Mcanada
JF-Expert Member
- Jun 8, 2020
- 982
- 1,942
Umetisha sana kaka mkubwa, uncle wangu mmoja walimuua hapo Tanzania mwaka 2021 na hao hao panya road anawatetea huyo mtoa mada.. nasisitiza wauliweeeeeWewe nae haueleweki. Hakuna mtu anayefurahia kuona hawa madogo wanadhibitiwa kwa style hii ila ndio namna rahisi iliyopo ya kuwanyoosha. Wewe unadhani vile wanavunja maduka ya watu hata mara 4 kwa wiki na kuacha majeraha na kudhuru watu kuwatia vilema ni jambo zuri?!
Sasa wewe jifanye mwanaharakati za binadamu. Hao vijana unaosema wanajivutia bangi na sio wahalifu wewe una uhakika gani na ushahidi upi namna wanayatumia masaa yao kwa siku?!
Hebu siku tukupeleke kwa watu wenye makovu ya mishono mwilini ujionee hao vijana walivyowatukutu na wasivyostaili kuachiwa waendelee kupumua.
Ugaidi huanza hivi hivi kwa watu kama wewe ambao haujawi pitia au kuexpirience shambulio la hawa wahalifu kutetea kuwa haki za binadamu zinakiukwa.
Kama ni haki yao kuishi pia basi ni haki yao kuishi kwa kuheshimu raia wengine na kutii sheria. Maisha ni magumu kweli na ajira ngumu ila sio excuse sasa yakuwa mhalifu na kudhuru watu wengine.
Hivi wewe mtu anaenyanyua panga na kumkata mtu asiyemjua na hajamkosea lolote kwasababu ana hasira ya ugumu wa maisha na analenga kumnyang'anya mali yake utakuwaje na huruma na mtu wa hivyo?!
Wewe subiria siku mkeo, baba au mama yako, kaka yako, dada yako itokee kashambuliwa na uvamizi wa hawa wahuni uone majeraha ya kukatwa mapanga vidonda vibichi vikitoka damu na mishono ya nyuzi sehemu za usoni ndipo utavuta picha ya ukatili uliofanywa na hawa jamaa na ndipo utajua kwann serikali kupitia jeshi la polisi wameamua kuwa aggressive na hao takataka.
Jambo lingine usije ukadhani askari wanaruka tu kuja kukamata vijana hovyo bila kuwa na background data. Mtoto wako kama ni muhalifu kila mtu atamuona kwa mwenendo wake na tabia na hata hao wahuni wanapokamatwa huwa wanataja wenzao. Ni ngumu muhuni kumtaja mtu asiyemjua na asiye na mazoea nae ambae hawashindi pamoja. Wanapo kamatwa na kutiwa mbaroni sura zao zinatia huruma sana unapowatazama utasema hawa vijana mbona wanaonekana ni waadilifu ni maisha ya kipato cha chini tu yanawapa muonekano mbaya sasa wewe ngoja ukutane nao eneo la tukio la uhalifu ndipo utajua kuwa shetani akimvaa mtu nini huwa kinatokea.
So funga tu bakuli lako na uwe muungwana kwa jamii yako. Nenda hospital ya temeke mwambie nesi naomba unionyeshe majeruhi wa matukio ya panya road then uone kama utaendelea kuongea haya maneno yako ya unafiki.