Uongo kuhusu ATCL ni tone tu kwenye bahari, Tumedanganywa mengi tu!

Uongo kuhusu ATCL ni tone tu kwenye bahari, Tumedanganywa mengi tu!

Hapo nimekuelewa. Kwamba kuna kosa lilifanyika kwa kuwa na mandege mengi kuliko uwezo wa kuyahudumia kwa faida. Tungeanza na chache halafu tukawa tunaongeza kadiri ya faida tuipatayo.

yes yes ila sasa kosa limeshatokea hata mkianza kutukana na vijembe haisadii chochote zaidi mapendekezo yangefaa zaidi, yawezekana alikua na nia nzuri ila approach was bad
 
Umuhimu wake uko wapi wakati tunapata hasara? Kwanini izo pesa tusizipeleke kwenye miradi ambayo italeta faida kwa wananchi wote,

Mkuu ivi wewe una akili kweli?

kwahio ukipata hasara ndo kwamba huo mradi hauna umuhimu? kwahio tuanze kungoa reli na zile hospital za kata ambazo huduma nyingi zinatolewa bure tuzivunje pia?
 
yes yes ila sasa kosa limeshatokea hata mkianza kutukana na vijembe haisadii chochote zaidi mapendekezo yangefaa zaidi, yawezekana alikua na nia nzuri ila approach was bad
Halafu ndugu yangu naona mwenyekiti wa UVCCM ndugu Kheri James anaomba radhi kama kuna mahali chama kilikosea au kiongozi anayetokana na CCM alimkosea mtu. Ana maana gani?
 
mangapi mengine amedanganya maana inaonekana we mjuaji sana, tuambie mengine
Hata mi nimeuliza swali tu, Doa moja linatisha kabisa kusababisha shati jeupe lisivalike, Tutazidi kupata majibu mbele kwa mbele subira muhimu
 
Hakuna wizi tena chini ya uongozi wangu. Au nadanganya ndugu zangu?
 
Mimi hii biashara ya ndege kwangu naona zaidi kama ni 'private-centric'. Serikali - tena hasa kama hii ya kwetu, kujihusisha nayo ni kutengeneza matatizo tu ya uharibifu wa fedha za umma.
 
we can call that a weakness ofcourse, uwazi ni muhimu sana
Tumedanganywa mangapi? Bungeni wabunge wa upinzani walipiga kelele kwamba ATCL haipati faida bali ni hasara tu, mbona wabunge wa CCM walikuja juu kwa kelele za TAARIFA na kueleza kwamba shirika linatengeneza faida kama Rais alivyokua akisema, hii ni kusema hawa wabunge wa CCM kuna mengi walikua wanatudanganya kwa lengo la kumkingia kifua Rais na chama chao!!?? Watanzania tuungane tuanze upya hakuna namna. Tumuunge mkono mama.
 
hakuna biashara inaanzishwa apo apo inamke profit, for an airline bussiness its even worse you have to do trial and error nyingi tafauti but you still need to pay your workers.

Sielewi umeandika vitu gani hapa! Yaani ununue ndege kibao then ufanye mchezo wa kubahatisha wa trial & error nyingi?
Kichwa yako itakuwa na tope kidogo.
 
Usisahau hili shirika lilitoa gawaio kwa serikali ikimaanisha ilikuwa ikipata faida
Gawiwo linakikokotoo chake halihusiani na faida uliza ueleweshwe. Tatizo lenu you are overdoing hoja itakapojibiwa mtaaibika maana mnakubaliana na conclusive statements badala ya kutoa room of doubt. Haya endeleeni na sherehe.
 
anaweza kujibu hayo maswali ni yeye mwenyewe but mm i think airlines ni muhimu sana, serikali inaweza kuikumbatia ATCL mpaka ikapata faida
ATCL kupata faida ni kama ndoto tu maana siasa ni nyingi katika uendeshaji. Kwa mfano safari za Chato kama zilikuwepo ni wazi zitakuwa zilikuwa za hasara tu. Sema ATCL inaweza kukumbatiwa kwa malengo ya kuleta faida indirectly. Kwa mfano ikileta watalii ambao labda wangepitia Nairobi nk. Lakini hiyo nayo lazima ipimwe kiutaalamu isije ikazidi kiwango.
Kwa mfano dukani unaweza kuweka pipi si kwa madhumuni ya kupata faida ya kuuza pipi bali kuwagawia watoto ili kila wakitumwa dukani waje kwako, maana yake faida ya pipi inaonekana kwa kuuza mfano mchele zaidi; lakini lazima uangalie isije faida yote ya mchele ikaliwa na pipi!
 
Mambo sasa yanaanza kujianika kwenye mkeka wa uhakika. Ukweli unauzidi nguvu uongo kama mbegu inapochomoza kwenye udongo. Ukweli unaanza kutamalaki kama mashabiki kindakindaki au mwalimu na chaki. Tumedanganywa sana na kwa muda mrefu.

CAG amemwambia Mhe. Rais kuwa ATCL imekuwa ikijiendesha kwa hasara ya mabilioni ya shilingi za kitanzania kwa miaka mitano sasa. Lakini Mwendazake na wenzake wamekuwa wakituamisha kuwa ATCL imekuwa ikijiendesha kwa faida. Katika kuchagiza hilo, ATCL imekuwa ikitoa hadi gawio kwa Serikali. Tulikuwa tukidanganywa.

Serikali ya Mwendazake ilijaa propaganda na uongo mkubwa. Tumeanza kuona upande wa pili wa tulichokuwa tukiambiwa. Ukweli unaupiga kumbo uongo uliotaka kudumu kwa muongo mzima. Amini nawaambia, hilo ni tone tu kwenye bahari ya propaganda zilizokuwa zikiendelea wakati wa uongozi wa Mwendazake. Mengi yanafuata baada ya tuta.

Ndugu yangu Kichere, angekuwepo Mwendazake ungeiwasilisha Ripoti ile inayoanika ATCL na hasara zake?

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)
Mnaanza kujichanganya mapema mnamsema vibaya mwenda zake kwa kujipendekeza kwa mkalia kiti kwa sasa kana kwamba hakuwepo wakati wa uamuzi wa kitu chochote iwe mapato na matumizi.

Mwisho wa siku mtaanza kutakiwa kila mmoja wenu kuthibitisha madai hayo. Anayetakiwa kusimamia na kudhibiti matumizi ni waziri wa fedha na katibu mkuu wake tofauti na hapo mnatafuta mchawi asiyeonekana kwa matendo yasiyo na taswira na matokeo yanayobishaniwa.
 
kwahio ukipata hasara ndo kwamba huo mradi hauna umuhimu? kwahio tuanze kungoa reli na zile hospital za kata ambazo huduma nyingi zinatolewa bure tuzivunje pia?
Ebu niambie hospital ipi ya kata imeleta hasara kwa taifa kama ATCL?

Alafu ebu nitajie faida ya ATCL kwa taifa
 
Gawiwo linakikokotoo chake halihusiani na faida uliza ueleweshwe. Tatizo lenu you are overdoing hoja itakapojibiwa mtaaibika maana mnakubaliana na conclusive statements badala ya kutoa room of doubt. Haya endeleeni na sherehe.
Kama gawio halihusiani na faida ni nini hicho basi ni gawio la mtaji?
 
Na gawio nalo limeibwa sehemu alafu serikali ikajigawia[emoji3][emoji3]
 
Na gawio nalo limeibwa sehemu alafu serikali ikajigawia[emoji3][emoji3]
 
Back
Top Bottom