Unaweza usiambiwe, ila sio vizuri kufanya mambo haya

Kwenye bufee usijaze sahani pomoni na usifike mwisho wa vyakula, chagua vyakula usivyovila mara kwa mara. Chukua chupa moja ya kinywaji inatosha. Usijioneshe unajua kula sana. Umekuta meza ina vinywaji vingi usinywe tani yako acha wenyewe watachukua vinywaji vyao. Usirudie kuongeza chakula hata kama hujashiba utaaibika na kuonekana una njaa kali na huwa huli kwako
 
But why?
Sina utani kabisa kwenye sekta ya chakula. Nakula hadi mwisho

Yaani chakula kabisa usile chote, kwanini? Unambakishia nani sasa wakati umeletewa ule na mtu uko na njaa? Au tuanze kupita vibandani kwanza unapiga zege ndio unaenda Kwa watu?
 
Bibi harusi usionekane unajua sana kucheza muziki, una mbwembwe za kulishana keki, meno njenje, macho kodo, shela umeshusha, huna aibu, wakati wa kula unakula kama uko kwako utaonekana ni muhuni na hutatulia ndoani
 
Umeenda kwa watu ukakaribishwa chai, pisi mbili za vitafunwa na kikombe kimoja inatosha. Usitake kula pisi zaidi na kikombe cha pili.
 
Ukikaribishwa kula, kama ni kujipakulia usipakue chakula kingi, pakua kidogo na usiongeze, kama ni kushiba kale kwako ushibe.
 
Yaani chakula kabisa usile chote, kwanini? Unambakishia nani sasa wakati umeletewa ule na mtu uko na njaa? Au tuanze kupita vibandani kwanza unapiga zege ndio unaenda Kwa watu?
Ukiniambia karibu kula tambua ya kwamba nikiamua kukaribia nakaribia kiukweli😅
 
Kuna wale wanajaza wali, hua nashangaa sana kwan makwao hua hawali?
Kwenye sherehe hua nachukua kitu ambacho kwa mazingira yangu hua n vigumu kupata mfano labla samaki na hasahasa bites na sio kujaza wali.
 
Ukiwa na miadi na mtu fika kabla ya muda mliokubaliana

Kushabikia Simba
 
Wengine wataweka msisitizo sana ukaribie mezani, ila kiuhalisia unachokiona hata hakiwatoshi, kuwa tu muumgwana uombe maji au juice.
Juice ya kazi gani mkuu, hapo maji tuu
 
Hil
HIli sikubaliani na wewe,kwenye msosi hapana.
 

Lakini si ulifanya kitu unachojisikia? Sasa hapo Kuna wenzio wangetupa au kubakisha hicho kipande kilichobaki kisa unamfurahisha mchumba...

Hii post aione kaka Lukas
 
Hili jambo lako na kaka Lukas mmenipa jukumu zito la kuhakikisha kinatokea, ndio maana naliangalia Kwa marefu na mapana yake.
Mambo yetu tuachie sisi wenyewe yatakuumiza kichwa bure🤸
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…