United States of Africa - ndoto itakayotimia

United States of Africa - ndoto itakayotimia

Afrika ilikuwa moja,ni Berlin Conference ilituweka kwenye hii mipaka ya kubuni,kwa hiyo wazungu wamekuwa kama baba zetu kwa kutukatia vipande kama baba amkatiavyo mwanae eneo kwa ajili ya urithi.

A
Kwenda zako huko
Unafikir hatujasoma history
Haikuwa nchi Moja
Acha kupotosha
 
Sasa huo umoja hauwezekan kamwe
Kwangu inawezekana,wanaoutaka umoja huu ni raia wa Afrika kama Mimi na wapi wengi ila viongozi hawa wazaliwa wa miaka ya 60 ni vikwazo ila kwangu Mimi kama kijana mwenye nia njema na waafrika na kesho ya Afrika yetu nikipewa nafasi ya uongozi wa juu hakika kwa uwezo wa Mwenyezi MUNGU sitaiacha damu ya Gaddafi iende bure nitalipigania ili kwa sababu Afrika hii ya Sasa Ina vijana wanaojitambua,wew angalia kwenye issue ya Traore jinsi waafrika sehem mbalimbali walivyomsupport
 
Kwenda zako huko
Unafikir hatujasoma history
Haikuwa nchi Moja
Acha kupotosha
Inayokuathiri ni elimu uliyonayo,jinsi Mimi ninavyoona ni tofauti na wew brother,jinsi ninavyoweza ni tofauti na wew unavyoweza ,wew unaona haiwezekan mm ninaona inawezekana,kijana ni hiv "being in the United States of Africa is more realistic than being in the heaven".
 
I
Again, Unalinganisha nchi na bara.

Marekani ni nchi iliyopo bara la Marekani ya Kaskazini.

Bara la Marekani ya kaskazini ni bara la tatu kwa ukubwa.

Bara la Marekani ya kaskazini lina nchi 23.

Mojawapo ya nchi zilizopo kwenye bara hilo ni Marekani.

Kulinganisha nchi ya Marekani na bara zima la Afrika si sahihi.

Ingekuwa sahihi endapo ungelinganisha bara la Marekani ya kaskazini na bara la Africa.

Ukitaka kulinganisha nchi ya Marekani na nchi ya Nigeria, hapo sawa maana zote zina muundo unaofanana.

Linganisha bara kwa bara na nchi kwa nchi!

Endapo bara la Marekani ya kaskazini lingekuwa nchi zake zote zimeungana na kutengeneza nchi moja, hapo ndo ingekuwa sahihi kulilinganisha na bara la Afrika.

Lakini kulinganisha nchi moja iliyopo ndani ya bara la Marekani ya kaskazini na bara zima la Afrika lenye nchi zaidi ya 50 si sawa.

Au hujui tofauti ya bara na nchi?
Ni nani aliyekuletea concept ya Bara na Nchi?
 
Kwenda zako huko
Unafikir hatujasoma history
Haikuwa nchi Moja
Acha kupotosha
Wew ni mwafrika uliyechoka,you don't have passion,umepoteza matumain yote ni sababu ya watawala wako,oooh ni nani atapambania waafrika na Afrika kama sio wew kijana?,huwaoni vijana wa kiafrika wameamka wanaitaka Afrika yao?,Mimi ni muafrika Mimi ni damu ya mababu wa kiafrika,Afrika ni urithi wetu vijana wenye maono wanajua ni nini Cha kufanya.HATUWEZI KUWAACHIA WAJINGA WATAWALE NCHI HII YA AFRIKA.
 
Afrika ilikuwa moja,ni Berlin Conference ilituweka kwenye hii mipaka ya kubuni,kwa hiyo wazungu wamekuwa kama baba zetu kwa kutukatia vipande kama baba amkatiavyo mwanae eneo kwa ajili ya urithi.

A
Africa hatujawahi kuwa kitu kimoja,tulikua na nchi zetu tena Africa kulikua na nchi nyingi zaidi ya 54 tulizonazo sasa,hii ni kwa sababu nchi zilikua katika muundo wa makabila na machifu ndio walikua maraisi,,kwa mfano nchi ya kisukuma,nchi ya kizaramo,nchi ya kimwera,nchi ya kizulu,nk.. kwahiyo sio kweli kwamba Africa tuliwahi kuwa wamoja sio kweli..ila baada ya ukoloni wa wazungu ndio zikapatikana nchi 54 za Africa ambazo ndio zipo Hadi leo...kidato Cha kwanza somo la history Kuna topic inaelezea mambo ya African states ukirejea hii topic utaelewa ninayoyasema,,,, kwahiyo Africa hatujawahi kuwa kitu moja na haitawezekana kutokana na sababu nyingi tu...japo ni wazo zuri Africa kutaka kuungana ila haiwezekani
 
Back
Top Bottom