Unawafahamu watu waliofanikiwa kwa kuwatoa kafara watu wao wa karibu?

Labda alikuwa anapendelea baiskeli ili afanye mazoezi au kuficha mambo yake kwa watoza ushuru wasimsonge songe au anabeba mizigo ya bangi n.k
Sioni uhusiano wa moja kwa moja wa huyo tajiri aliyeamua kutumia baiskeli na uchawi.
 
Exactly japo hisia zinaweza kuwa sahihi au zisiwe sahihi
Tatizo linakuja kwamba kwanza unakuwa na hisia fulani kaenda kwa mganga(huna uhakika), unakuwa na hisia(huna uhakika)kwamba huyo mganga ni kweli amebadilisha mambo yake na unakuwa na hisia tu(huna uhakika) kwamba katika kuwekewa mambo yake sawa fulani ametolewa kafara kwa kuuwawa au kufanywa kichaa. Hapa unakuwa mlolongo wa hisia tu bila uthibitisho!
 
Uchawi , nguvu za giza, utajiri wa kafara upo!!!! Lakini uchawi wa aina yoyote ni Siri na gharama kuanzia pesa, muda,kujitoa na kila kosa utakalofanya Lina gharama zake..... Usijidanganye mchawi aje atoe Siri zake hapa au formular zake kwako wewe ambae ni key board fighter usiweza kumsaidia lolote na huna impact yoyote kwake....... Ukichagua kuamini uchawi upo amini na ukichagua kutokuamini amini hivyo pia.
 
Kumbe hadi kuna wanawake wenye utajir wa namna hii
 
Kama uchawi ni siri watu baki tu wa mtaani huwa wanafahumu vipi kwamba fulani ametajirika kwa sababu ya uchawi?
 
Kuna waziri mmoja wa afya familia yake ina story ya kutatanisha sana lako hata yule meneja wake diamond wa morogoro inasikitisha sana kuona utu umepotea.
Ukifuatilia story za kila familia duniani unaweza kusema ni za kutatanisha sana ila kiwango cha utajiri na umaarufu ndio unazifanya familia nyingine kuongelewa zaidi kuliko familia nyingine.
 
Kumbe hadi kuna wanawake wenye utajir wa namna hii
Huyo mama ni tajiri kabla ya kugundua pesa zake ni za madawa nilienda kukaa likizo kwake.
Hilo jumba la kifahari nilijihisi mtoto wa mfalme nikapewa chumba ghorofani kipo full kuanzia tv mpaka friji.

Kuna watu wanaishi kama wapo mbele vilee halafu kazi yake anayoifanya nikisema inachekesha

Niishie hapa labda yupo humu asije akaona akaunga dots usiku akanifata buree
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…