Utt bond account, masuala ya nyumbani yote kuendesha familia,Kula unachotaka kitawezekana hapa hatà ukipata ajari au maradhi ya kudumu utajihudumia wewe mwenyewe pasipo msaada kutoka kokote utaishi kama mtumishi wa umma.
Kumbi za sherehe, hapa utakuwa unapokea cash kabla ya watu kutumia ukumbi wako.hapa nakushauri wewe uwe unachukua Hela ya ukumbi tu Haina longolongo kabisa. music,chakula, na mengineyo waachie wengine. Sherehe ikiisha we chukua kofuri unafunga ukumbi wako, huku unasubiri gawio la mwezi la UTT.
Nunua Shamba na wekeza kufuga nyuki Kwa kisasa zaidi, tafuta maingineer wafanye design ya Shamba la nyuki, hapa utapata asali ya kutosha na kuuza Kwa Bei nzuri tu. Even if mambo yakienda vibaya UTT Bond Bado itakubeba.
Nunua Shamba na panda mbegu nzuri ya machungwa au machenza au mapapai,au karoti au ndizi tamu, hakikisha unalima kisasa sio unategemea mvua za misimu hapana, tafuta maingineer wafanye design kabisa, na pia miradi hii ikibumaa UTT Bond Bado itakulinda.
Zama mtaani kufanyà research uone watu wanataka nyumba zipi za kuishi, then Jenga nyumba za kupangisha, ukishazimaliza kabla ya kuzipangisha zitafutie hati then ingia bank kuchukua mkopo, halafu sasa zipangishe, unakuwa hutegemei Hela ya wapangaji maana najua ni ndogo sana. Yani wapangaji unawafanya kama walinzi tu wanyumba bila wao kujijua maana nyumba inatakiwa kuwa active Ili ipendeze. Hela ya mkopo unaweza ifanyia kazi nyingine ambayo itarudisha faida Kwa haraka.
Tafuta Shamba then Jenga mabwawa ya kisasa ya kufuga samaki,chukua samaki wenye soko tu hapa namanisha sato,migebuka wa kigoma na pia unaweza Fuga na dagaa chukua mbegu ya ziwa Victoria na ziwa tanganyiKa, tafuta eneo kingine Jenga frem za bucha ya samaki tu unaweza kuwa unapangisha hizo bucha then wapangaji wako unakuwa unawauzia Kwa Bei ya chini kidogo then wao ndo wanauza, hapa mambo ya TRA wao ndo watamaliza weed unakuwa mbali na TRA kabisa maana utakuwa kama mkulima wa samaki.
Kama wewe ni mtaalamu wa network Hela nyingine kiasi kidogo ungewekeza kwenye FOREX trading japo ni risk sana unaweza poteza.
"""""***"""""*****""""*****"""""""