Unayeamini kwamba ajira hutolewa kwa kujuana, tuambie Magufuli alijuana na nani mpaka akawa Rais wa nchi

Mnaosema kama hauna mzito unaye fahamiana nae serikali/ shirika fulani huwezi pata kazi, haya mbona uncle magu alilamba uraisi na alitokea chato, kwanini wewe unaamini katika connection? Mbona uncle magu alitoboa bila ya connection?
Huwa unakaa na kuwaza kabla ya kuandika?
Huwa unafikirisha ubongo (critical thinking) kabla ya kuandika?.

Nilijua Memkwa ni changamoto kubwa kumbe hata BRN Ni changamoto kubwa sana katika taifa hili Kwa sasa
 
Mnaosema kama hauna mzito unaye fahamiana nae serikali/ shirika fulani huwezi pata kazi, haya mbona uncle magu alilamba uraisi na alitokea chato, kwanini wewe unaamini katika connection? Mbona uncle magu alitoboa bila ya connection?
Yaani wewe ni poyoyo sana, raisi ni cheo ambacho kinahitaji kujulikana/connection kuliko utumbo ulioandika

Kitendo cha kuwa mbunge connection ilihusika mpaka akapita kura za maoni - CCM

Kuwa waziri ni connection ya raisi aliyemchagua

Kuwa raisi ni connection (kura za maoni)

NB
Uraisi ni process ndefu (inahitaji maandalizi ya muda mrefu)

Nafasi zote aiizochaguliwa ni connection ambazo zilimuandaa kuwa raisi

Kuna unaona uraisi hauna connection tutajie mtu yoyote ambaye hajawahi kushika nafasi yoyote kubwa ya Uongozi kabla na kisha akapewa agombee uraisi

Pia imani yako bedo ni dhaifu, hata huyo aliyepata kazi kwa connection anamtegemea MUNGU ila connection ni sababu tu ya kupata kazi kama wewe usio na connection unavyofanya interview ili upate kazi
 
Mnaosema kama hauna mzito unaye fahamiana nae serikali/ shirika fulani huwezi pata kazi, haya mbona uncle magu alilamba uraisi na alitokea chato, kwanini wewe unaamini katika connection? Mbona uncle magu alitoboa bila ya connection?
Urais sio ajira. Ajira unaipata kwa academic qualifications na nafasi zilizopo, sio kwa kupigiwa kura
 
Mnaosema kama hauna mzito unaye fahamiana nae serikali/ shirika fulani huwezi pata kazi, haya mbona uncle magu alilamba uraisi na alitokea chato, kwanini wewe unaamini katika connection? Mbona uncle magu alitoboa bila ya connection?
hii nayo ni post? Hii forum sio tena home of great thinker, forum imejaa wajinga sana
 
Ila mimi naamini katika Mungu, kama wakati wako haujafika, haujafika! Ukifika unaona hizo connection zinanyooka zenyewe! Wapo watoto wa maskini kibao, anakueleza sikuwa na mtu, lakini nimepata ajira! Na kwenye familia yetu, sijui ukoo ni mimi pekee mwenye ajira serikalini. Ushuhuda wa utafiti fulani.
 
Back
Top Bottom