Uuaji ni uuaji!
Panyarodi aliyeua mtu, na mtu aliyemuua panyarodi wote, ni wauaji!
Kwa wasio na dini, uuaji wa kulipa kisasi Kama hivyo ni halali!
Kwa wenye dini wote, wakumbuke dini zao zinafundisha juu ya haki zilizoamriwa na Mwenyezi Mungu!
Wakumbuke mamlaka za ulimwengu zilizosimamishwa na Mwenyezi Mungu!
Mamlaka hizi zipo kusimamia haki na kutoa hukumu!
"Eti tusikulaumu kuua kwa sababu wewe ndio ulioibiwa! Chefuuu!
Kwani sheria zilizowekwa za kutoa hukumu hazijui kuwa wewe na wenzako munaibiwa?
"Eti ukipeleka polisi mwizi anarudi mtaani,"
Watu wazima hovyoo
Atarudi kwa sababu hamuendi kutoa ushahidi,. Mbona kumuua munashirikiana watu zaidi ya ishirini, kwanini ushirikiano huo musiupeleke polisi Kisha mahakamani? Watu ishirini wote mutashindwaje kumtia mtu hatiani?
"Eti serikali yenyewe haiwajibiki na hivyo acha wahalifu wauawe!" Khaaah
Mbona kila kukicha munashangilia viongozi wa Serikali?
Mbona hamuwapindui kwa kura zenu au hata maandamano?
Na ajabu haohao wanaoshadadia wauwaji wa wahalifu wakiamini vyombo vya dola haviwajibiki, Ni UVCCM wakubwa!
Kukicha Ni kumwaga sifa kwa serikali yao!
Lazima tukubali jamii imetawaliwa na roho za kikatili! Mwizi katili na walioibiwa Ni katili pia!
Haiwezekani roho njema ishangilie mateso na kifo Cha mtu aliyeiba television nyumbani kwako!
Nooooo! Lazima kwanza uwe na roho mbayaaa!
Lazima jamii hii ibadilike iwe ya kistaarabu yenye kuwajibika chini ya sheria zetu wenyewe
Cha kushangaza jamii inalalamika pale kiongozi anapoongoza kikatili bila kujali sheria, na tunasahau huyo ni kiongozi kutoka jamii yetu ambayo haioni thamani ya kuishi kwa kufuata sheria!
Kuna tofauti gani kiongozi kuagiza raia anayokwamisha serikali auawe, na raia kumuua mwizi aliyokwapua pochi ya sista du kule mburahati?
Sent from my Infinix X657 using
JamiiForums mobile app