Unywaji wa pombe aina ya Banana inaathiri nguvu kubwa sana ya vijana

Kumbe hizi pombe bado zipo, huku Dar sizioni kabisa
 
Kuna moja inaitwa barabara ya vumbi ni hatari na nusu chupa 300.
 
Me huwa nahisi hii Banana hizo alc percentage zilizoandikwa hapo kwenye chupa sio sahihi huenda zimezidi na TBS labda walihakiki za kwanza kwanza nyingine zinapigwa tu lebo [emoji3][emoji3] maana watu wanaopiga hii mambo ni kama kunywa gongo [emoji3] au kitoko na Double kick wamechoka sana !
 
Acha wanywe mkuu.

Acha wanywe wanaume tubakie wachache tufaidi hawa watoto wazuri.

Mimi nina wanawake kadhaa wake za watu ambao wanaume zao wanaendekeza pombe, nawasaidia kuwazalishia wake zao na wananisaidia kunilelea DNA yangu.

Acha wanywe.
 
Inasikitisha ila walevi wengi huwa hawali misosi,wakishaanza kunywa wao ni kata mti panda mti hakuna anayekumbuka kula.

Hivi Vipombe vidogo vodogo ni hatari ,kuna Double Kick na Burudani vinapendwa sana sababu ya bei rahisi.

Bila kula mwili hauwezi kupata nguvu.
 
Balaaa linakuja kizazi kijacho. Sahivi kila mtu anaangalia namna ya kujipatia pesa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…