Elections 2015 Unaunga mkono Lowassa kuhamia CHADEMA na kuwa mgombea Urais?

Elections 2015 Unaunga mkono Lowassa kuhamia CHADEMA na kuwa mgombea Urais?

Unaunga mkono Lowassa kuhamia CHADEMA na Kugombea Urais?

  • NDIYO

    Votes: 318 59.8%
  • HAPANA

    Votes: 214 40.2%

  • Total voters
    532
  • Poll closed .
Naunga mkono Lowasa kwenda jela, siungi mkono Lowasa kuhamia UKAWA

mwache aje atuambie vizuri ile richmondi ilkua yake au ya jamaa yake - hadi uchaguzi ufike tutaona mengi. Siri zote zitafichuka:doh:
 
Nasema toka moyoni Kabisa tena kwa uchungu Chadema acheni hii mambo. Kama mnapima upepo nawaomba Kabisa. Mtatuambia nini sisi Watu Wa mMwanza tulioacha shughuli zetu na kuimba Rais Rais mji mzima. Halafu mlete mambo ya ajabu. Acheni kama mnasikia. Huu Uzi umeniharibia siku Kabisa.

Watu wa mwanza au wewe we unajua mawazo ya watu wote wa mwanza jisemee wewe wengine hujui wanapenda nn
 
Hawawezi kufanya hivyo, usiwe na wasi wasi mkuu.....Poll hii na propaganda nyingine zinazoendelea hapa hazihusiana na UKAWA !
 
Wewe Salary Slip CCM mambo ya chadema na kutaka maoni yanakuhusu nini. Ebu tuondolee upuuzi wako. kila siku chadema Chadema. If you can not fight then join them. Kama unaipenda acha kuteseka njoo ujiunge na chama lenye nguvu. Unakosa usingizi wa bure ya nini
Je,utaunga mkono uamuzi wowote wa kumfanya Lowassa awe mgombea uraisi kwa ticket ya CHADEMA/UKAWA endapo uamuzi huo utafikiwa?

Jibu Ndio/Hapana/Sijui

Kura hii inawahusu Pro-UKAWA wote na wengine wenye kuunga mkono umoja huu tu.
 
Je,utaunga mkono uamuzi wowote wa kumfanya Lowassa awe mgombea uraisi kwa ticket ya CHADEMA/UKAWA endapo uamuzi huo utafikiwa?

Jibu Ndio/Hapana/Sijui

Kura hii inawahusu Pro-UKAWA wote na wengine wenye kuunga mkono umoja huu tu.

Ndiyoo
 
Aliyekuwa kiongozi mkuu wa China (baada ya kifo cha Mao Tse Tung) na ambaye aliasisi mageuzi makubwa ya kiuchumi yaliyoifikisha hiyo nchi ilipo leo, Deng Xiaomping aliwahi kusema: "Haijalishi kama paka ni mweusi au ni mweupe ili mradi akamate panya". Hapa Deng alikuwa anamaanisha ili kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kuondoa umaskini, mbali na ujamaa, China pia itakumbatia soko huria (ubepari). Kwa kuzingatia huu mfano, hapa kwetu huwezi kuota maendeleo ya maana na endelevu; haki na usawa kwa wananchi wote bila kuiondoa CCM madarakani. Hivyo kama China walitumia ubepari kama kichocheo tu cha uchumi, Ukawa wanaweza kumtumia Lowassa kama 'catalyst' ya kuiodoa CCM madarakani. Hii hatua (approach) inaitwa PRAGMATISM. Muhimu ni kutokuyumba kwenye misingi ya kisera, kiimani, kiitikadi na kifalsafa.
 
Siungi mkono huyo jamaa kuhamia chadema. Mbona tuna hazina ya kutosha kugombea kiti cha urais!ana tuhuma nyingi sana huyo
 
Ndio..100/100

Kura yangu itakwenda kwa Ukawa...
 
Mtunga Swali umekosea, na huwezi kutumia Swali kama hili kupata maoni ya kiutafiti maana litakululetea majibu ambayo sio rahisi kutolea tafsiri.

Mfano aliye jibu hapana anaimanisha nini? Lowasa ahamie chadema na awe mwanachama wa kawaida, asihamie chadema kabisa, au ahamie lakini asiwe mgombea urais?
 
Back
Top Bottom