Undumila kuwili wa wamaagharibi mgogoro Gaza, Putin Dume!

Tatizo lilopo Palestina ni la muda mrefu kutokea kwenye unyakuzi wa maeneo yaliyokuwa ya wapalestina kufanywa taifa la Israel. Pia unyakuzi wa maeno zaidi ulioendelea kufuatia vita mbali baina yao 1967 na 1973.

Duniani kote watu wanaandamana kupinga ulipizaji kisasi wa Israel kwa wapalestina wote, kwa vita vyake na HAMAS:

View: https://m.youtube.com/watch?v=0bfIBhWquTU

Uingereza imepiga marufuku kunyanyua bendera ya HAMAS hadharani, lakini bado zinapanda. Maandamano ni kwingi duniani. Tokea mashariki ya mbali, kati, ya magharibi hadi New York huko, ni maandamano mtindo mmoja na si madogo.

Syria, Lebanon na West Bank kumeshakuwepo makabiliano (ya moto) na makombora mazito mazito. Huko ni maeneo mapya ya makabiliano.

"Hezbollah (Lebanon) Kwa hakika wapewe maua yao kwa kusimama na wapalestina kwa vitendo vikamilifu katika wakati huu mgumu." Bila kusahau Iran iko na Palestina na Hizbolla. Na Iran Iko na Urusi.

"Revenge or collective punishment" ni haramu kokote kulikostaarabika. Katibu Mkuu UN anasema hata vita zina sheria zake. Kwamba haki za binadamu na natural justice lazima kuheshimiwa.

Marekani na washirika wake wameapa kuiunga mkono Israel kwa lolote. Bila shaka "lolote" ni kwa maana yake kamili.

"Putin amekuwa wazi. La muhimu Sasa hivi ni kisisitiza vita kusimama mara moja. Bila kusahau historia ya mgogoro huu kwenye ni kwenye uvamizi wa ardhi ya Palestina."

Maneno kuntu kabisa kutoka kwake Vladimir Putiin, (pamoja na ukakasi Ukraine) rais wa Urusi.

"Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni."

Kwa hakika Nyerere, Mandela, Tutu na wa namna hiyo wangekuwapo, wangesha walaani Israel na kuwaunga mkono Palestina. Kwa hakika wangekuwa wameyafanya hayo hadharani na mchana kweupe.

Uzi huu unahusika:

Kama tunataka Katiba Mpya, Tusiionee "Haya" Haki ya awaye yote

Unamuongelea Putin yupi mkuu? Huyu kiungo wa Simba au yule anayepekekeshwa puta na Mr Zelesky? Hao Hizbullah soon watakipata wanachokitafutana usije kurudi tena hapa na misemo yenu " Pray for Lebanon"
 
"Revenge or collective punishment" ni haramu kokote kulikostaarabika. Katibu Mkuu UN anasema hata vita zina sheria zake. Kwamba haki za binadamu na natural justice lazima kuheshimiwa.
Upo sahihi kwa hili...
 
Wengine wanasubiri unabii utumie,
Kwamba wayahudi watajikusanya Dunia mzima na kufanya ufisadi mkubwa na Kisha kutwaa msikiti ,
Ila mwisho msikiti utakuja kutwaliwa tena kutoka Kwa mayahudi.
Hivyo huu ni mlolongo wa matukio lakini Bado ufisadi utaendelea.
Kudos Kwa Putin apewa maua yake ila sio mkombozi ktk huu mgogoro.
Huu unabii nani ameutoa?
 
Mnamganda sana putin ila yeye anawakataa. Kama kweli yuko pamoja na waarabu apeleke jeshi kama alivyofanya Ukraine.
 
Nimekuwa nikiangalia Maandamano huko New York nimefurahishwa sana na Demokrasia Waisraeli na Wapalestina wote waliandamana kwa AMANI.

Lakini hebu Imagine kama Wayahudi wangeandamana Iraq au Yemen au Saudi Arabia for sure wangeuwawa huku watu wakichant Alaahu Akbar

Umeona tofauti?
Si mfano mzuri, Waarabu ni first party na Israel ni first party, Marekani ni 3rd party.

Urusi ambaye anamuunga mkono Palestina pia kuna wayahudi wengi tena wafanya Biashara wakubwa kama Avram, Tanzania, Kenya, Uganda kote kuna mashabiki wa pande zote mbili.
 
Mnamganda sana putin ila yeye anawakataa. Kama kweli yuko pamoja na waarabu apeleke jeshi kama alivyofanya Ukraine.
Unahisi Hamas wanachofanya sasa hivi kulipua ndege na kuaibisha IDF ni uwezo wao? Hamas wapo well Equiped wametoa wapi hizo Silaha, wana silaha za kisasa za Marekani ambazo zilipelekwa Ukraine wamezipata wapi?
 
Onesha official statement kutoka kwenye serikali ya urusi kwamba wana waback Palestinians na watapeleka silaha kama marekani alivyofanya. Achana na silaha za kusmuggle
 
Ushindani na mwenye nguvu unachotakiwa ujifanye mjinga. Panga karata zako weka malengo ya muda mrefu ndo uje u attack. Wapalestina wangetumia majanga yao kusoma na kuzamia nchi za first world kwa kusaka refugee asylum. Na kuingia kwenye system zao. Then ndio wangeweza kuishinda Israel. Maana waisraeli kinachowabeba wako kwenye system zote za dunia. Wapalestina wamejitahidi lakini wamejiamini mapema sana.
Wapi Israel wapo wapalestina hawapo?
1. Waziri mkuu wa Scotland analalamika mama mkwe wake amekwama Gaza, ni wapalestina hawa wana Cheo kikubwa tu Scotland.

2. Nenda Usa kuanzia kina Hadid, hadi kwenye MA engineer wakubwa Wa nyuklia unawakuta wapalestina,

3. Nenda South America RAISI El Salvador Mpalestina, Makamu Raisi Honduras Mpalestina, wana mabiashara makubwa na ni Mabanker wakubwa wakubwa wenye pesa za maana.

4. Ukija Nchi za kiarabu kuna wapalestina kibao mawaziri na vyeo vikubwa.

Issue hapa ni Uzayuni, hawa Zionist ni wakubwa kuliko Israel na Palestina ni wakubwa kuliko Uyahudi wana agenda zao nyengine kabisa.

Kuna wa Israel wengi mno hawaitaki hii vita leo tu asubuhi nimeona video ya orthodox jews wakiwa suppressed na IDF sababu ya kupinga vita.

So issue ni uzayuni na sio Palestina.
 
Onesha official statement kutoka kwenye serikali ya urusi kwamba wana waback Palestinians na watapeleka silaha kama marekani alivyofanya. Achana na silaha za kusmuggle
Sawa kaa isubirie hio official statement nchi ikikiri imesaidia kikundi kisicho kuwa na mamlaka.
 
Unahisi Hamas wanachofanya sasa hivi kulipua ndege na kuaibisha IDF ni uwezo wao? Hamas wapo well Equiped wametoa wapi hizo Silaha, wana silaha za kisasa za Marekani ambazo zilipelekwa Ukraine wamezipata wapi?
Putin mwenyewe alikua ndani kajifungia ahhhahh alivyoona Americans wameelekea middle east jamaa akatoka chap kwenda pale kyrgstan ata hana habari na waarabu wanaokufa gaza zaid ya matamko. 😀😀
 
Tatizo kwa Hawa wenzetu Waislam liko kwenye mafundisho ya Mtume Mohammad wao. Anafundisha chuki. Na hata watu wengine wa dini za Kikiristo, Hindu, Buddha hatuko salama.
Umeandika ukaingiza chuki zako..
 
Myahudi atawatesa mpka ujio wa masihi. Na ukichokoza acha ushuhulikiwe sawa sawa
Sawa na wewe endelea kushabikia wazayuni mpaka masihi aje, mtu ambaye anasema kila siku mtu mweusi hapaswi kukaa bila kufanywa mtumwa.
 
Tatizo lilopo Palestina ni la muda mrefu kutokea kwenye unyakuzi wa maeneo yaliyokuwa ya wapalestina kufanywa taifa la Israel. Pia unyakuzi wa maeno zaidi ulioendelea kufuatia vita mbali baina yao 1967 na 1973.

Duniani kote watu wanaandamana kupinga ulipizaji kisasi wa Israel kwa wapalestina wote, kwa vita vyake na HAMAS:

View: https://m.youtube.com/watch?v=0bfIBhWquTU

Uingereza imepiga marufuku kunyanyua bendera ya HAMAS hadharani, lakini bado zinapanda. Maandamano ni kwingi duniani. Tokea mashariki ya mbali, kati, ya magharibi hadi New York huko, ni maandamano mtindo mmoja na si madogo.

Syria, Lebanon na West Bank kumeshakuwepo makabiliano (ya moto) na makombora mazito mazito. Huko ni maeneo mapya ya makabiliano.

"Hezbollah (Lebanon) Kwa hakika wapewe maua yao kwa kusimama na wapalestina kwa vitendo vikamilifu katika wakati huu mgumu." Bila kusahau Iran iko na Palestina na Hizbolla. Na Iran Iko na Urusi.

"Revenge or collective punishment" ni haramu kokote kulikostaarabika. Katibu Mkuu UN anasema hata vita zina sheria zake. Kwamba haki za binadamu na natural justice lazima kuheshimiwa.

Marekani na washirika wake wameapa kuiunga mkono Israel kwa lolote. Bila shaka "lolote" ni kwa maana yake kamili.

"Putin amekuwa wazi. La muhimu Sasa hivi ni kisisitiza vita kusimama mara moja. Bila kusahau historia ya mgogoro huu kwenye ni kwenye uvamizi wa ardhi ya Palestina."

Maneno kuntu kabisa kutoka kwake Vladimir Putiin, (pamoja na ukakasi Ukraine) rais wa Urusi.

"Mnyonge mnyongeni haki yake mpeni."

Kwa hakika Nyerere, Mandela, Tutu na wa namna hiyo wangekuwapo, wangesha walaani Israel na kuwaunga mkono Palestina. Kwa hakika wangekuwa wameyafanya hayo hadharani na mchana kweupe.

Uzi huu unahusika:

Kama tunataka Katiba Mpya, Tusiionee "Haya" Haki ya awaye yote

Hamas watandikwe ndio njia pekee ya kuishi na mwarabu
 
Sawa na wewe endelea kushabikia wazayuni mpaka masihi aje, mtu ambaye anasema kila siku mtu mweusi hapaswi kukaa bila kufanywa mtumwa.
We kwanini usilalamikie madhila ya waafrica wanachofanyiwa na waarabu hapo dafur Sudan au wewe akitajwa mwarabu unaona katajwa mtume. Miafrica bure kabisa
 
1. Hilo ni Eneo la vita,
2. Hakuna Muisilamu ama mwarabu anaeshabikia hivyo vitu, huo ni uhalifu kama uhalifu mwengine.

Hapa tunaongelea Apartheid ama uhalifu ambao upo backed na Dini/Nchi.

Kuna watu weusi wengi tu Nchi za kiarabu wenye vyeo vikubwa hadi viongozi, Wa nchi, hivyo hakuna ubaguzi wowote uliohalalishwa na Katiba ama viongozi,
 
Kuna watu wanafiki humu sijawahi kuona
Masai wanahamishwa na kuuwawa wana tofauti gani na Palestine wanaotolewa Makwao
Halafu mtu anashangilia

Aborigines na Red Indians na Kurds wana tofauti gani mbona tunakuwa warahisi kusahau hivi
Acha nipumzike tu
 
Back
Top Bottom