Nilikutana nae njiani. Alikua pisi kali haswa kalikua mwaka wa mwisho diploma ya ualimu somewhere. Nikamuomba namba tukawa tunachat. Nikamuuliza jina lake akanitajia, Irene. Akaniuliza la kwangu nikamdanganya. Dini nikamdanganya. Tukawa wapenzi. First date akaja kwangu akapika mazaga tukala kisha nikamla na yeye.
Ikawa kila weekend anakuja getto anafua anapika analiwa maisha yanaenda. Vibe kama lote. Alijua ameshapata wa kufanana nae. Mambo yakaanza kua serious sasa. Akaanza kua ananishirikisha mambo ya kwao huko na familia yake. Mzinga pekee anaoomba ni wa kumuunga bundle tu. Mwenyewe nikawa najiongeza akija getto kulala weekend namtoa 50k akawa anagoma, eti niibajeti ktk mambo mengine ya msingi kwa maana yeye hana shida ya pesa anachohitaji mda wangu tu na mapenzi.
Ikabidi mwisho wa siku nimuweke chini. Nikampa makavu. Sina future nae, dini yangu hainiruhusu kuoa mwanamke tofauti na sisi. Nikamtajia na jina langu halisi. Hakushtuka zaidi akauliza kitu gani kingine ulinidanganya? Nikamwambia ni hayo tu. Akalia akasepa zake. Baada ya wiki akahamia mazima getto. Amekomaa anataka kubadili dini nimuoe. Mpaka sasa tunapika tunapakua, soon atanibadilisha cheo ntaitwa baba...