Unyama huu wanaoufanya Polisi utamgharimu Rais Samia

Sawa, I am sorry sipo hapa kubishana Wacha yatukute
 
Hakika
 
Mwambie kijana wako aepuke makundi
 
Na wewe unayetetea panya road subiri Siku wakuvamie, wakucharange mapanga na kuwabaka ndugu zako ndio utaelewa...
Mtu nitafute Mali kwa jasho halafu waje wao kunipora na kunidhuru mwili!!! Wauwawe tumechoka kuishi kwa hofu
 
HILI LA KUUA PANYA ROaD SIO SAHIHI.. kila mtu asikilizwe na ahukumiwe na sheria mahakamani. Mtu akifa unaweza kumpa hatia yeyote hata kama aliuliwa kwa makosa...
Ile tume ya kuangalia Jeshi letu ifanye kazi kwa haraka..
sijui kama umewah kuibiwa wewe, tena hao police wanafanya kazi. Huku kwetu tunap
eleka wezi wanatoa Tu. Mpaka nataman tuwe tunapiga tunaua Tu. Hata wakihukumiwa miezi 6 au mwaka wakirudi tabu iko palee pale. Ukiona mtoto kashakua kibaka Hana dawa zaidi ya kifo. Wanakera sana
 
Kwa hiyo bw Robert, ukikutwa na na panya road, adhabu yako ni kifo?
Huwa nasoma makala zako nakuona kama ni mtu mbobevu,
Kumbe unashabikikia uuwaji wa watuhumiwa,?
Mahakama zifutwe ili police watoe hukumu kwa watuhumiwa,
Kwa komenti au post za wachangiaji wanaunga mkono police kuua watuhumiwa kisa wakifika polisi wanatoka huku wakisahau kuwa kama rushwa ndio chanzo cha kuwatoa nje hao police ndio huwashika wahalifu ili wapate pesa na wakipata huwaacha huru bila kuwapeleka mahakamani ili uwe mchezo endelevu.
 
Kwa maelezo ya hapo juu nawaunga mkono polisi, labda ungesema vijana wanakamatwa majumbani kwao wakiwa wamelala..
Watu wanafuatwa ndani usiku wa maneno.
Police jamii au sungusungu wakisema tu au kupeleka list ya wahuni wa mtaa polisi basi hapo kifo unacho.
 
Wengi hawajui kinachoendelea huko mitaani.
Kijana anafuatwa kwao usiku wa manane. Baada ya siku mbili tatu ndugu wanafuata maiti Muhimbili.
Hebu watu tuwe na utu. Kwanini tunakuwa kama wanyama
 
Watu wanakwapua mipesa ya umma na kujinunulia ma harrier , nako mtaani huwapa heshima kuwa ni ma fighter kumbe ni wauaji maana pesa zilizokwapuliwa zingeboresha huduma za afya na kupkoa uhai
 
Mlilalamika polisi hawafanyi kazi. Sasa mnalalamika wanapofanya kazi.
Mtoa mada umejuaje kuwa hao wanaouwawa sio panya road? Elekeza polisi panya road walipo.
Naona uko mbali na mada.
Police ni lini wamepewa authority ya kuua?
Ni chombo kipi kina idhini ya kutoa hukumu ya kifo?
Kama kila mkosaji auawe je, kibaka na fisadi wa mabilioni yupi alipaswa kuwa wa kwanza kuuawa?
Sasa hivi sungusungu wakipeleka jina lako polisi kata kuwa ni miongoni mwa vijana wavuta bangi basi utafuatwa na ndugu zako wataifuta maiti yako Muhimbili.
Haya endeleeni kushangilia mauaji.
Hata siku moja sitashangilia mauaji maadamu nina akili timamu
 

“hakuna kitu kinauma Kama unatafuta kwa jasho alafu mtu anakuja kukupora, kukusababishia ulemavu au kukuua kabisa ili tu akunyang'anye mali yako”
 
Acha wafyekwe wanachosha hawa wehu wanaogofya watu wema, wanaua watu wasio na hatia,wapuuzi kweli hawa je wakichekewa chekewa unadhani huko mbeleni itakuwaje?
 
Nilijibiwa kashfa mnooooo kwamba ninatetea wahuni ila najua Tanza-nia Polisi ndio wahuni zaidi
Hao "wahuni" siku wasipokuwapo hautaupata hata huo usingizi kwenye hiko kitanda unachotypia hizi comment. Ni kawaida ya binadamu ku-take something for granted pale kinapokuwepo.

Siku hao Panyaroad watakapo-take over utajua "mhuni" zaidi ni nani, maana hata hiyo simu ya kutypia na kupost humu hutakuwa nayo, achilia mbali mikono.
 
Excellent kabisa wako watu kipuuzi kabisa wanafikiri kwa kutumia makalio.
 
Tushukuru nchi yetu hairuhusu kumiliki risasi kiholela,hawa panya road wangesumbua zaidi ya hapa! Imagine umetoka out kula na girl wako afu mvamiwe na paka road!!!
 
Binafsi nishachoka kulala na tv chumbani kila siku kazi ya kuihamisha tu kuwaogopa hao vibaka,polisi wafanye kazi yao sasa maana tulishaanza kuwalaumu kwa matukio ya wizi huku mitaani

[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…