Unatumiaje laki tatu kwa mwezi?

Unaishi mkoa Gani ? Huo mshahara naona unasababisha niache kazi soon, mana kula tu hautoshi Zanzibar,
 

Hakuna namna ya ku balance hiyo hela, pambana tu, weka hasira kwenye kutafuta hela au kazi bora zaidi.

Kama inatosha kula, achana na akiba kwa sasa, maana kuweka akiba itakuwa kutesa familia.

How comes una watoto wawili katika ugumu wa maisha wa kukaa nyumba ya 30,000? Maisha magumu sana.

Usije ukalogwa ukaongeza mtoto, maana mtoto mwingine bila mkakati ni kujipiga muuri wa umaskini.
 
Da iyo laki tatu ni ndogo sana, unafanya kazi Ili uishi,
 
Biashara itakufa
 
Mtu anae kwambia mshahara haujawahi kutosha ujue ana kuosha ubongo tu , mtu anapokea 1.5 million ni tofauti na 300k, na huyu wa 1.5million anaweza na kuku ajiri na akaendelea kuishi fresh, mtu anakwambia mshahara haujawahi kutosha na anatembelea matako we unaendelea kutoboa viatu.
300k ukitoboa, ujue Kuna kauwizi ndani yake katika shughuli unayofanya.
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
300k kwa maisha ya sasa ni ngumu kwa mtu anayeanza maisha na kupanga chumba, bili ya umeme& maji, mahitaji ya chakula, usafiri na ziada ya dharura haitoshi..
 
Hakuna mshahara unaotosha jiongeze mdau kwa kuhakikisha unakula kulingana na urefu wa kamba yako
 

Sawa Engineer nakuelewa unachosema. Tatizo ni kwamba mahitaji na matumizi ya wengi yanabadilika kulingana na kipato

Mtu anaelipwa 1M hatataka apange chumba kimoja Cha 30k. Hapo ndio msemo wa mshahara hautoshi unapoanzia.

Binafsi tatizo sio unalipwa kiasi gani, zaidi ni unafanyia nini kile unacholipwa? Hapo ndio tofauti inapokuja.

Nakumbuka nilikua nalipwa 100k, nikapata kazi ya 340k, awali niliona pesa nyingi sana...hiyo furaha ilidumu miezi miwili tu ya awali. Hapo tunaongelea 2005.
 
300k kwa maisha ya sasa ni ngumu kwa mtu anayeanza maisha na kupanga chumba, bili ya umeme& maji, mahitaji ya chakula, usafiri na ziada ya dharura haitoshi..
Mzee baba tatizo ni familia hapo..
Ila angekua alone inatosha hiyo
 
Mzee baba tatizo ni familia hapo..
Ila angekua alone inatosha hiyo
Ni kweli familia inaweza ongeza au kupunguza matumizi ya fedha , ila laki tatu kwa mshahara huwezi fanya saving .. labda walau ujinyime na kuishi maisha ya papatu papatu miaka miwili ili ununue bodaboda utakayempa mtu akuletee 7k kwa siku .... tofauti na hapo huna ujanja
 
Yaani hapo kujinyima na watoto.. plas mke daaah
Hiyo itakua ishu nyingine.
Hapo a
Alternative way ni nini mkuu.?
 
Yaani hapo kujinyima na watoto.. plas mke daaah
Hiyo itakua ishu nyingine.
Hapo a
Alternative way ni nini mkuu.?
Mtoto na mke wanapaswa kupata mahitaji yote ya muhimu kwa sababu wewe ndiye uliyechagua aina ya maaisha unayotaka. Kuhusu kujinyima ni pamoja na kukubali kudharaulika ili siku moja uwe na kwako .


Tunashindwa kwa sababu, ila tunapaswa kuzishinda sababu .. Wengi wetu tunakimbilia majukumu bila ushauri kutoka kwa walio mbele yetu na yakishushinda ni kuanza kuzunguka zunguka huku mitaani.. Jenga familia ukiwa umejipanga la sivya jiandae
 
Daaah hapo ni changamoto aiseeee
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…