Sakasaka Mao
JF-Expert Member
- Sep 29, 2016
- 16,028
- 23,380
Maelezo haya yangelitolewa na mwanamme ingelikuwa ni agenda.Tukiwa tuandelea kujiandaa na tarehe 9 kuelekea uhuru wa Tanganyika nimeona nilete swali kama hoja pamoja na maswahibu yangu
Nafikiri mwaka ukiisha mnipe tuzo ya watesekaji bora wa mahusiano jf
Nipo na huyu Kijana mwezi wa pili sasa lakini Naona kama mapichapicha japo since tunaanza niliona ni mtu wa hivyo ila nikasema nimpe muda..
Huyu jamaa angu kwenye upande wa mawasiliano ni kipengele.. anaweza kujitahidi siku mbili mkawasiliana vizuri hizo siku zinazobaki sasa utasema ana mashetani.. halafu hayuko romantic yaani yeye hata kuita majina ya kimahaba hola naitwaga (mamtu) sawa haina tatizo maana nishazoea
Ila hii tabia yake ya kuwa kimya bila sababu ya msingi inaniumiza.. kuna kipindi ilipita siku 2 hatuwasiliani nikamtafuta kwa kutuma na kupiga simu hakunijibu.. na mimi nikakausha akaja kunitafuta tena yeye..
Sasa mimi inaniumiza nawaza au kwasababu jobless maana maandamano yamefanya nipoteze kazi nipo home tu labda ningekuwa na kazi ningekuwa bize.. maana unakuta unatamani kuongea na mpenzi wako ila haoneshi ule utayari ama ushirikiano inanifanya nakata tamaa
Ningeweza kumuacha lakini nimeona nijaribu kumvumilia mwisho wa siku naweza kujikuta nabadilisha mahusiano kila wakati.. ni kijana mwenzangu kanizidi mwaka 1 26/27
Nimeona naweza kutengeneza nae maisha maana wote ni vijana ila sijajua kwa upande wake kama ananihitaji
Naombeni njia za namna ya kuishi na mwanaume wa namna hiyo.. ambae anaweza kukunyamazia tu bila sababu..
Na kama hanifai pia mnaweza mkanambia
Lakini kutolewa na mwanamke, hata bila maelezo kutoka upande wa pili, mimi nahukumu!
Huyo 'mmeo' utoto mwingi kichwani, unamuona kama makamo yenu mnalingana mpo sawa, kumbe unakosea 'umeolewa' na mtoto sana kwako.
Wee ulisikia wapi mwanamke ananuniwa au kuringiwa, yaani anakuzira kabisa hadi siku mbili badala ya kukudekeza kiromance, haya ni maajabu ya dunia sasa!
Kama unataka na kama inavyoonesha kutokana na maelezo yako, unapenda amani, upendo, furaha pamoja na utulivu katika mahusiano, basi huyo jamaa hakufai, kuendelea naye huku ukijipa moyo ni kujipotezea muda wako, maana tabia ni kama ngozi, haiwezi kubadilika.
Hauwezi kuanza kupata manyanyaso ya mapema katika penzi changa, halafu ukategemea 'mkizeeshana' ipo siku utapata furaha kutoka kwa huyo mbinafsi wako, never on earth.