Unawafahamu watu waliofanikiwa kwa kuwatoa kafara watu wao wa karibu?

Unawafahamu watu waliofanikiwa kwa kuwatoa kafara watu wao wa karibu?

Namfahamu jamaa mmoja alikuwa tajiri sana enzi sisi tunakuwa jamaa alikuwa anatumia baiskeli tu kama usafiri wake binafsi ila alikuwa na magari mengi tu.

Ajabu alikuwa na hilux ya mizigo ila bidhaa za duka lake alikuwa anafuata yeye mwenyewe kwa baiskeli yake ila kwa wengine anakodishia hizo gari za kubeba mizigo.

Sisi tulizoea kumuita TAJIRI MCHAFU wananzengo walikuwa wanasema kamtoa sadaka mdogo wake na huyo mdogo mtu alikuwa chizi fresh anakaa hapo dukani kwa kaka yake tu na hakuna wakumtoa hapo.

Haya mambo yanawezekana ila nafikiri ni mateso sana.
 
Mojawapo ya story huwa nazisikia sana na mtu kuwatoa watoto wake au ndugu zake kafara ili afanikiwe katika biashara au siasa. Utoaji kafara huwa unaelezewa kwa mtu huyo aliyoetolewa kafara kufariki kwa kinachodhaniwa kifo cha utata au kupatawa matatizo ya akili(kichaa).

Unaweza kuonyeshwa kichaa fulani ukaambiwa huu ni mtambo wa kutengeneza pesa wa tajiri fulani au ndio chanzo cha mafanikio cha mwanasiasa fulani.

Unajuaje au unathibitishaje kwamba fulani amefanikiwa kwa sababu ya kafara ya mtoto, mzazi, mke au ndugu yake?
Kuna nyuzi kadhaa za ndugu UMUGHAKA hata Tanzanian Dream kipindi hiki ana nyuzi yake ya Dark side of Business ukipitia na ukatulia vizuri utaelewa haya uliyoyazumgumza
 
Zipo kwenye mahandaki
Ogopa😁
20241105_223339.jpg
 
Mtazamo wangu kwenye hili upo kwenye maeneo mawili,imani na ujinga.Wengi wa wanaokuhadithia haya watakwambia nao wamesikia kuwa fulani kafanya hivyo.Hizi ni dili za Waganga tu kupiga pesa za Wajinga.Cha kujiuliza ni kwani bila hayo yanayosemwa kufanyika vifo au magonjwa ya akili hayapo?Hofu yangu ni kuwa Mganga akishatoa maelekezo basi kuna Mtu anaweza kuathiriwa kiukweli kwa kupewa sumu, kuchomwa kisu n.k ili afe. Kikubwa ni jamii kuacha tamaa,kutamani utajiri kwa kudhulumu uhai wa mwingine ndio nini bana.
 
Back
Top Bottom