Unaweza kuwa tajiri kirahisi, mtaji mdogo tu fanya biashara ya bucha la nyama ya ng'ombe

Unaweza kuwa tajiri kirahisi, mtaji mdogo tu fanya biashara ya bucha la nyama ya ng'ombe

Nimewahi kushu

Nimewahi kushuhudia ulaji wa nyama maeneo ya Shimbi yaani siku ya Jumapili na Alhamisi nyama hata uchinje ng'ombe 3 wanaisha siku hiyo hiyo, na nikabaini mtu kama yuko maeneo ya Rombo hii fursa ni nzuri sana.
Hata Mimi ni wa Rombo Tarakea ko kitu ni kile kile...... Yaaan ng'ombe wanalika sana

Au bucha za nguruwe daily unauza! Nashukuru kwa kuwa Shahid hapa najua wapingaji wapo!
 
Ni kweli Mkuu, mambo ya kwenye writings na ground huwa ni tofauti sana

Unaweza kukopa kisha kujaribu kuingia Kwenye hiyo biashara ukabaki na madeni tu huku Mtaji ukikata bila returns
Achaaa🙌
 
Wazo: BUCHA La NyamaCapital: 4MBidhaa: Nyama ya Ng'ombeKwanza, Biashara hii ni Fursa nzuri sana ikiwa tu itaendeshwa kwa Ufanisi na kwa kutumia vifaa vya kisasa, kwasabb NYAMA inalika kila kona ya nchi. Nataka nikupe mchanganuo mzima kuanzia Mtaji hadi FAIDA inavyopatikana.
View attachment 3235498
GHARAMA:
1. Frame: 150k × 3months (450,000)
2. Mashine ya Kukatia (1.2M)
3. Mzani Digital (Kg40) (120,000)
4. Freezer (200L) (800,000)
5. Visu, mifuko etc (100,000)
6. Mabango (500,000)7. Vibali E.g Leseni, Ukaguzi,Cheti cha Afya, Halmashauri (200,000)TOTAL= Tshs. 3,370,000
View attachment 3235497

Nyama machinjioni 1Kg =8,000
Tuseme utachuku Kilo 75.
75 × 8,000 = 600,000
Usafiri (machinjioni- buchani) 15,000
Jumlisha🙁Vifaa + mtaji wa nyama + usafiri)(3,370,000 + 600,000 + 15,000) + Umeme 5,000
Jumla ni 3,990,000/=

Assume kila siku utauza Kg 50 pekee na hizo 25Kg zitabaki. Ukumbuke sehemu unaweza kulipa kodi ya 150,000 kwa mwezi ni site nzuri, means bado ulikuwa na uwezo wa kutafuta Frame ya 70K au Laki moja, Lkn mimi nimekupendekezea utafute sehemu nzuri kodi 150K. Bei ya buchani = 10K+

Mahesabu:50Kg X 10,000 = 500K TOA Mtaji (50Kg)- 400,000 Mfanyakazi- 10,000
Usafiri hadi buchani- 15,000
Mifuko ya kufungia- 5,000 Umeme- 5k
Jumla = 435K
500,000 - 435,000 #FAIDA (Tshs 65,000)
Everday deposit Bank Tshs 40,000/= Remain with 25K
Kwa mwaka:40,000 X 365 Days = 14,600,000
Kumbuka hiyo ni Bucha moja tu, Times Two (02) butchery.14.6M × 2 = 29,200,000 within 1 Year.
Lengo letu miaka ni miaka miwili.29.2M X Two Years = 58.4Millions
Hapo nimekupigia mahesabu ya Bucha mbili pekee na kila siku utauza 50Kg
Tajiri mimi nakushukuru hili wazo tayari nilishaongea na My Wife.

Sina mtaji ila naanza kujikusanya kwa maeneo niliyopo nahitaji kama 2M tu.

Hiyo Mahsine ya 1.2M naachana nayo kwanza naanza na Mapanga na visu na gogo la Mti🤣🤣
 
Biashara ya nyama ya ng’ombe inalipa zaidi ukijihusisha na ng’ombe za deal😂 ila haki haki utachelewa
Una manisha ngombe za wizi?🤣🤣

Mtoa mada ametwambia unakunja elfu 40 kila siku.

Hajatwambia ada ya watoto unalipaje, kodi, chakula nyumbani na mlo wako binafsi kwenye hizo harakati.

Lakini ni wazo zuri watu wanaishi humo
 
Tajiri mimi nakushukuru hili wazo tayari nilishaongea na My Wife.

Sina mtaji ila naanza kujikusanya kwa maeneo niliyopo nahitaji kama 2M tu.

Hiyo Mahsine ya 1.2M naachana nayo kwanza naanza na Mapanga na visu na gogo la Mti🤣🤣
Hizo zana kijijini ndo zenyewe mashine umkatie mtu mifupa watakususia 😂
 
Kwa dsm mabucha yanauza at least

Mimi kule kijijini kwetu jumapili ukichinja ng'ombe wa kg 150 anaisha hata saa sita haifiki!

Katikati ya wiki unachinja mbuzi au kondoo hata mara mbili

Kwa kijijini kwetu uwe na moto na masufuria basi!

Wanaobisha sijui lkn my father was doing this hata mm nawish kuwa na bucha la kisasa lenye kila kitu so lzm niuze 50kg lkn kuloga muhimu 😂
Kwa hiyo wewe ni mtoto wa kigagula!
 
Wazo: BUCHA La NyamaCapital: 4MBidhaa: Nyama ya Ng'ombeKwanza, Biashara hii ni Fursa nzuri sana ikiwa tu itaendeshwa kwa Ufanisi na kwa kutumia vifaa vya kisasa, kwasabb NYAMA inalika kila kona ya nchi. Nataka nikupe mchanganuo mzima kuanzia Mtaji hadi FAIDA inavyopatikana.
View attachment 3235498
GHARAMA:
1. Frame: 150k × 3months (450,000)
2. Mashine ya Kukatia (1.2M)
3. Mzani Digital (Kg40) (120,000)
4. Freezer (200L) (800,000)
5. Visu, mifuko etc (100,000)
6. Mabango (500,000)7. Vibali E.g Leseni, Ukaguzi,Cheti cha Afya, Halmashauri (200,000)TOTAL= Tshs. 3,370,000
View attachment 3235497

Nyama machinjioni 1Kg =8,000
Tuseme utachuku Kilo 75.
75 × 8,000 = 600,000
Usafiri (machinjioni- buchani) 15,000
Jumlisha🙁Vifaa + mtaji wa nyama + usafiri)(3,370,000 + 600,000 + 15,000) + Umeme 5,000
Jumla ni 3,990,000/=

Assume kila siku utauza Kg 50 pekee na hizo 25Kg zitabaki. Ukumbuke sehemu unaweza kulipa kodi ya 150,000 kwa mwezi ni site nzuri, means bado ulikuwa na uwezo wa kutafuta Frame ya 70K au Laki moja, Lkn mimi nimekupendekezea utafute sehemu nzuri kodi 150K. Bei ya buchani = 10K+

Mahesabu:50Kg X 10,000 = 500K TOA Mtaji (50Kg)- 400,000 Mfanyakazi- 10,000
Usafiri hadi buchani- 15,000
Mifuko ya kufungia- 5,000 Umeme- 5k
Jumla = 435K
500,000 - 435,000 #FAIDA (Tshs 65,000)
Everday deposit Bank Tshs 40,000/= Remain with 25K
Kwa mwaka:40,000 X 365 Days = 14,600,000
Kumbuka hiyo ni Bucha moja tu, Times Two (02) butchery.14.6M × 2 = 29,200,000 within 1 Year.
Lengo letu miaka ni miaka miwili.29.2M X Two Years = 58.4Millions
Hapo nimekupigia mahesabu ya Bucha mbili pekee na kila siku utauza 50Kg
Biashara ya maandishi kuiweka kwenye fremu ni mtihani mwingine.....kikubwa umesomeka
 
Umepiga mahesabu ya kodi 3 months alafu unawela faida ya mwaka mzima?! How? Hiyo miezi mingine 9 unapanga bure? Hizo kilo 50 unadhani kila siku ni sikukuu? Ukijitahidi sana Kilo 20 shukuru! Angalau ukiwa mfugaji mwenyewe kidogo utaona faida.
 
Back
Top Bottom