Nazgur
JF-Expert Member
- Apr 19, 2020
- 3,729
- 2,851
Mzee
Ninachojua ndege hizi kama zimefanya kazi zina miaka miwili na ushee, na ATCL imekuwa ikijiendesha kawa hasara toka ndege zife na ilibaki na madeni amabayo serikari ilikuwa inayabeba,
Kama kulipa wafanyakazi wakiobaki,
Kulipa ghalama za kimataifa na mengine wakati haina ndege.
Sasa hii miaka miwili na kitu hizo ndege zitalipa hayo madeni na kuanza kujiendesha kwa faida?
Kama mnataka kuchambua hiyo taarifa ya CAG Basi leteni hapa taarifa kabla ya ndege ununuliwa kulikuwa na deni la sh ngapi na sasa shirika lina deni la sh ngapi,
Na bado mjue hizo ndege bado shirika linailipa serikari mtaji wake.
Mzee tupatupa kama ripoti ya CAG inasema ATCL imejiendesha kwa hasara ya miaka mitano, je hiyo miaka mitano kulikuwa na ndege ngapi?Mambo sasa yanaanza kujianika kwenye mkeka wa uhakika. Ukweli unauzidi nguvu uongo kama mbegu inapochomoza kwenye udongo. Ukweli unaanza kutamalaki kama mashabiki kindakindaki au mwalimu na chaki. Tumedanganywa sana na kwa muda mrefu.
CAG amemwambia Mhe. Rais kuwa ATCL imekuwa ikijiendesha kwa hasara ya mabilioni ya shilingi za kitanzania kwa miaka mitano sasa. Lakini Mwendazake na wenzake wamekuwa wakituamisha kuwa ATCL imekuwa ikijiendesha kwa faida. Katika kuchagiza hilo, ATCL imekuwa ikitoa hadi gawio kwa Serikali. Tulikuwa tukidanganywa.
Serikali ya Mwendazake ilijaa propaganda na uongo mkubwa. Tumeanza kuona upande wa pili wa tulichokuwa tukiambiwa. Ukweli unaupiga kumbo uongo uliotaka kudumu kwa muongo mzima. Amini nawaambia, hilo ni tone tu kwenye bahari ya propaganda zilizokuwa zikiendelea wakati wa uongozi wa Mwendazake. Mengi yanafuata baada ya tuta.
Ndugu yangu Kichere, angekuwepo Mwendazake ungeiwasilisha Ripoti ile inayoanika ATCL na hasara zake?
Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Dodoma)