Mr Ezek
JF-Expert Member
- Nov 7, 2023
- 298
- 105
Salaam Afrika ,Salaam Wana na Binti wa mama Afrika,Enyi watu wake aliyewaridhia.ni ndoto ya kila mwafrika wa kweli mwenye maono ya ukombozi kuona waafrika wanakuwa kitu kimoja,wanakuwa taifa moja na wenye nia moja.
Huu Uzi huenda ukawa ni upumbavu kwa wengi ila ninauandika kwa tafakuri na nia ya dhati katika kuendeleza na kuyaishi mawazo ya wazee wetu hayati Kanali Muhammar Gaddafi na hayati Nkwame Nkrumah juu ya KUJENGA TAIFA MOJA LA AFRICA LENYE NGUVU NA USTAWI MKUBWA.hakuna ukombozi wa Afrika pasina muungano wa waafrika,hakuna amani Afrika pasina nguvu ya pamoja ya waafrika.tumebarikiwa kuwa na rasilimali vitu ila tumekosa rasilimali watu,ni huzuni kwa wana na binti wa Afrika na hata ni ngumu kufikirika wanakufa maskini katika nchi ya asali na maziwa.
Nilishawai kutafakari msemo mmoja "ukiwa baba mwenye mji na watoto wanakimbia nyumba yako na kwenda kuishi kwa jirani,kama baba jua kuwa hapo kwako kuna matatizo makubwa". watoto wengi waafrika wanakimbia mataifa yao na kuvuka bahari kwa nia ya kuusaka mkate,yote ni kwa sababu ya umaskini unaosababishwa na uongozi usio na dira na nia njema.
Fikra zangu juu ya ukombozi wa kweli wa waafrika zipo katika umoja wa waafrika katika taifa moja lenye NGUVU lenye serikali moja,jeshi moja ,pesa moja na sauti moja kimataifa.kwa Sasa bado sisi ni watumwa tulio na uhuru usio kamili, hatuwezi kusimama kama nchi moja moja kujitetea na kupambania maslahi yetu.Afrika Inahitaj sauti yangu na yako katika kukipigania kile Hayati Gaddafi na Hayati Nkrumah walichokuwa wamekiona.
Ukweli ni kwamba ukombozi wetu utakuja pale tu tutakaposimama kwa ndugu tukishirikiana katika kuijenga Afrika yetu .ninaona mbali na kufikiri juu ya faida ya sisi vijana wa kizazi hiki kupambania jambo hili,Mimi ni miongoni mwa vijana kutoka Tanzania ninayeishi katika mawazo ya wazee wetu Hayati Gaddafi na Hayati Nkrumah, MUNGU wa baba zetu awarehemu wazee hawa kwa nia Yao ya dhati katika kuiunganisha Afrika.inawezekana ,kwa pamoja tunaweza na hakika muda wa kuanza ni sasa, Afrika iwe moja isiyo na mipaka.ninaona fursa nchi katika United States of Africa,ninaona amani, ninaona umoja utakaonufaisha waafrika kwa rasilimali zao.insha'Allah siku moja nitaipeleka Tanzania katika United States of Africa.