🤣🤣🤣Yani kashenzi sana kanalala ile sehemu ambayo wewe unalala wewe.
Kuna mda kanakuangalia kwa kukushusha na kukupandisha kwa dharau .
Kuna kamoja nilikafuga kenyewe kalikua kanakaa kwenye zulia tu yani hakataki kugusa chini .
Then nikitokea kananiangalia huku kamelala kwa madharau makubwa as if kenyewe nika boss kangu. Ukiangalia hakakua na mchango wowote kwangu zaidi ya kula vizuri mda mwingne zaidi yangu na kulala tu .
Tofauti kabisa na mbwa ambae anachukulia tatzo lako ni lake, kuna mda ata ukiishiwa pesa mbwa anajua ,anashare na wewe huzuni . Tofauti na paka anakuona kama kituko.
Hili nimelishangaa kwa kuku sana. Kuku ukisogelea banda lao kuna mlio majogoo wanautoa “kokokoo”. Hata kama upo ndani unajua kuna mtu kasogea karibu na banda.Kuku wanatofautiana tabia kama binadamu, pia kuku wanamtambua binadamu mbaya, wanatoa ishara kwa namna tofauti ya milio yao.
Wana kitu kama uwezo wa kusoma akili ya mtu. Hata kama wewe ni ndio unamfuga, siku ukimpangia tukio ambalo yeye haliyomfurahisha utashangaa hiyo siku anakukwepa hakusogelei karibu.Hasa Mbwa ni mwepes kumtambua mtu mzuri na mbaya
na pia Mbwa anapokutizama sana machoni ana uwezo wakutambua ikiwa humpendi au unampenda
Ukiona Mbwa anakutizama sana machoni ujue anakusoma hvyo
Mbwa ni chakula Bora kwa chatu Sasa mbwa anamchokoza chatu afu anakimbilia uelekeo wako🤣🤣🤣Mbwa akiona chatu anafunguka mbio hatari
Mbwa niliwahi kuwapoteza wawili waligongwa tu na nyoka wa kawaida
Paka akifanya kosa ukiwa unampiga Kuna mlio huwa analia wa kama kuomba msamaha bas hapo yakupasa umuachePaka na mmbwa huwa hawapotei kabisa wakisafirishwa hata umbali gani ilimradi uwe mji huo huo..
1990s tulishawahi kuweka paka mmoja kwenye boksi kisha tukamsafirisha mbali sana kama km 70 alitupwa bwawani maana alikuwa anadokoa mno mboga jikoni na kunya hovyo hovyo, baada ya siku 4 tulipofungua mlango asubuhi 06:00 hrs alikutwa akiwa amelala nnje ya mlango mkuu wa nyumba.
Mmbwa, Poppy mbegu ya kizungu aliyotoka nayo Mzee Brazil na kuifuga Morogoro, alikuwa mkali sana na alisababisha majeraha kwa wanafunzi na baadhi ya Watu. Alikuwa anakodishwa kuwinda wanyama porini ila bado alileta balaa. Mshua aliamua kumuuzia Rafiki yake kuepuka balaa aliyekuwa akiishi umbali kama km 52 ila baada ya wiki 1 mmbwa alitoroka na kurudi home.
Paka anafundishika tabia njema ila usijichanganye kumfungia ndani ukiwa pekeyako eti umpige, atakuua na usijesema sikukuambia tukikutana paradiso.
Sent from my CPH2387 using JamiiForums mobile app
PAKA...
Huyu anafugwa sehemu nyingi sana sanaaa
Anatumika kama urembo pia kama mlinzi dhidi ya wadudu waharibifu kama panya,
Kiufupi hili beef Lao halitokuja kuisha hata iweje..
Paka naye ni kiumbe anayepends starehe sana, asilimia kubwa ya maisha yake anayatumia kulala tu .
Jamaa hana mambo mengi akishiba analala zake.
Shida ya paka anapenda kudeka sana utakuta kalala juu ya kitanda chako au Kanyea unga hasa wakiwa bado watoto..
Hii nimeshuhudia personal...
In our childhood, mzee aliletaga paka mkubwa kabisa akiwa kwenye mfuko,yule.paka alikuwa ni tofauti kabisa na hawa wa kwetu mitaani mkia wenye manyoya mengi, uzito mkubwa, manyonya mengi mwilini! Alipendeza kumuangalia for sure..
Shida yake alikuwa jeuri wa kiwango cha kutupwa na alikuwa na urafiki na mimi na mzee wangu tu!
Wengine lilikuwa linawapa chechi sanaaa..!
Sikumoja bibi yetu yeye alikuwa ametoka akaacha mkeka wake chini then akaenda zake, kurudi anakuta paka hilo letu limelala kwenye mkeka wake lime relax...!
Ikabidi achuukue mfagio alitandike guess what!
Nilishuhudia paka akituna kama mpira unavyojazwa upepo then akamrukia mzee yule kifuani!
Bibi wa watu mpaka chini akaenda anabaki anapiga yowe tu mpaka mzee akaja anasema "acha acha"ndipo akaacha yule paka then likaondoka kijeuri taratibu kabisa.
Paka yeye kamwe hutamuona akizaa However mimi nimeshuhudia kwa macho yangu, na wala hahitaji msaada wa mtu anatafuta palipo na privacy atazaa
Kitu kama hicho kwa paka ni very rare kwahiyo nikajifunza kitu tangu that day.
Ingawaje yule paka alipotelea tu mtaani hakuonekana tena maskani I think alishakufa huko ..
Remember kucha za paka ni sumu kwa mwili wa binadamu hivyo usipende kucheza michezo na paka maana tabia zake ni ngumu kujua hata ukiamuangalia usoni ngumu sanaaa.
Tujifunze kitu
Paka ana kucha za aina mbili:- za kawaida (wengi hufahamu hizi) na kujikinga akiwa na hasira dhidi ya adui yake, hizi ziko ndani na kali sana.Nimefuga sana Paka na nilikuwa Rafiki mzuri sana kwake na pia nilikuja kugundua Paka anakucha ndefu kama vidole vyetu vya mikono
Uko sahihi mkuuPaka ana kucha za aina mbili:- za kawaida (wengi hufahamu hizi) na kujikinga akiwa na hasira dhidi ya adui yake, hizi ziko ndani na kali sana.
[emoji120][emoji120][emoji120]Okay[emoji1787][emoji1787][emoji1787] nilipouona huu uzi niliudharau lakini leo nikasema ngoja nione kilichoandikwa kumbe ni thread moja nzuri sana oky lets me share baadhi ya vitu juu ya hawa wanyama .
PAkA.
Huyu ana akili sana japo ni mbinafsi . Mara nyingi anapomkamata panya anapenda amchezee sanaaa na ndipo mwishowe aweze kumlaa . Mara nyingi huwafanya hivi kwa lengo la kumvunja panya mifupa yotee. Hivyo kila anapomchezea panya na kumuacha huwa anamuangalia je ni sehemu gani ya mwili bado inafanya kazi ili aendelee na zoezi la kumvunja .
- Paka jike Mara nyingi huwa na dume moja tu . Na hili dume mara nyingi huwa ni lile lilombikiri , sisemi madume wangine hawawezi kula mzigo . Ili dume jingine lile mzigo moja inabidi liwe na nguvu na mwanzoni lazima liangushe kipigo kikali sana kwa huyu jike. Na hapa ndiyo utakapo sikia mapaka usiku yanalia nyaaaaaau nyaaaaauu yakipigana lakini pia halii hutokea hata kwa lile dume la kwanza lilombikiri kwani kuna wakati kwasababu azijuazo jike mwenyewe kama vile kuchoka au kutotamani tendo kwani mara nyingi maani(mbegu) za paka dume huwa ni za moto sanaa na hupelekea paka jike kuungua pindi zinapomuingia wakati wa tendo ( ndiyo maana mara nyingi paka dume baada ya tendo ikishamuachia paka jike utamuona paka jike anagaragara chini ni kwasababu zile mbegu zinapokuwa zinaingia ndani zaidi ya paka jike hupelekea paka jike kuungua ) na kupelekea paka jike kuwa mkali na mwenye hasira sanaa ambayo hutaka kumjerui paka dume kwa kucha lakini mara nyingi hushindwa kwani paka dume kabla ya kumuingia huhakikisha kamdhibiti vyema kwa kumshikilia sehemu ya shingo na ndyo maana dume hupaswa kuwa na nguvu nje na hapo hawezi kula mzigo . Kwa wale mliowahi kukaa mabibo hostel hasa kule kwenye zile block za watu wa masters basi hili swala la paka kulana mzigo mbele za watu nadhani mtakuwa mmeliona sana na kuwa mashahidi juu ya hichi nacho kiandika hapa na hata wale ambao hawajawahi kuona paka wakifanya mapenzi nawashauri waende mabibo hostel wakajionee utaliii wa bure kabisaa .
hivyo paka jike kuna wakati hujikuta tu hataki kutoa mzigo kwasababu ya kuchoshwa na kuungua hivyo halii hupelekea dume kukasirika sana nakuangisha kipigo huku akimvizia paka jike azubae tu ili akamate shingo na kujilia zake mzogo . Maana paka mara nyingi ushikapo shingoni huwa anakuwa hana ujanja .
kuku
huyu mengi yameshazungumzia na wadau huko juu . Ila lakuongezea tu ni kuwa huyu usiku mdomo wake huwa na sumuu hivyo inabidi kuchukua tahadhari sanaa wakati wa usiku asije kukudonoa . Maana anaweza kukuachia sumu ambayo inaweza kukudhuru kiafya hapo baadae .
Jogoo na tetea .
Lakini bado tukiwa hapa kwenye kuku . Huku nikuulize shwari je umeshawahi kujiuliza kwanini ukiambiwa umkamate tetea inaweza kuchukua nusu saa pengine hata saa nzima kuweza kufanikiwa kumkamata au wakati mwingine ukashindwa kumkamata kabisa ? . Lakini jogoo anapo mfukuzia tetea huchukua dakika 5 au mbaka 10 kumkamata tetea ?..
Jibu .
Mara nyingi jogoo anapomfukuzia tetea . Pale kuna mchakato wa kibiolojia unaofanyika kama ilivyokwetu tu binadamu . Pindi ukutanapo na mwanamke huwezi tu kumvua nguo mwanamke na kuchomeka ni lazima umuandae basi sasa turudi kwenye mada yetu . Basi hata jogoo pindi anapomfukuzia tetea zile dk 5 au 10 za kumfukuzia tetea husaidia kumuandaa tetea kiakili na kimwili ili jogoo anapokuja kumuingia asiweze kumuumiza na kumchubua [emoji1787][emoji1787] ina chekesha lakini ndyo hivyo .
Mbwa .
Mengi yaliyosemwa juu ya mbwa na wadau yapo sahihi kabisa . Lakini cha kuongezea ni kwamba . Umfugapo mbwa nyumbani kwako basi na yeye huwa anatabia ya kuweka mipaka ya kiutawala tena hii hufanywa mara nyingi na mbwa dume ( kama ni wale wasiofugiwa bandani ) . Mbwa dume huweka mipaka ya kiutawala kwa kunya mavi au kukojoa kaskazini , kusini mashariki na magharibi ili kutoa ishara kwa mbwa wengine wageni na yeyete atakaye ikililia mipaka yake basi hapo kipigo kitamuhusu labda awe mbwa jike hapo msamaha utahusika kama mjuavyo tena
Njiwa wa nyumbani .
Jamani wengine naona tumezungumzia mbwa , ng'ombe punda lakin tumemsahau njiwa. Hawa nao wana tabia zao za kushanga sana .
1) mara nyingi njiwa hutaga mayai mawili tuuu . Na katika mayai haya moja huwa njiwa dume na jingine huwa njia jike .
2) njiwa hawa wawili hukuwa pamoja na kuwa wapenzi . Na pindi njiwa jike atakapo taga mayai swala la kuatamia na mayai ni shwala la wote . Na maanisha nini ? . Mayai yatahatamia na njiwa dume huku njiwa jike akiwa kaenda kitafuta chakula na kuna muda mayai utahatamiwa na njiwa jike huku njiwa dume akiwa kaenda kutafuta chakula hukuna kutegea na dume akileta tu utegezi kwenye kuatamia hushushiwa kipigo na njiwa jike vizuri tu na hii huendelea hata pindi wapatapo makinda shwara la kuwalisha ni swala la woteee ( hapa wanatufundisha mgawanyo wa kazi katika malezi )
3) hapo juu tumeona njiwa huwa wanakuwa wawili wawili toka utotoni mbaka katika maisha yao ya ukubwani . Sasa nini hutokea pindi njiwa dume anaondokewa na njia jike ??. Kimsingi kama aliekufa au aliyepotea ni njiwa jike basi inashauriwa ni bora ukamchinja huyu dume maana hali ya upweke ambayo hubaki nayo huweza kupelekea njiwa huyu dume hata kufa . Kwani humchukua muda mrefu sana kumpata mwenza mwingine . Lakini kama ni jike wala huwa hamnashida sana kwani hueeza kupata dume jingine mapema sanaa.
4) kama utafuga njiwa inashauriwa kila asubuhi ni bora ukawa unawarushia kiasi fulani cha nafaka kama vile mchele huku ukiwaambia mawili matatu . Hii itakusaidia pindi ukutwapo na majanga kama msiba kwani ukipata msiba unaweza kutumia ile fursa ya asubuhi kuwa wapa taarifa kuwa umepata msiba hivyo wakiona watu wengi na makele ya vilio wasistuke . Kwani usipofanya hivyo hupelekea njiwa kuhama na kuamia kwa mfugaji mwingine .
Nguruwe .
Wengi wamemzungumzia huyu . Lakini ningependa kuongezea kuwa kama utataka kumfuga huyu basi ni bora ukamjengea banda la juu kwa kutumia mabanzi au mbao . Kwani kama utatumia matofari ya kuchoma au ya cement basi inaweza kuwa hasara maana nguruwe akiwa na njaa huyageuza matofari kama chakula na kuyala .
- pua ya nguluwe ni ngumu kuliko hats uionavyo . Hutumia kufukulia hasa kwa yale mabanda ya chini yaliyosakafiwa na hata kusafisha banda lake pindi lijaapo kinyesi .
- wafugaji hawashauriwi kumzoesha kumpa mabaki ya nyama ya ng'ombe nguruwe kwani hii huleta shida sana pindi awapo na watoto wadogo . Kwani pindi atakapochelewesha chakula au akawa na njaa ya ghafla hupelekea kula kitoto chake mwenyewe .
- Samaki ni moja ya kitoweo kikubwa sana wakitumiacho wezi kumuiba nguruwe . Wezi huvamia banda la nguruwe na kutengeneza uwazi utakaomuwezesha nguruwe kupenya
. Baada ya hapo huchukua samaki aliyochwa na kumfunga kamba na kumuweka nje ya banda la nguruwe waliyedhamiria kumuiba . Pindi nguruwe aipatapo harufu ya samaki huyo basi huwafuata wezi hawa mwenyewe kimya kimya mbaka machichioni . Na kubaki wakikushangaza mfugaji imewezakana vipi kumbeba nguruwe mkubwa kiasi kile bila ya nguruwe kupiga kelele ???.
- miwa ni miongoni mwa chakula kingine akipendacho nguruwe . Hivyo usije kulima shamba la miwa karibu na wafugaji wa nguruwe utawalaumu bureee tu.
Nimeona niongee haya machache lakini pia ntafurahi kuona na wengine wakiongezea mengine na kuufanya uzi huu kuwa uzi bora kabisa mwaka 2024.
Kamba hiii... Hawezi kuwa na kucha ndefu kama vidole.. labda wewe una vidole vidogo sana hapa duniani. Muwe mnaangalia na uongo wenumNimefuga sana Paka na nilikuwa Rafiki mzuri sana kwake na pia nilikuja kugundua Paka anakucha ndefu kama vidole vyetu vya mikono
Sio kweli miaka na miaka wazee wamefanya hivyo na wapo tu
Anatakiwa pia kumwagiwa mkojo wa mama yake wewe unasema maji ya baridi unataka kumuua ndama?
Hata hivyo unaweza kumpangusa na kumfuta futa ila hii ndio the best ndama atakuwa ng'ombe bora sana
Ni ngumu kuielezea kwa maandishi ila Fanya majaribio haya mkuu:.
Mkuu mm nafuga kuku wa kienyeji natamani kujua hzo ishara na hyo milio unayoizungumzia
Hakika wewe ni mfugaji makini sana yaani umeeleza vitu ambavyo wafugaji wengi hawawezi kuvinotisi na ni uhalisia asilimia zote.Hili nimelishangaa kwa kuku sana. Kuku ukisogelea banda lao kuna mlio majogoo wanautoa “kokokoo”. Hata kama upo ndani unajua kuna mtu kasogea karibu na banda.
Jogoo ana akili sana. Jogoo analinda mitetea hata kumi pekee yake. Ukiwafungulia wakiwa nje wanaswampa, kila mtetea akitaka kutaga jogoo anamrudisha bandani akatage. Sijui wanawasilianaje kwakweli.
Ukiwawekea chakula jogoo hali kwanza anaacha mitetea ile hadi ishibe kisha yeye ndio anaingia kula.
Kwenye kuwapanda sasa😂😂😂anawapanda wote halafu sijui kila akishapanda anawaweka alama utaona anaendea ambaye bado mpaka wote waishe.
Kuku kama kuna muda ukifika unawafungulia nje, huo muda kila ukifika ukichelewa kuna milio wanatoa kukukumbusha kwamba ukawafungue. Na ukiangalia saa unakuta muda ni ule ule.
Nimejikuta naenjoy sana kufuga kuku.
Napenda sana ufugaji mkuu, na ninapenda sana urafiki na mifugo unakuta wakati mwingine napiga nao story kama wananielewa vile. Sasa hivi nina mbwa na kuku na ninajua tabia zao vizuri sana.Hakika wewe ni mfugaji makini sana yaani umeeleza vitu ambavyo wafugaji wengi hawawezi kuvinotisi na ni uhalisia asilimia zote.
Mimi kuna yule jogoo ambaye ni alfa male. Huwa nikimsikia mlio wake hata nikiwa ndani naelewa kabisa hapo kuna kitu amekiona na anatoa taarifa fulani.
Wakati mwingine unakuta kuna kikuku labda kinatoa mlio wa kuashiria hatari na kumbe hakuna hatari yeye atatoa ule mlio wa kama kuwapoza hapo wote watanyamaza tayari anakuwa ameona hakuna hatari ila ni uoga wao tu.
Ufugaji raha sana kama una passion.
Wewe tumia hiyo sayansi yako ya kukariri darasanj elimu ya helsb then sisi tutumie njia za miaka yote zinazofanya tumiliki mifugo isiyohesabika wewe miliki ng'ombe watatu then utumie hiyo sayansi kama hata faida utapataUnaleta knowledge ya wazee kwenye sayansi! hauko serious mzee........unaujua ugonjwa unaosababisha homa ya vipindi wa brucellosis, madaktari wa binadamu wengi hawautambui.......wanaweza kutibu malaria na typhoid hadi wakachoka. Ni rahisi kuambukizwa na majimaji ya ng'ombe aliyezaa yakiwemo hayo mnayoyonyonya kwa ndama......chukua hii kama ulikuwa hujui.
Aliyekwambia stimulation ya maji ya baridi inaweza kumuua ndama ni nani, ni hao hao wazee?........ongeeni na wataalamu msije mkajikuta kwenye matatizo yasiyojulikana kwa kuendeleza mambo ya wazee.