Unaweza jiuliza hali iliyoko ya nchi ya kuelekea kupoteza umoja imeletwa nani

Hii ni maajabu
 
Kwani hao watu wa pwani ni lazima wajiunge CHADEMA? Una kauendawazimu Fulani kwenye uchaguzi wa viongozi wa CHADEMA nionyeshe huyo profesa muislamu aliyegombeaa, na nionyeshe dalili za udini kwenye uchaguzi ule?

Na waliokuwa wanawapigia kura ni wajumbe ambazo hawakutoka kanisani bali kwenye mikoa na Kanda za CHADEMA, muislamu yupi aliyejitokeza akakataliwa? Hizo ni akili zako za kiuendawazimu.

Ilikuwa ni Lissu na Mbowe wala siyo dini, Bob Makani alikuwa muislamu na ni muasisi na hakuna aliyezungumzia dini yake. You are so low
 
Waislam baadhi yenu mnapenda sana battle za udini sijui kwanini aisee.

Mnapenda sana kuetetea walio wenu kwa mlengo huo bila hata kujudge angle nyingine na mbaya zaidi mitaani waislam wenzenu hata hawana mawazo ya kidini kama mnayojipandikiza ninyi.

Nimecheka hapo uliposema wakristo hawakumchagua Lipumba kisa muislam wakamchagua Mkapa, na vipi battle ya Kikwete na aliewahi kua padri Slaa??, hapo waislam wakawa wengi wakamchagua Kikwete sio??

Ishu ni ccm mzee sio huo udini unaojaribu kuuleta. Hizi hoja zikifanyiwa masikhara zitachota wengi sana, ndio maana mnapigwa spana wenye mlengo wa namna hii.

Unasema sheria ya ugaidi imetungwa dhidi ya waislam, na mbona inasulubu hata wakristo kina Mbowe?? Au alibadili dini?
 
CHADEMA ina ushawishi na inakubalika zaidi Dar es salaam angalia kesi ya Lissu kisutu, na sijui vigezo gani unavyotumia na uliwahi kuongoza halmashauri ndani ya jiji hili
 
Hata Nyerere aliwahi kusema mtu aliyefilisika mawazo ataanza kufikiria kwa mtazamo wa dini, asili, kabila nk. Machizi kama hawa kwenye jamii ni WA kupiga spana, jiwe alipingwa spana humu si kwa dini yake wala kabila lake bali matendo yake
Nazungumzia nadharia ya partonagism. Ukanda wa pwani kuwa wengi wa dini moja is just a result. Lkn kumbuka ktk siasa kila kundi la jamii linapigania maslahi yake wenyewe. Hivyo ni jukumu la chama cha siasa kuweka maslahi ya makundi makubwa ya kijamii. Kama huwezi basi walau uwawekee puppets tu wataridhika.

Chadema bwana. Utawajua kwa mavazi yao. Lkn kufikiri kwao ni kama maccm walioathiriwa na unyerere.

Waulize waislam wanamuonage mzee wetu Nyerere. Waulize kitendo chake cha kuzuia kujengwa chuo kikuu cha waislam pale temeke wanamuona alionyesha urafiki kwa jamii ya waislam?

Waulize kwanini waislam aliwavunjia mtandao wa uongozi wa waislam africa mashariki EAMWS uliyotaka kujenga chuo kikuu hicho na kuacha mtandao wa uongozi wa jumuiya wa wakatoliki duniani uendelee. Unawachukuliaje watu wa mwambao, wanamuonaje, na ninyi mnawaonaje watu hawa ambao ktk uchaguzi huu wamebaki watulivu.

Mimi nawasaidia tu kuona upande wa pili wa shilingi
 
Mateso aliyoyapata Mbowe miezi 9, walislam zaidi ya 1000 wameyapata miaka 60 iliyopita.

Anyway mimi najaribu tu kuwaonyesha upande wa pili wa shilingi. Kwa nia njema tu. Ukikataa ushauri huu. Endeleeni kuwa na matumaini wakati hamko na ushawishi dsm. Mjii huu waachieni wenyewe kwa njia kuwafata na kuomba ushirikiano na wao. Kwa kuwapa position nafasi ya juu.

Hebu muwekeni Sh Ponda pale juu ili watu hawa wajihisi nao ni sehemu ya mfumo wenu.

Huu ni ushauri wa bure ndugu zanguni
 
Hatuwezi kusaidiwa na wapumbavu, nijibu kwanza ilikuwaje CHADEMA kuongoza halmashauri ya kinondoni au waislamu walihama? Dar es salaam siyo ya waislamu ni ya watanzania, upumbavu wote unaousema hapa ni kuwachukua hao waislamu wenzio mkajiunge na chama mnachoona kina maslahi ya waislamu.

Ni upumbavu narudi UPUMBAVU kuzungumzia siasa za udini kwa Tanzania ya leo. Wewe ni juha hata kuendelea kuzungumza na wewe ni kuhakikisha upumbavu wako unaishia kwako
K
 
Sheikh Ponda mpeleke ACT, na Dar es salaam CHADEMA Wana ushawishi labda misikitini.
 
CHADEMA ina ushawishi na inakubalika zaidi Dar es salaam angalia kesi ya Lissu kisutu, na sijui vigezo gani unavyotumia na uliwahi kuongoza halmashauri ndani ya jiji hili
tatizo ulikuwa hujafika Enzi zile za NGANGARI. Enzi zile za kesi za uamsho. Kisutu kulikuwa na idadi ya wanakijiji.

Sasa utafananishaje waliojitokeza kesi la lisu, au mbowe.

Nini ni minority hapa jijini. Naombeni jamii ya watu majority. Ndio movement pekee ya ushindi
 
Nilipiga Kura mara ya kwanza 1985, kitu ambacho hujanijibu wewe mdini ilikuwaje CHADEMA wakipata wabunge wengi Dar es salaam? Ilikuwaje waliongoza hadi halmashauri kama hawakubaliki Dar es salaam?.

Udini wako peleka kwa Mtoro, kwanini ni CHADEMA? Kama ni chama cha wakristo hamuoni mbadala? Punguza bangi
 
Sheikh Ponda mpeleke ACT, na Dar es salaam CHADEMA Wana ushawishi labda misikitini.
Sawa. Lkn kumbuka Tamko la Sheikh mwaka 2020, likipelekea JPM kuacha kampeni na kuanza kutafuta harakati za ushindi wa mezani. Kwa kauli ya Sheikh kusema nanukuu; 'Waislam wa Nchii kwa kauli moja tumeamua kura zote za waislam tutamchagia Mh Lissu.

siku chache badae tukasikita JPM kasitisha kampeni na karudi dodoma. Na matokeo yake si tu kulikuwa na wizi wa kura, bali ujambazi.

Unakumbuka nguvu ya kauli ile. Fikiria sasa awe ni sehemu ya waandamizi. Samia atajitafuta.

Kinyume chake tukiamua kumshaeoshi Sh Ponda aseme mwaka huu waislam wote tumeamua kumpa kura zetu Samia. Nawaomba Msije kulia lia
 
Umoja wa waTanzania uliimarishwa sana na Nyerere na Karume hadi kipindi cha awamu ya Kikwete kwa kuweka mifumo sahihi kwa wakati huo, na ilibadilishwa kila wakati kwa kuzingatia mabadiliko ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Kwa sasa kinachotutesa ni kuchelewa kuboresha katiba yetu na kutokuwepo na dhamira au utashi wa kisiasa wa dhati wa viongozi kujenga na kuimarisha umoja kwa kuweka mifumo sahihi inayoendana na changamoto zilizopo. Tuangazie katiba haraka.la sivyo itatugharimu sana miaka ijayo.
 

..tatizo na adui ni CCM.

..wakati CUF ni chama kikuu cha upinzani kiliitwa chama cha Waislamu magaidi.

..Chadema nayo ilipokuja juu kipindi cha Dr.Slaa wakaitwa chama cha Wakatoliki.

..Dr.Slaa alipoondoka, na kipindi ambapo Mwenyekiti wa CCM, na Rais alikuwa Mkatoliki, Chadema ikapigwa vita kuwa ni chama cha Wachaga.

..Sasa hivi jitihada za kuishambulia Chadema kidini zimepamba moto na pia wanashutumiwa kuhamasisha maasi.

..Ni kawaida ya CCM kutengeneza fitina za Kidini, au Kikabila, dhidi ya chama cha upinzani ambacho ni tishio ktk wakati husika.

..Jambo la msingi ni kuhakikisha tunakuwa na MIFUMO HURU ya uchaguzi ili kura ya mwananchi iwe ndio inayoamua mshindi ktk uchaguzi.
 
Huyo ni sheik wako, na hizo ni ndoto zako za utuopia unazoota kuwa kauli ya Ponda ilitoa impact against the wishes ya dikteta uchwara JPM, nini alichobadilisha?

Mwambie awaambie misukule wampigie kura dikteta wa kwanza mwanamke Afrika uone kama muislamu wake utambeba dhidi ya wenye akili timamu siyo majuha kama wewe
 

..Mufti wa Bakwata naye si alisimama upande wa CCM na Magufuli wakati wa kampeni?
 

..chama kinachopambania kuwepo kwa mifumo inayotoa HAKI SAWA kwa vyama vyote ndicho kinachostahili kuungwa mkono.

..tusikubali tena CCM itugawanye kidini au kikabila kwani madhara yake sote tunayajua.
 
Unajiweka position ya kutenda kosa kwa mwamvuli wa dini, ukidakwa unasema unaonewa, dini inakandamizwa na malalamiko ya namna hiyo.

Jimbo la Kawe lililokua la upinzani lina wapiga kura toka tarime??

Ndio maana huko juu unaambiwa shida sio dini ila ni ccm na mfumo wake kandamizi.

Uchaguzi ukiwa huru na haki, mzee hii dar upinzani na ccm watagawana majimbo.
Kile kimbunga cha 2015 hakuna mwanaccm anataka kijirudie.

Hiyo 2015 huko Zenji wapinzani Cuf & ACT waliwawadhia moto watawala.

Acha kujificha kwenye kichaka cha uzenji na uislam.
 

..CCM wanapokutesa sio kwasababu ni Muislamu au Mkristo ni kwasababu ni mpinzani wao.

..Tundu Lissu alinusurika kuuwawa wakati Mwenyekiti wa CCM na Raisi ni Mkristo mwenzake.

..Kuna wanachama wa Chadema zaidi ya 400 walitiwa magerezani na Magufuli na hakuchagua dini.

..Wazanzibari huuwawa katika kila uchaguzi na askari toka Tanganyika bila kujali Rais wa muungano na Amiri Jeshi Mkuu ni Mkristo au Muislamu.

..unaweza kumuweka Sheikh Ponda katika nafasi ya juu ili kuwavuta Waislamu.

..lakini kumbuka akitoka Mama Samia atakuja Emmanuel Nchimbi ambaye ni Mkristo.

..Wakati huo sasa CCM watageuka na kuanza kushambulia chama cha upinzani kuwa ni cha Waislamu.

..Kwa upande wa Zanzibar wao wataendelea kupelekewa moto kama ilivyo desturi kwani kule kampeni za Udini hazina nafasi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…