Unywaji wa vinywaji hivi nini matokeo yake miaka 10 ijayo?

Unywaji wa vinywaji hivi nini matokeo yake miaka 10 ijayo?

Bushmamy

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2019
Posts
9,140
Reaction score
15,963
Miji mingi yenye hali ya hewa ya joto wengi tumeshuhudia. Matumizi makubwa ya soda na vinywaji vya energy. Baadhi ya watu hutumia soda hadi tatu kwa siku pamoja na vinywaji vya energy, na wengi wao wanakuambia hawawezi maliza siku bila kunywa soda/energy

Wengi wa wanaofanya kazi juani muda mrefu mfano mzuri Ni mafundi ujenzi. Vijana wa boda boda, wamachinga Nk. Ndio watumiaji wakubwa wa aina hii ya vinywaji tajwa hapo juu kila siku na Kwa. Maelezo yao ni. Kuwa. Vinywaji hivo hukata kabisa kiu haraka.

Unywaji wa aina hii hauna madhara yoyote kwa badae?

=====

Pia soma: Vinywaji vya kuongeza nguvu (energy drinks) vinamaliza nguvu kazi za Taifa
 
Hao madokta wenu wa kisabato watawaua kwa hofu

Binadamu wa zamani walishindia matunda na nyama mbichi lakini wako wapi? wamekufa wote

We achana na sisi kufa kupo tu
As long as tunaenjoy
Tusitishane.

Niko napata coka,supu ya makongoro na chapati nne hapa . Alaaah
 
9934bd04-3f2b-4b44-bf03-4dfa1f0862a1.jpg
 
Hao madokta wenu wa kisabato watawaua kwa hofu

Binadamu wa zamani walishindia matunda na nyama mbichi lakini wako wapi? wamekufa wote....
Hoja yako haifichi ukweli kwamba unywaji wa soda,na sukari ni hatari kwa afya yako.

Haijalishi tutakufa,walikufa na watakufa,Ila sukari bila kujalisha ya energy au soda au ya kawaida ni mbaya na haifai kwa matumizi ya binadamu.

Mnatengeneza vitambi,vidonda kuchelewa kupona,mchubuko mdogo tu kidonda hiko!! Mashine kuwa ndogo na kusinyaa(kwa wanaume) na matatizo mengine mengi tu.

Soda na energy siyo chakula. Usifananishe na matunda na nyama mbichi walizokula wazee wetu huko Zama za mawe.
 
Miaka 10 ijayo madaktari watakuwa bize sana. Nna kiduka mtaani kwetu nauza na vileo, kuna mteja mmoja kwa siku anaweza kunywa Ambiance 5 kwa siku na kila akinunua Ambiance ananunua na Energy. Just imagine nini hatima yake? Kwa wasioijua Ambiance ni sawa na Kitoko/Double Kiki huko Daslam
 
Acha kuujaza mwili vitu visivyo na umuhimj wa kula mkuu.

Unautesa mwili bila sababu. Generator yake mafuta ili i-operate kwa ufanisi,kwa nini uchanganye na maji?

Food industry imevamiwa na products nyingi Sana za kutumaliza kimyakimya.
Hakuna tunachokula kilicho salama kwa sasa mkuu, hizo mbogamboga tu zina chemicals za kutosha. Ukisema tuache kula na kunywa chemicals labda wote turudi shamba tukalime wenyewe kwa mbolea ya mboji/samadi.
 
Hiyo ya unga ndio vumbi la congo ila kijana una balaa [emoji23] ukishamkamata mshangazi hapo kwisha habari yake

[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji2089][emoji17]
 
Hoja yako haifichi ukweli kwamba unywaji wa soda,na sukari ni hatari kwa afya yako.

Haijalishi tutakufa,walikufa na watakufa,Ila sukari bila kujalisha ya energy au soda au ya kawaida ni mbaya na haifai kwa matumizi ya binadamu.

Mnatengeneza vitambi,vidonda kuchelewa kupona,mchubuko mdogo tu kidonda hiko!! Mashine kuwa ndogo na kusinyaa(kwa wanaume) na matatizo mengine mengi tu.

Soda na energy siyo chakula. Usifananishe na matunda na nyama mbichi walizokula wazee wetu huko Zama za mawe.
Taja sababu kuu ya kisukari nione kama kweli unajua unacho andika
 
Miaka 10 ijayo madaktari watakuwa bize sana. Nna kiduka mtaani kwetu nauza na vileo, kuna mteja mmoja kwa siku anaweza kunywa Ambiance 5 kwa siku na kila akinunua Ambiance ananunua na Energy. Just imagine nini hatima yake? Kwa wasioijua Ambiance ni sawa na Kitoko/Double Kiki huko Daslam
Atakufa zake Wala hatosumbua madakitari kuwa na amani
 
Mwaka jana nilienda home kusalimia nikakuta bi mkubwa anajenga banda la nguruwe basi nikasimamia kidogo mafundi wakawa wamemaliza katika kusafisha mazingira niliokota kopo za energy drink za azam na mo extra zaidi ya 70 na hizo ni zile wanazokunywa wakifika kazini kulikua na mafundi wanne tu kwenye kazi kile kitu kilinishangaza na muda wa kazi ilikua kama wiki mbili na kidogo nikaja kumuuliza fundi mkuu vipi mbona energy nyingi? Akanijibu asee siwezi anza kazi bila chupa moja mchana akila anakunywa au apige soda alafu jioni akifunga kazi lazima apitie dukani anunue moja kwa siku anasukuma 2 mpka 3 asee ni hatari
 
Miaka 10 ijayo madaktari watakuwa bize sana. Nna kiduka mtaani kwetu nauza na vileo, kuna mteja mmoja kwa siku anaweza kunywa Ambiance 5 kwa siku na kila akinunua Ambiance ananunua na Energy. Just imagine nini hatima yake? Kwa wasioijua Ambiance ni sawa na Kitoko/Double Kiki huko Daslam
Usiwe unampa nyingi sasa kwa kujali afya yake 😀
 
Hao madokta wenu wa kisabato watawaua kwa hofu

Binadamu wa zamani walishindia matunda na nyama mbichi lakini wako wapi? wamekufa wote

We achana na sisi kufa kupo tu
As long as tunaenjoy
Tusitishane.

Niko napata coka,supu ya makongoro na chapati nne hapa . Alaaah
Au sio
😆 😆 😆
 
Back
Top Bottom