Unyama huu wanaoufanya Polisi utamgharimu Rais Samia

Hili zoezi nina hakika limepoteza vijana wasio na hatia
Hao vijana wamepoteza maisha ya watu wasio na hatia zaidi ya sana. Wanawavamia watu majumbani mwao wakiwa wamelala, hawajaiba cha mtu halafu wao wanaenda kuwaibia na kuwatoa uhai.

Watu wa aina hii ndiyo unaleta ngonjera zq kijinga ahapa kuwatetea? Au kwakuwa hawajaua ndugu yako hata mmoja?

Nashauri polisi na serikali kwa ujumla, mtu yeyote mwenye walakini ktk mwenendo wake akamatwe na kuuawa. Nchi yetu Tanzania ani nchi ya amani. Hawa Panya-road wauawe wote.
 
Kijana anashikwa ndani ya masaa 12 anakuwa ameshakatishwa uhai. Upelelezi wa kutosha umefanyika? Hili zoezi nina hakika limepoteza vijana wasio na hatia. Hebu wapelekeni mahakamani mkawaue baada ya mahakama kuwatia hatiani.
Ninyi si ndiyo mlikuwa mnalalamika Panya road mkawa mnasema mtajichukulia Sheria Mkononi kuwakomeshA? Imekuwaje Tena mnaposaidiwa kazi mnalalamika? Au upo upande huo? Sifurahii kuonewa mtu lakini kama ulivyosema vyombo vyote sita nadhani haviwezi kukosea kumtambua kijana mwalifu vinginevyo iwe ni hujuma!
 
Wote wanaoshinda kwenye vibanda vya kubeti wenye milegezo na wapiga debe wote wapigwe risasi.

Hongereni sana polisi kwa maamuzi haya mazuri
 
Kuna mtoto mmoja wa kiongozi mkubwa namaanisha mzazi wake yuko kwenye utatu Mtakatifu.
Ni mtukutu sana na lisumbufu, angekuwa Uswahilini naye angepigwa risasi kwa tabia zile.
Je, huyo mtoto ni panya road na anahusika na uporaji? Ukweli ni kuwa polisi hawaruhusiwa kuuwa, lakini je panya road wanaruhusiwa kukata watu mapanga, kupora, na kuua? Hawa panya road na majambawazi wakiachiwa amani haitakuwepo mtaani. Najua ni jambo kubwa kwa mzazi kuuliwa mtoto wake, lakini inafika mahali inabidi tuukabili ukweli. Ita kuuwawa "panya road" na majambawazi mengine ajali kazini. Kama hawataki polisi wawakamate waachane na ujambazi utaona kama [olisi atawafuata na kuwaua.
 
HILI LA KUUA PANYA ROaD SIO SAHIHI.. kila mtu asikilizwe na ahukumiwe na sheria mahakamani. Mtu akifa unaweza kumpa hatia yeyote hata kama aliuliwa kwa makosa...
Ile tume ya kuangalia Jeshi letu ifanye kazi kwa haraka..
Hayajakukuta ya Panya road ndio maana unaandika hivi. siku yakikukuta ndo utajua umhim wa Polisi kusaga kunguni.
 
Ila ww akili zako za kitoto sana........Kama unajua kuna msako kwa Nini ukakae vijiweni na ujingani.

Siku wakuvamie wakubake wakuibie tuone kama utakuja hapa kusema hayo unayosema
 
Kwa sasa ukiona mtu anamtetea panya road basi ujue ni eidha na yeye ni mmoja wa hao panya road, au ana ndugu yake, mtoto wake, rafiki yake ambae ni panya road.
Mtu wa kawaida kabisa unaefahamu unyama unaofanywa na hawa mbwa hauwezi kamwe kuja kuwatetea humu mitandaoni kama wanavyofanya baadhi ya hawa wahusika wenzao.

Natamani polisi iwe inapita humu JF kuwafuatilia na kuwachunguza vizuri hawa wanaowatetea hao vijana makatili.
 
HILI LA KUUA PANYA ROaD SIO SAHIHI.. kila mtu asikilizwe na ahukumiwe na sheria mahakamani. Mtu akifa unaweza kumpa hatia yeyote hata kama aliuliwa kwa makosa...
Ile tume ya kuangalia Jeshi letu ifanye kazi kwa haraka..
Yaa i watu wanatetea uvunjwaji wa sheria kisa tu yanayowakuta ni watoto wa maskini! Hivi tukisema mtu akifanya kosa auawe bila kufuata sheria wangapi watauawa. Mfano hao watoto wa ushuani wakichukua gari za baba zao na kwenda nazo kwenye sherehe za birthday za ulevi kisha kutokana na kuendesha gari wakiwa wamelewa wakisababisha ajali nao wauawe papo hapo au wazazi wao watakuwa wa kwanza kutaka sheria ifuatwe? Au watoto wao humo ndani wakibaka housegirl mbona wanajitahidi kuyamaliza kimya kimya? Je nao wauawe bila kuhukumiwa mahakamani?

Ni vyema tutatue matatizo ya jinai mbalimbali kwa kufuata sheria.
 
Kwahiyo kijana akikimbia tu,apigwe risasi??
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…