Unyama huu wanaoufanya Polisi utamgharimu Rais Samia

Unyama huu wanaoufanya Polisi utamgharimu Rais Samia

Yaa i watu wanatetea uvunjwaji wa sheria kisa tu yanayowakuta ni watoto wa maskini! Hivi tukisema mtu akifanya kosa auawe bila kufuata sheria wangapi watauawa. Mfano hao watoto wa ushuani wakichukua gari za baba zao na kwenda nazo kwenye sherehe za birthday za ulevi kisha kutokana na kuendesha gari wakiwa wamelewa wakisababisha ajali nao wauawe papo hapo au wazazi wao watakuwa wa kwanza kutaka sheria ifuatwe? Au watoto wao humo ndani wakibaka housegirl mbona wanajitahidi kuyamaliza kimya kimya? Je nao wauawe bila kuhukumiwa mahakamani?

Ni vyema tutatue matatizo ya jinai mbalimbali kwa kufuata sheria.
Mtoto wa masikini anaruhusiwa kuwa panya?
 
Tunarudi pale pale, je mahakama zifungwe Ili mamlaka ya kuua yakaimishwe Kwa POLISI?

Au tuwawezeshe POLISI mafunzo na vitendea KAZI kuhakikisha POLISI wetu hawadhuriki na wahalifu??
tunawaona mnavyotetea panya road , hv mahakama kaz yake ni kuendesha kesi za panya road tu ? je unajuwa kuwa polis akikuambia simama hutakiw hata kutikisika ? sasa unamlaumije polis kwa makosa ya mharifu , kama hujui uliza au kama ww ni panya road bas tafuten kaz halali , tunajuwa mnalipwa ili kuja kupotosha umma mpate namna mpy ya kurudi kuchafua aman yetu
 
Nina wasiwasi hata hapa JF kuna panya road kama sivyo bas kuna wale wajuaji kila Jambo wanajifanya wanathink beyond. Hakuna dawa nyingine nzuri kama kuwaua hawa vibaka. Tena hii operation ingefanyika nchi nzima. Mtoto akishaharibika kaharibika akifungwa mwaka akitoka ndio anakua hatar Zaid. Dawa ndo hii mpka nchi inyooke
 
Unahitaji counceling, kwako wewe ni sawa kusema upanga Kwa upanga,jino Kwa jino,

Serikali IPO madarakani na inakusanya Kodi Ili kulinda raia sio kuua raia.

Sheria zifuatwe, POLISI watimize wajibu wao, mahakama ifanye KAZI yake, JAMII pia iwalee watoto ktk maadili Ili wasijekuwa wahalifu.

Ameeeen
dah tuna kaz ya ziada , hv mtu aliyefungwa mara mbili na bado unaamin jela itakuwa suluhu , hv unahis kodi ya watanzania zipo kwa ajili ya watu waliokata kujirekebisha , hata ulaya unapoambiwa simama ukitikisika unalambwa shaba , sasa usipotaka panya road wafe bas acha kuchoma moto wezi na pia washauri panya road waache kuua watu , kama polis ingekuwa inauwa watu wa mchongo bas tungesikia wanaendelea kupiga matukio , wanajijua na wanajuwa kuwa wanajulikana na ndio maana wametulia tuliii
 
Nasisitiza POLISI wapewe facilities wawakamate wahalifu na kuwafikisha mahakamani Ili wahukumiwe huko.

Katiba ya nchi hairuhusu Police kama wasimamizi wa Sheria kufanya KAZI ya mahakama kuhukumu watu vifo Kwa utashi wao.

Umeelewa????
katiba ya nchi inaruhusu panya road kupora na kuiba na kuua watu ? sio ? kuna namna una nufaika na uharifu wa PANYA ROAD
 
Good
Haya mawazo ya watu kuunga mkono mauaji ya short cut ni dalili kuwa Watanzania wengi wana matatizo ya akili
wewe ni mnufaika wa panya road kama sio mfadhir au mweneza propaganda , unaongelea upande wa polisi , ila hatuon ukikemea panya road , Huez tegemea mahakama na jela kusaidia kwa wahuni walioizoea jela , wanafungwa na kurud mtaani na kuendelea mauaji , hajauliwa ndugu yako ndio maana haikuumi , mm nmeona matukio matatu ya hao wahuni ndan ya wiki mbili hz , nashangaa kuona mtu unatetea uhai wa hao wahuni
 
Ndio hao wanaokata VICHWA wake zao Kwa kupishana tu kauli ndani ya nyumba.
kuna namna mnanufaika na huu uhalifu au huenda mna kauitindio wa ubongo , hao panya road wanajulikana tangu zaman kama hujui uwe unauliza sisi tumeish mitaani tunaelewa situation nzima na vijiwe hao panya road hawaendag kabisa mf pale vingunguti mwisho wa lami kuna kijiwe kinaitwa fellow hawapiti pale wanaeza tokea airport bas wakaja wakapitia hata bonden wakatokea sahara wakaendeleana uporaji sabab wanajuana na wanajua wakiharibu wanafuatwa kweny vijiwe vyao , polis wanwajuwa waharifu na wanapewa tu miongoz na ndio maana hakuna hata mmoja kauliwa hakuwa muharifu
 
Watu wana msongo wa mawazo na hawamjui adui yao halisi
duh siasa zinakufanya chiz , polis wafanye kazi yao , bila hata kumjua nan anawatuma lazima tuwatie uoga hata wale walioanza kuona uhuni ndo mchongo wa kutoboa kirahisi
 
Ndugu kinachoendelea ni dhahama
Sasa Sungusungu na police jamii chini ya wajumbe wakipeleka jina lako polisi kata kuwa mwenendo wako si mzuri utakuja kuchomolewa nyumbani kwako muda wowote na ndugu zako wataikuta maiti Muhimbili.
Is this fair?
Mungu hawezi kuibariki nchi ya kishetani namna hii
Kwanini uwe na mwenendo usiofaa?
 
We mgeni Nchi hii, hukusikia mbeya POLISI walimkamata mfanya biashara wa madini walipomkuta na mil 30 wakakubaliana kumuua Ili kufuta ushahidi?

POLISI haruhusiwi kuua kisheria, nendeni shule msitege!!!
ulikuepo kwenye tukio au ulihadithiwa , waswahili hatuaminiki kokote kule sabab tunajua kupika data , hata mm ndugu yangu cheti feki alitimuliwa ila ntakuambia alikuwa na ugomv na ccm iwe kama defensive mechanism mbali na hiyo kesi ilipelekwa wilayan kuwa shule x ilikuwa inatoa majibu kwa wanafunz basi afisa elimu aliandaa mitihni ghafla na cha kushangaza aliepeleka malalamiko watoto wake walidrop kwa 50% na wale waliolalamikiwa walimaintain performance , usimuamin mswahili kwa story za mdomon
 
Najiuliza kitu...kama panya road wanatembea makundi makundi inamaana wanajuana sasa inashindikana vipi kuwakamata mpaka wanauawa?
walishakamatwa na kwenda jela wamerudi ila ndo wamejiupgrade aya jiulize ukiwapeleka tena wakirud si ndo watashika bunduki kbs , lzm tuondoe hiz taka taka kama mnavyochoma moto wezi
 
Hapana mkuu...kumuua mtu bila uthibitisho sio fair...Pia kumbuka kuna watoto wadogo wasiojitambua wanatumiwa.
mbona tushaandika sana ,WANAJULIKANA TANGU ZAMAN TTZO LENU WASWAHILI VICHWA VIBOVU KUELEWA , WALIKUWA WANAFANYA MATUKIO SANA ILA LILILOWASTUA WENGI NI TUKIO LA KAWE ILA WALIKUEPO SANA TU , SO WANAJULIKANA VZR TU SIO KWAMBA POLISI INAOTEA HAPANA
 
Ndugu kinachoendelea ni dhahama
Sasa Sungusungu na police jamii chini ya wajumbe wakipeleka jina lako polisi kata kuwa mwenendo wako si mzuri utakuja kuchomolewa nyumbani kwako muda wowote na ndugu zako wataikuta maiti Muhimbili.
Is this fair?
Mungu hawezi kuibariki nchi ya kishetani namna hii
acha uongo wewe , kwann mwenyekiti na sungu sungu wapeleke jina lako polis kama mienendo yako mizur
 
Hata kukiwa na uthibisho hakuna Sheria inayosema akibainika apigwe risasi hapohapo, tunafika huku kwa sababu ya malezi mabovu, haya matukio hapa dar hayajaanza Leo na zipo familia zinabariki matukio haya kwa kula na watoto wao, zipo familia hata baada kuambiwa mwanao anajishughulisha na haya mambo hata hawaangaiki, Kuna vikundi mtaani mpaka vimejipa utawala na vinaogopeka mtaani na ni vitoto vidogo tu . Watoto shule hawafiki kutwa wanashinda machimbo, kwenye vijiwe na mzazi hajishughulishi kumfatilia mtoto sasa nani unategemea akusaidie kulea
yaan watu wanachoma moto wezi ambao sio hatar kwa usalama ila watu wanawatetea panya road ambao ni hatar kwa usalama wa raia , Kwann nisiwahisi kuwa hawa ni panya road pia ?
 
Habari!

Miaka 5 hivi imepita tulikuwa tukikemea mambo fulani mtandaoni. Kitendo cha serikali yenye zaidi ya vyombo sita vya usalama na haki kujichukulia sheria mkononi.

Serikali ifuate procedure katika kila zoezi, kama sheria itamtia mtu hatia na kuhukumiwa kuuawa auawe, kama itamfunga jela afungwe kama itamwacha huru aachwe.

Sasa polisi wanafika mitaani na kukusanya vijana wasio na kazi, na wale wanaowashuku kuuza au kuvu bangi kisha kuwaua kinyama. Misiba ni mingi mitaani, inatia huruma. Hili jambo ni kinyume na haki za binadamu.

Kijana anashikwa ndani ya masaa 12 anakuwa ameshakatishwa uhai. Upelelezi wa kutosha umefanyika? Hili zoezi nina hakika limepoteza vijana wasio na hatia. Hebu wapelekeni mahakamani mkawaue baada ya mahakama kuwatia hatiani.

Rais Samia utakuwa na mwisho mbaya. Police wamegeuza Kitonga Dar kuwa machinjio ya binadamu. Hata familia zenu zina vijana wa hovyo, wangekuwa wanaishi uswahilini tungewaita panya road. Serikali (mzazi na mlezi mkuu) inakwepa jukumu lake la kuwalea watoto wake na badala yake inwaua.

NB: Mimi si mhalifu, ni raia safi kabisa, sijapoteza ndugu yangu kwa hii operation na wala sina ndugu mhalifu, ila nimeumia tu na haya yanayotokea. Misiba ni mingi, huzuni na vilio. Huku viunga vya Kitonga ambako wamekugeuza machinjio ndiko ninakoishi. Jana nilienda uswahilini Tandika na Buza ni huzuni.
Nilivyokuelea ni umeandika mawazo yako bila ushahidi hata wa tukio moja.

Fafanua kidogo zaidi, ulitaka iweje? Kijana aliouliwa/ waliouliwa hawana majina? Hawana umri? Au nawe ni mmoja wa hayo makundi ya wahalifu?

Hao vibaka na Panyarodi hawana sabbu ya kufikishwa mahakamani, wauliwe na watafutwe wale wanaonunua mali walizoina nao wauliwe, au wewe ni mmoja wao mnaowalea hao wahalifu?
 
Kwanza mwandishi ulivyoandika kwa hisia na kujihamii inaanza kututia shaka....
1. UNATOA MALALAMIKO YA JUMLA
2. UNAJIHAMI KUWA WEWE SIYO MHALIFU NA HUNA NDUGU MHALIFU [NDUGU ZAKO WOOOOTE]
3. MALALAMIKO YAKO NI YA JUMLA NA HUJATOA HATA MFANO WA TUKIO AU MTU ALIYEUAWA BILA HATIA NA MAZINGIRA YA KUUAWA KWAKE....

KWANZA NAOMBA KUSEMA WAZI KUWA SIUNGI MKONO MAUAJI YA HOLELA YASIYOFUATA SHERIA...

LAKINI NINA HAYA YA KUSEMA KUHUSU BANDIKO LAKO HILI:-
1. Kutokana na uandishi wako ni either unataka huruma juu ya kile kinachoendelea na unahitaji kisimame mara moja ili upate nafuu.. Je wewe ni mnufaika kwa namna moja au nyingine juu ya hiki kilichokuwa kinafanywa na panya road?

2. Ni kipi kinawapa vijana jeuri ya kuendelea makundi hasa maeneo hatarishi na nyakati hatarishi kama hawa majukumu ya kufanya kwa nini wasikae majumbani ili kutoa nafasi kwa walinda USALAMA kufanya kazi zao?

3. Operation nyingi za polisi kwenye zoezi hili wanapata info kutoka kwa raia wanaochoshwa na vitendo vya hawa panya road ambao mara nyingi ndugu na jamaa huwakingia kifua wanapofanya uhalifu na kuumiza wengine...



USHAURI TUSHIKIANE NA VYOMBO VYA ULINZI NA USALAMA KUKOMESHA VITENDO HIVI...

KWA RAIA WALIOATHIRIKA NA VITENDO VYA PANYA ROAD WANAOA KUNA TIJA MAANA PANYA ROAD WAMEPOTEA MITAANI NA AMANI INAREJEA!!!!!
ameniii
 
Unyama unyama wametaka wenyewe,ujawahi kuvamiwa na wezi??nakumbuka 2011 nilipo maliza form 4 nikazama mtaani huku nikisubiri matokeo ya advance,nikaanza kujishikisha kwenye vikazi vya saidia fundi nilikusanya pesa yangu safi tu,wezi walinivamia wakachukua pesa zangu zote,nguo zangu zote na. Kuku wangu niliyofuga walikuwa wanakata vichwa na kuwaweka kwenye viroba takribani kuku 50 waliondoka nao alafu ni majogoo wakubwa,niliwahesabu walikuwa wezi zaidi ya 15,wakanipiga sana sitaka nisahau siku ile,basi sasa nimekuwa sina huruma tena nikishajua wewe mwizi nanikajiridhisha kukupiga na vitofali siwazii
sasa hv hao hao panya road wanakuvamia na kukupiga mapanga haijalish umewapa ela au hujawapa
 
Ndugu kinachoendelea ni dhahama
Sasa Sungusungu na police jamii chini ya wajumbe wakipeleka jina lako polisi kata kuwa mwenendo wako si mzuri utakuja kuchomolewa nyumbani kwako muda wowote na ndugu zako wataikuta maiti Muhimbili.
Is this fair?
Mungu hawezi kuibariki nchi ya kishetani namna hii
Tupe japo jina la mmoja wa aliyefanyiwa hivyo na utuoneshe kuwa hakuwa mhalifu.

Jiji lote limetaharuki limetekwa na wahuni wachache wanaojiita panyarodi, wauliwe tu.
 
Back
Top Bottom