Unatumiaje laki tatu kwa mwezi?

Ushauri wa maana sana.
 
Dah acha tu mm wakat nafanya kazi mshahara wangu ulikuwa lak 6 take home ila still nilioma hautoshi kwasababu ya kufanya investment za mbeleni..
 


Ulichokiandika kinakaribiana sana na uhalisia

300K kwa mwezi bila kujiongeza haitoshi
 
Hizo hela anatoa wapi sasa mtu analipwa laki3 na ana familia, ata-save vipi pesa ya kukodi shamba na ghalama za kulimia
 
Ukibajeti vizuri laki 3 inaweza kutosha kwa matumizi ya kujibana ya kawaida mwezi mzima kwa familia ya watu 4. Fanya hivi.

Chakula120,000/= mchele kg 15-20, mahindi debe 1, ngano kg 5, mafuta 5ltr, tambi elfu 15.

Energy ya kupikia 35,000 (gas & mkaa).

30,000 kodi, elfu 20 bili za maji na umeme.
Mkeo unamuachia elfu 50 matumizi mengineyo. Unabaki na elfu 40 unatamba nayo mwezi mzima, Hapo utajua hujui kiukweli maisha yamepanda laki tatu haitoshi.
 
Maisha ni tofauti aana mm napokea 2.5 m hazinitoshi sipati ya kuweka akiba
 
Kweli mshahara haujawahi kutosha na hata ukiongezeka na mahitaji hayo yanaongezeka.
Ila pia wakati mwingine mazingira yanaweza kuamua upate saving kwenye kimshahara chako au usiweze kusave.
Mfano kwa mshahara wa rafiki yetu kwa mazingira ya mjini mfano Dar huo mshahara ni ngumu kidogo kufanya saving hasa ukizingatia ana familia inayotegemea ihumiwe kwa mshahara huo ila ukiwa mazingira ya vijijini kwa mshahara huo unafanya saving.
 
We ni mwalimu uko halmashauri gani
 
Kwanza;- 300k ni nyingi sana ukiamua kukabiliana na maisha na sio anasa za dunia

Pili;- Mtangulize Mungu katika kazi zako
•Mshirikishe mwanamke wako katika kila unalo lipanga wanawake wetu ni mibaraka katika kila hatua tunayo piga

Tatu;- Jua katika maisha ya ndoa na kazi ili mambo yaende inabidi uangalie source of income yako inaendaje usitegemee mshahara tu
•Kwa sisi tulio kulia maisha ya vijijini baba anafanya kazi kiwandani anapata 7k per day mama yupo nyumbani lakini hakuacha kumshirikisha

NOTE:- Wanawake wamebarikiwa akili ya utambuzi kwa haraka katika hali ya maisha nitakupa mfano Leo unaona single mother wengi walio na utambuzi wanatoboa kwasababu chukua ilo mshirikishe mke wako lakini msikilize pia mawazo yake

Nne;- Jua jinsi ya budgeting, hapa ninacho maanisha angalia vitu muhim kwanza nyumbani
•Utahitaji chakula ili kesho uwe na nguvu ukafanye kazi
•Watoto watahitaji kalamu na daftari waende shule
•Utahitaji maji na umeme au vyanzo muhim katika nyumba
•Mkeo mpe pesa yaa kutunza mji
•Anzisha biashara ambayo itakusaidia wew kujaza kibaba ndani kwa msaada wa mke wako

Tano;- Jua kutunza taarifa (Record keeping) hii itakusaidia wew kujua mwezi huu nipo katika hatua gani na utatambua je mwezi ulio pita nilitumia kiasi gani sehem flan na mwezi huu nimetumia kiasi flan, Kumbuka kila siku vitu vinapanda bei.

Muhim zaidi jifunze pia mfundishe mke wako kuangalia fursa mbali mbali na kuzitumia
Pia mkumbushe mke wako lengo la familia tukumbuke wanawake wapo vizuri lakini wengi wanajisahau pale unapo anza kuingiza 6k per day wakati juzi ulikuwa unaingiza 3k.
 
Jinga sana [emoji1] [emoji1787] [emoji23] [emoji38]
 
Wasomi wetu kwa kujiendekeza watu wanatumia laki kwa mwezi na ana familia na watoto wanaenda shule na maisha yanaenda safi kabisa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…