Unazingatia Vitu gani kabla ya kuingia kwenye Ndoa?

Mimi napendekeza namba 1 ibadilishane na namba 3 au itoe tu namba 1 kisha namba 3 ipandishe hapo 😅
 
Aisee, wengine tumejikuta tu tupo ndoa ndoani...hayo mengine yanajiseti yenyewe! Mungu ana mipango yake katika kila hatua ya mwanadamu. Mimi ukinirudisha leo sekondari ukaniambia nichague cha kufanya, labda ningetamani kuwa Kasisi wa Kikatoliki (Padre)....lakini acha tu nikomae na ndoa yangu, maana ndiyo 'msalaba' wangu!
 
Kwa matukio niliopigwa sina hata hamu ya kuingie kwenye mahusiano Wala ndoa.
 
Watu WASALITI sio KE sio ME wanagawa gadi kwa idadi weeeh Thubutuuu!!
Wengine viburi, ujuaji na kupiga.!!
Mi NITAJIOA nikitaka mtoto nitatafuta wa ku adopt
Juzikati nilikuwa nimekaa sehemu na mzee fulani akawa ananiambia yanayomsibu Kwenye ndoa yake.

Aliniambia yeye na mkewe hawapatani kbsa japokuwa wanaishi katika nyumba moja lakini wamegawana vyumba kila mtu na chumba chake.

Aliniambia yeye anajipikia chakula chake naye make anajipikia chake.
 
Swadakta, 💯. Mwanaume hupaswi kuangalia suala la kiuchumi la mwanamke. Kuna hili suala la mwanaume kukwepa wanawake wenye UCHUMI mzuri kwa kuhofia dharau kutoka kwa wenzi wao. Wee unakionaje hili kwako unaliangalia pia?
Nadhani ni hofu ya dharau na kutoheshimika kama ulivyosema. Wengi wa wanawake waliohuru kiuchumi wanajisahau sana, wanashindwa kutenganisha career na familia, hilo linawa-cost sana!
 
Alikwambia tatizo ni nini??
Hizi ndoa zina mambo mengi sana.!! Sasa hao wanaishi hivyo km watu ambao hawakuwahi kupendana?!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…