Aliyekuwa kiongozi mkuu wa China (baada ya kifo cha Mao Tse Tung) na ambaye aliasisi mageuzi makubwa ya kiuchumi yaliyoifikisha hiyo nchi ilipo leo, Deng Xiaomping aliwahi kusema: "Haijalishi kama paka ni mweusi au ni mweupe ili mradi akamate panya". Hapa Deng alikuwa anamaanisha ili kuleta mapinduzi ya kiuchumi na kuondoa umaskini, mbali na ujamaa, China pia itakumbatia soko huria (ubepari). Kwa kuzingatia huu mfano, hapa kwetu huwezi kuota maendeleo ya maana na endelevu; haki na usawa kwa wananchi wote bila kuiondoa CCM madarakani. Hivyo kama China walitumia ubepari kama kichocheo tu cha uchumi, Ukawa wanaweza kumtumia Lowassa kama 'catalyst' ya kuiodoa CCM madarakani. Hii hatua (approach) inaitwa PRAGMATISM. Muhimu ni kutokuyumba kwenye misingi ya kisera, kiimani, kiitikadi na kifalsafa.