Mwaka jana nilienda home kusalimia nikakuta bi mkubwa anajenga banda la nguruwe basi nikasimamia kidogo mafundi wakawa wamemaliza katika kusafisha mazingira niliokota kopo za energy drink za azam na mo extra zaidi ya 70 na hizo ni zile wanazokunywa wakifika kazini kulikua na mafundi wanne tu kwenye kazi kile kitu kilinishangaza na muda wa kazi ilikua kama wiki mbili na kidogo nikaja kumuuliza fundi mkuu vipi mbona energy nyingi? Akanijibu asee siwezi anza kazi bila chupa moja mchana akila anakunywa au apige soda alafu jioni akifunga kazi lazima apitie dukani anunue moja kwa siku anasukuma 2 mpka 3 asee ni hatari