Unyama huu wanaoufanya Polisi utamgharimu Rais Samia

Unyama huu wanaoufanya Polisi utamgharimu Rais Samia

Hapana mkuu...kumuua mtu bila uthibitisho sio fair...Pia kumbuka kuna watoto wadogo wasiojitambua wanatumiwa.
Hata kukiwa na uthibisho hakuna Sheria inayosema akibainika apigwe risasi hapohapo, tunafika huku kwa sababu ya malezi mabovu, haya matukio hapa dar hayajaanza Leo na zipo familia zinabariki matukio haya kwa kula na watoto wao, zipo familia hata baada kuambiwa mwanao anajishughulisha na haya mambo hata hawaangaiki, Kuna vikundi mtaani mpaka vimejipa utawala na vinaogopeka mtaani na ni vitoto vidogo tu . Watoto shule hawafiki kutwa wanashinda machimbo, kwenye vijiwe na mzazi hajishughulishi kumfatilia mtoto sasa nani unategemea akusaidie kulea
 
Habari!

Miaka 5 hivi imepita tulikuwa tukikemea mambo fulani mtandaoni. Kitendo cha serikali yenye zaidi ya vyombo sita vya usalama na haki kujichukulia sheria mkononi.

Serikali ifuate procedure katika kila zoezi, kama sheria itamtia mtu hatia na kuhukumiwa kuuawa auawe, kama itamfunga jela afungwe kama itamwacha huru aachwe.

Sasa polisi wanafika mitaani na kukusanya vijana wasio na kazi, na wale wanaowashuku kuuza au kuvu bangi kisha kuwaua kinyama. Misiba ni mingi mitaani, inatia huruma. Hili jambo ni kinyume na haki za binadamu.

Kijana anashikwa ndani ya masaa 12 anakuwa ameshakatishwa uhai. Upelelezi wa kutosha umefanyika? Hili zoezi nina hakika limepoteza vijana wasio na hatia. Hebu wapelekeni mahakamani mkawaue baada ya mahakama kuwatia hatiani.

Rais Samia utakuwa na mwisho mbaya. Police wamegeuza Kitonga Dar kuwa machinjio ya binadamu. Hata familia zenu zina vijana wa hovyo, wangekuwa wanaishi uswahilini tungewaita panya road. Serikali (mzazi na mlezi mkuu) inakwepa jukumu lake la kuwalea watoto wake na badala yake inwaua.

NB: Mimi si mhalifu, ni raia safi kabisa, sijapoteza ndugu yangu kwa hii operation na wala sina ndugu mhalifu, ila nimeumia tu na haya yanayotokea. Misiba ni mingi, huzuni na vilio. Huku viunga vya Kitonga ambako wamekugeuza machinjio ndiko ninakoishi. Jana nilienda uswahilini Tandika na Buza ni huzuni.
Kwanza mwandishi ulivyoandika kwa hisia na kujihamii inaanza kututia shaka....
1. UNATOA MALALAMIKO YA JUMLA
2. UNAJIHAMI KUWA WEWE SIYO MHALIFU NA HUNA NDUGU MHALIFU [NDUGU ZAKO WOOOOTE]
3. MALALAMIKO YAKO NI YA JUMLA NA HUJATOA HATA MFANO WA TUKIO AU MTU ALIYEUAWA BILA HATIA NA MAZINGIRA YA KUUAWA KWAKE....

KWANZA NAOMBA KUSEMA WAZI KUWA SIUNGI MKONO MAUAJI YA HOLELA YASIYOFUATA SHERIA...

LAKINI NINA HAYA YA KUSEMA KUHUSU BANDIKO LAKO HILI:-
1. Kutokana na uandishi wako ni either unataka huruma juu ya kile kinachoendelea na unahitaji kisimame mara moja ili upate nafuu.. Je wewe ni mnufaika kwa namna moja au nyingine juu ya hiki kilichokuwa kinafanywa na panya road?

2. Ni kipi kinawapa vijana jeuri ya kuendelea makundi hasa maeneo hatarishi na nyakati hatarishi kama hawa majukumu ya kufanya kwa nini wasikae majumbani ili kutoa nafasi kwa walinda USALAMA kufanya kazi zao?

3. Operation nyingi za polisi kwenye zoezi hili wanapata info kutoka kwa raia wanaochoshwa na vitendo vya hawa panya road ambao mara nyingi ndugu na jamaa huwakingia kifua wanapofanya uhalifu na kuumiza wengine...

USHAURI TUSHIKIANE NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUKOMESHA VITENDO HIVI...

KWA RAIA WALIOATHIRIKA NA VITENDO VYA PANYA ROAD WANAOA KUNA TIJA MAANA PANYA ROAD WAMEPOTEA MITAANI NA AMANI INAREJEA!!!!!
 
Unyama unyama wametaka wenyewe,ujawahi kuvamiwa na wezi??nakumbuka 2011 nilipo maliza form 4 nikazama mtaani huku nikisubiri matokeo ya advance,nikaanza kujishikisha kwenye vikazi vya saidia fundi nilikusanya pesa yangu safi tu,wezi walinivamia wakachukua pesa zangu zote,nguo zangu zote na. Kuku wangu niliyofuga walikuwa wanakata vichwa na kuwaweka kwenye viroba takribani kuku 50 waliondoka nao alafu ni majogoo wakubwa,niliwahesabu walikuwa wezi zaidi ya 15,wakanipiga sana sitaka nisahau siku ile,basi sasa nimekuwa sina huruma tena nikishajua wewe mwizi nanikajiridhisha kukupiga na vitofali siwazii
 
Unaambiwa mtume muhammed alikua hawachekei kima wa namna iyo ya panya road ilishawahi tokea kisa kuna wahuni waliingia madina wakajifanya wema na walikua wanaumwa ugonjwa flani dawa yake ilikua ni maziwa ya ngamia wale wahuni wakatibiwa vizuri kuna siku wameenda machungoni na mwenyeji wao wakamamuua wakaiba ngamia taarifa zilipomfikia mtume akatuma msako wahuni wakadakwa
Alichawafanya sasa

Walikatwa mguu mmoja mmoja kila muhuni akabaki na single leg wakatobolewa macho alafu wakaachwa juani wafe mdogo mdogo[emoji16] usichukulie poa jua la jangwani.. alafu akawaambia hii ndo hukumu ya jambazi

Kwaiyo mtoa mada acha huruma huruma maamuzi magumu yakiume yanatolewa muda mwingine kulinda watu wenye roho nyepesi kama zenu ndo maana leo huwezi sikia vigenge vya kiarifu kweny nchi kama saudi arabia waliweza kukomesha vitabia vya kishenzi kama vya panya road ukiona mtu kakamatwa na polisi ujue kuna tatizo pahala kaa kwakutulia dawa iingie
 
Unahitaji counceling, kwako wewe ni sawa kusema upanga Kwa upanga,jino Kwa jino,

Serikali IPO madarakani na inakusanya Kodi Ili kulinda raia sio kuua raia.

Sheria zifuatwe, POLISI watimize wajibu wao, mahakama ifanye KAZI yake, JAMII pia iwalee watoto ktk maadili Ili wasijekuwa wahalifu.

Ameeeen
Unatambua polisi mmoja anahitaji kuhudumia raia wangapi? Kodi unayolipa ili kila raia aweze kulindwa na polisi ni kiasi gani? Nabaki na msimamo wangu hawa ni wa kupunguza tu hizo sheria zinachelewesha maamuzi, hizo sheria ndo zimewaachia hao wanaorudi kuja kuua, hizo sheria ndo zimeachia kwa dhamana hao wanaorudi kuja kuua. Kwangu the only remain solution is by ELIMNINATION. Na tamani kuona hata OPORD na SMEAC hazitumiki bali polisi wajikite kwenye Elimination mpaka hapo baadae. Kuwachekea chekea ndo maana wajiona vidume.
 
umefanya utafit wap ? mbona mnafanya siasa hatarishi kwa taifa , jitahidin kuheshimu vitengo vya watu , wenzenu wapo mtaan kufanya research , ww upo jf kufanya research hlf research yako ndo unataka tuiamin , nakupa story fupi Mzee JPM anaingia madarakan , aliomba list ya wahuni wote wa mitaa ilipelekwa kwa wenyeviti na ikawa imepigwa tukio akashikwa mmoja bas akiwataja na ikaonekana upo kweny list bas umeisha , waliangushwa watu huko Vingunguti kukatulia kbs nikahamia Vingungut nlikuwa natembea saa 7 usiku sikabwi , ila alipofarik siku ya pili likapigwa tukio daktar mmoja alikuwa na laptop plus laki tatu ya mauzo ya duka lake la dawa alivamiwa alipgwa mapanga na kuibiwa laptop , simu na laki 3 zote , siku iliyofuatia wakapiga matukio 3 , vingungut ikawa haikalik , wakaenda mpk airport wakapiga tukio mbele ya airport na jeshi la anga lipo krb , tulikaa vikao watu wakasema wanawajua ila kuwataja ni hatari sabab wakienda polisi wanarudishwa na unakuwa hatarini uliewataja , nlihama vngungut baada ya kuona wanaogopa kuwakuchukulia hatua kali mpk kesho huko vingungut hao watoto huwa wanafunga mtaa muda wa mchana kweupe ( km Syria vile , ndo unavyotaka ? ) , nlihamia chamaz palikuwa shwar ila baada ya tukio la kawe napo pakawaka moto kila siku wanavamia mitaa ya huko chamaz , rpc alikuja wiki moja iliyopita wananchi walisema wanawajua hao panyaroad ila wakiwataja bas watoto wanapelekwa selo then wanarudishwa mtaani , jion ya siku hiyo ya kikao watoto wakapiga tukio krb na eneo hilo la kikao kilipofanyika uone walivyo na dharau , hao watoto wameiba na kuwafanya waty vilema hata kuwatia watu uchiz huko chamaz , nlipoona hali ni mbaya juz nmehama nmeona nihamie mbez beach huku nikiacha kodi ya miez 6 kisa hao watoto unawatetea , KAMA ULIZA NA SIO KUCHANGANYA SIASA NA USALAMA WA NCHI , WATU WANAANGAMIZWA VIBAYA KISA HAO WATOTO , HAMTANGAZIW TU ILA WANAYOFANYA HAO WATOTO NI BALAA WAKIULIWA SHUKURU NA SIO KULETA MIGAWANYIKO YA KISIASA , MM SIO WA NJANO ILA KWENY HILI WAULIWE TU HAO WAHUNI
Mwenzetu unaishi Jf siyo?

Haujawajua vizuri hao jamaa.
 
Watu wanakwapua mipesa ya umma na kujinunulia ma harrier , nako mtaani huwapa heshima kuwa ni ma fighter kumbe ni wauaji maana pesa zilizokwapuliwa zingeboresha huduma za afya na kupkoa uhai
Kikubwa elimu maana wanaua sekta ya elimu ambapo msomi anaweza hata kujiajiri.

Sasa hawa tunaowaona mitaani hata ukiwapa mitaji hawafiki nayobali.

Panya road ni zao la watawala
 
Kukaa makundi ni uhalifu? Unajua maisha ya uswazi? Hujui kukutana ni sehemu moja muhimu sana ya maisha ya ujana duniani kote? Tatizo lipo kwenye utawala ulioshindwa kila kitu unabaki kutumia mbinu za zima moto na matamko kuongoza. Si juzi juzi raia walikuwa wanahimizwa raia kuzaa kwa wingi? Walidhani wanaozaliwa wataishije?
mkuu mwambie kijana wako aachane na makundi
 
Habari!

Miaka 5 hivi imepita tulikuwa tukikemea mambo fulani mtandaoni. Kitendo cha serikali yenye zaidi ya vyombo sita vya usalama na haki kujichukulia sheria mkononi.

Serikali ifuate procedure katika kila zoezi, kama sheria itamtia mtu hatia na kuhukumiwa kuuawa auawe, kama itamfunga jela afungwe kama itamwacha huru aachwe.

Sasa polisi wanafika mitaani na kukusanya vijana wasio na kazi, na wale wanaowashuku kuuza au kuvu bangi kisha kuwaua kinyama. Misiba ni mingi mitaani, inatia huruma. Hili jambo ni kinyume na haki za binadamu.

Kijana anashikwa ndani ya masaa 12 anakuwa ameshakatishwa uhai. Upelelezi wa kutosha umefanyika? Hili zoezi nina hakika limepoteza vijana wasio na hatia. Hebu wapelekeni mahakamani mkawaue baada ya mahakama kuwatia hatiani.

Rais Samia utakuwa na mwisho mbaya. Police wamegeuza Kitonga Dar kuwa machinjio ya binadamu. Hata familia zenu zina vijana wa hovyo, wangekuwa wanaishi uswahilini tungewaita panya road. Serikali (mzazi na mlezi mkuu) inakwepa jukumu lake la kuwalea watoto wake na badala yake inwaua.

NB: Mimi si mhalifu, ni raia safi kabisa, sijapoteza ndugu yangu kwa hii operation na wala sina ndugu mhalifu, ila nimeumia tu na haya yanayotokea. Misiba ni mingi, huzuni na vilio. Huku viunga vya Kitonga ambako wamekugeuza machinjio ndiko ninakoishi. Jana nilienda uswahilini Tandika na Buza ni huzuni.
Polisi sio wapumbavu kama unavyodhani.
Wao wanajua pia kuna watu hawana hatia.Wanajua kazi yao kuliko unavyotaka kuwafundisha.
Najua watu mnaowatengeneza hawa watoto kuwa magaidi mmepaniki sana.
Ila usidhani viongozi ni makatili na wewe ndio mwenye roho nzuri.
Kwanza inabidi mtuambie mna lengo gani kuwafundisha watoto ugaidi?
 
Tunarudi pale pale, je mahakama zifungwe Ili mamlaka ya kuua yakaimishwe Kwa POLISI?

Au tuwawezeshe POLISI mafunzo na vitendea KAZI kuhakikisha POLISI wetu hawadhuriki na wahalifu??
Kuna kesi za kubaka, Wizi, Utapeli zitaendelea mahakamani Ila Kwa hili la panya road tunaomba tuwapunguzie mahakama KAZI ni mwendo WA Shaba!

Jichanganye na wewe tukulie timing

Sent from my SM-A032F using JamiiForums mobile app
 
mkuu mwambie kijana wako aachane na makundi
Sina kijana yoyote ila kama mwananchi mpenda haki inabidi nitetea vijana wote wa Dar. Shida yako naona unadhani kuwa (kama walivyo watanzania wengi) tatizo mpaka likupate wewe au mtu wako wa karibu ndiyo inabidi upige kelele. Ndiyo maana umeshafikia conclusion kuwa nina ''kijana wangu'' amekuwa victim. Mimi naumia sana kuona binadamu wenzangu wanateseka na kuuawa kwa bila kufuata sheria. Pengine wewe unadhani uko mbali sana na huu mfumo mbovu wa utawala, lakini nakuhakikishia hauko mbali. Kuna siku utakumbuka maneno yangu kwa sababu siyo lazima uathiriwe na hii ua ua au kamata kamata ya panya road tu, kuna mengi mengine unaweza kuja kuwa victim au mtu wako wa karibu.
 
umefanya utafit wap ? mbona mnafanya siasa hatarishi kwa taifa , jitahidin kuheshimu vitengo vya watu , wenzenu wapo mtaan kufanya research , ww upo jf kufanya research hlf research yako ndo unataka tuiamin , nakupa story fupi Mzee JPM anaingia madarakan , aliomba list ya wahuni wote wa mitaa ilipelekwa kwa wenyeviti na ikawa imepigwa tukio akashikwa mmoja bas akiwataja na ikaonekana upo kweny list bas umeisha , waliangushwa watu huko Vingunguti kukatulia kbs nikahamia Vingungut nlikuwa natembea saa 7 usiku sikabwi , ila alipofarik siku ya pili likapigwa tukio daktar mmoja alikuwa na laptop plus laki tatu ya mauzo ya duka lake la dawa alivamiwa alipgwa mapanga na kuibiwa laptop , simu na laki 3 zote , siku iliyofuatia wakapiga matukio 3 , vingungut ikawa haikalik , wakaenda mpk airport wakapiga tukio mbele ya airport na jeshi la anga lipo krb , tulikaa vikao watu wakasema wanawajua ila kuwataja ni hatari sabab wakienda polisi wanarudishwa na unakuwa hatarini uliewataja , nlihama vngungut baada ya kuona wanaogopa kuwakuchukulia hatua kali mpk kesho huko vingungut hao watoto huwa wanafunga mtaa muda wa mchana kweupe ( km Syria vile , ndo unavyotaka ? ) , nlihamia chamaz palikuwa shwar ila baada ya tukio la kawe napo pakawaka moto kila siku wanavamia mitaa ya huko chamaz , rpc alikuja wiki moja iliyopita wananchi walisema wanawajua hao panyaroad ila wakiwataja bas watoto wanapelekwa selo then wanarudishwa mtaani , jion ya siku hiyo ya kikao watoto wakapiga tukio krb na eneo hilo la kikao kilipofanyika uone walivyo na dharau , hao watoto wameiba na kuwafanya waty vilema hata kuwatia watu uchiz huko chamaz , nlipoona hali ni mbaya juz nmehama nmeona nihamie mbez beach huku nikiacha kodi ya miez 6 kisa hao watoto unawatetea , KAMA ULIZA NA SIO KUCHANGANYA SIASA NA USALAMA WA NCHI , WATU WANAANGAMIZWA VIBAYA KISA HAO WATOTO , HAMTANGAZIW TU ILA WANAYOFANYA HAO WATOTO NI BALAA WAKIULIWA SHUKURU NA SIO KULETA MIGAWANYIKO YA KISIASA , MM SIO WA NJANO ILA KWENY HILI WAULIWE TU HAO WAHUNI
Kwa hii stori ni kwamba panya road wanafahamika ila raia wema wanaogopa kuwataja kwa kuhofia usalama wao kwa hao hao panya road.
Kama ndio hivyo hao raia wema wafunguliwe mashtaka kwa kuwa wanashirikiana na wahalifu kwa kukataa kutoa ushirikiano kwa vyombo vya usalama.
Ikifanyika hivi ushirikiano watatoa na wahalifu halisi watapatikana na adhabu stahiki wapate badala ya kuzoa zoa na kusomba watu ambao wengine pengine wala hawahusiki.

Polisi wanashindwa kujiongeza tu. Wakiamua kuwawekea mtego hao panya road ni rahisi tu. Sidhani kama hawayajui maeneo yao ya kujidai.
 
Unyama unyama wametaka wenyewe,ujawahi kuvamiwa na wezi??nakumbuka 2011 nilipo maliza form 4 nikazama mtaani huku nikisubiri matokeo ya advance,nikaanza kujishikisha kwenye vikazi vya saidia fundi nilikusanya pesa yangu safi tu,wezi walinivamia wakachukua pesa zangu zote,nguo zangu zote na. Kuku wangu niliyofuga walikuwa wanakata vichwa na kuwaweka kwenye viroba takribani kuku 50 waliondoka nao alafu ni majogoo wakubwa,niliwahesabu walikuwa wezi zaidi ya 15,wakanipiga sana sitaka nisahau siku ile,basi sasa nimekuwa sina huruma tena nikishajua wewe mwizi nanikajiridhisha kukupiga na vitofali siwazii
Pole sana wezi wanaudhi sana na wanarudisha maendeleo ya watu nyuma. Yaani ukiibiwa unajisikia kuchanganyikiwa unakitafuta kitu kwenye mfuko wa shati au suruali wakati kitu chenyewe ni kikubwa kwa akili za kawaida hakiwezi kuingia.

Hao ni wezi bado mziki wa majambazi na magaidi, siyo poa kabisa. Polisi fanyeni kazi yenu hamuonei mtu ,apandaye bangi atavuna bangi.
 
Back
Top Bottom