kama huo unakuaje na familia aisee? Huo mshahara hata bachelor haumtoshi kabisa sembuse wewe mwenye Mke na watoto? Mnatoa wapi Nguvu ya Kuoa na Kipatao tia tia maji ivo, Ungekuwa mwenyewe ungepambana ila tayari una familia apo utaishi kama Shetani
 
Tatizo hujasema unaishi mkoa gani na umri wa watoto pia. Kuna mikoa hiyo hela ni kubwa mengine ni ndogo na mingine ni kiduchu.

Swala la matumizi muachie mkeo, wewe focus na kuitafuta hela tu, ishu za matumizi muachie mkeo.

Ila Mkuu ilikuwaje ukaanza familia kubwa kwa kipato kidogo au ni mambo yalienda arijojo wakati fulani?
 
Mbona ndogo sana elf 10?, walau 30 ya dharura
 
Wageni wasimtembelee
 
Kama unafanya kazi mbali kiasi cha kupanda daladala nunua baiskeli. Hela laki 2.5 inatosha sana kula na kulipa umeme na maji kwa familia ya watu4. Ila tu
Unga kilo 1 kila siku 30kg mwezi mchele 1kg kila week
Mboga elf60 mwezi, maji na umeme elf10. Sabuni ya kufua na kuoga 10k, mafuta pika 20k, chumvi 3000, sukari ya uji asubuhi 4kg mwezi,
 
Ukitaka kuishi bila stress ukipokea tu mpe mkeo hela yote hata matumizi yako akupangie yeye. Wanawake wanajua kubana na kutunza pesa
 
Hakikisha unakodi shamba ekari moja. Lima mahindi nusu eka na maharage nusu eka.
Hapo utakuwa kwanza umetatua changamoto ya misosi.
Wapigie simu ndugu zako kijijini wakutafutie shamba la kukodi.
Tuma hela ya kulimia, mbegu na mbolea.
Kwa mwaka utaweza kuokoa hadi Tsh milioni moja kwenye gharama za chakula.
 

Panga na mkeo acha kutusumbua sisi
Mbona hamuwaamini wake zenu?
Uje hapa utuombe wazo la biashara
Mambo ya matumizi ni wewe na mke wako
 
Achana na smartphone kwanza[emoji1]

Maaaba hivi vidude vinafilisi sana Hela zetu.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…